Mtazamohalisi

Thursday, November 18, 2010

Unyama Dhidi Ya Wafanyakazi wa Ndani Waingia Sura Mpya

Wapelekea mtikisiko wa kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Indonesia
Imekuwa ni jambo la kawaida kusikia wageni wana nyanyasika hasa wafanyakazi wa majumbani  nchini Saudia.Wengi wa waathirika hao ni wanawake kwa kufanyiwa vitendo vya kinyama, kubakwa na hata kutolipwa ujira wao.
Hivi karibuni niliweka video ikionesha wafanyakazi wa majumbani toka Kenya wanavyonyanyasika nchi Saudi Arabia ,unaweza kuangalia: http://mtazamojamii.blogspot.com/2010/11/wafanyakazi-wa-majumbani.html.


Sumiati
Raia Wa Indonesia aliyejeruhiwa vibaya na muajiri wake nchini Saudi Arabia
Sumiati binti Mustapa Salan.
                                                             
Hivi karibuni hali hiyo iliingia sura mpya baada ya mfanyakazi wa ndani toka Indonesia kuumizwa vibaya na  Muajiri wake Mwanamke raia wa Saudi Arabia.Muathirika Sumiati binti Mustapa Salan  amekuwa mara kwa mara akichomwa kwa chuma na kukatwa katwa kwa mkasi na kusababisha kubambuka kwa ngozi mwilini na kichwani ,kuvunjika kidole cha kati,kukatika kope za macho na kipande cha juu cha mdomo kukatwa.Uso wake ulijeruhiwa vibaya na hata miguu kupooza.

Kadhia hii iligundulika baada ya hospitali moja ya mjini Madina kushindwa kumtibu Muathirika hatimaye kutoa uhamisho katika hospitali ya Mfalme Fahad,kwani Sumiati alihitajika matibabu ya kina kutokana na majeraha makubwa.Sumiati ana miaka 23 na alikuwa ana muda wa miezi mitatu tangu aingie Saudi Arabia.

Kiongozi wa chama cha kutetea haki za wafanyakazi wa kiindonesia Didi Wahyed,amesema"Wanataka haki itendeke kwa wafanya kazi wao.Kwa jinsi muathirika alivyotendewa ni kinyume cha uislamu na ubinadamu.Huku ni kutowajibika kwa wakala wa wafanyakazi na tutamshitaki kwa hili".

Rais wa IndonesiaSusilo Bambang Yudhoyono  amemuamrisha waziri wa mambo ya nje kulishugulikia suala hili ipasavyo na kupeleka kikosi kwenda kuchunguza ukweli mjini Madina,Saudi Arabia na pia kutoa msaada wa kisheria kwa Sumiati kwa kumfungulia mashtaka muajiri wake.
Indonesia tayari imemuandikia balozi wa Saudi Arabia kutaka maelezo zaidi.
Chanzo: http://www.allvoices.com/contributed-news/7348775-sumiati-tortured-by-her-employer-in-medina-her-lips-cut-off-and-nearly-paralyzed.
 http://english.aljazeera.net/news/asia-pacific/2010/11/2010111743123857579.html.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...