Mtazamohalisi

Saturday, December 18, 2010

Pinda Avunja Ukimya Kuhusu Katiba Mpya

Aeleza kuhusu Dowans
Ofisi ya kadhi
Mkataba wa Tido Mhando

Friday, December 17, 2010

Angalia Athari Ya Mabadiliko Ya Hali Ya Hewa

Mashariki Ya Kati(Dec 13,2010)


Ulaya Viwanja Vya ndege ,shule na huduma nyengine zimesimama
(dec 18,2010 )

Cancun Na Kutofikiwa Makubaliano Ya Mabadiliko Ya Hali Ya Hewa

Ikiwa ni muendelezo wa mikutano mingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kama wa Kyoto,Copehagen na kwa mara nyengine  mkutano wa Cancun, Mexico umeendeleza kile kinachoonekana kufeli kwa makubaliano baina ya nchi tajiri na maskini kuhusu upunguzaji wa uzalishaji wa kaboni kwa digrii 4 kabla 2060.

Inasemekana 20% ya uzalishaji wa kaboni dunia inatoka Nchi zinazoendelea kutokana na uchomaji misitu hali nchi zilizoendelea zikiwa vinara wa uzalishaji wa kaboni kutokana na matumizi ya viwanda.

Benki ya dunia kama mdhamini wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani imekutwa na kashfa ya kutokuwa makini katika mambo yake hasa linapokuja suala la uchumi na nchi matajiri.Ni taasisi inayoendeshwa na mataifa tajiri  na kuzinyima sauti nchi maskini kwenye maamuzi makubwa ya uchumi wa dunia.
                   
 

 WIKILEAKS ilipiga msumari wa dau pale ilipotoa kashfa kuhusu nchi matajiri kutumia pesa za kuchangia kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa kwa nchi maskini kama rushwa ili kudhoofisha lengo la nchi tajiri kupunguza uzalishaji wa kaboni. Pesa hizi zinatolewa na nchi tajiri na kusimamiwa na Benki ya dunia,taasisi ambayo nchi maskini hazina imani nayo kutokana na uendeshwaji wake kutokuwa wa kidemokrasia.

Kabla ya mkutano wa Cancun nchi kama Marekani ilitishia kujitoa mkutanoni  kama matakwa yake hayata timizwa,Japan nayo ikisisitiza utekelezwaji wa makubaliano ya Kyoto hali Urusi ikishinikiza kuwa kama Japan haita ahidi  zaidi ya makubaliano ya Kyoto basi na wao hawako tayari.

Ingawa kulikuwa na shinikizo kubwa toka Marekani,nchi zinazoendelea na Ngo's ilikufikia mkataba mwengine unaolingana na ule wa Kyoto.Lakini juhudi hizo hazikuleta mabadiliko yoyote na kubaki kukubalina kutokubaliana.

Ikiwa maafikiano hayatafikiwa ili kutekeleza lengo la upunguzaji wa uzalishaji wa kaboni duniani kwa digrii 4 kabla ya mwaka 2060,watu na viumbe wengi duniani wataendelea kuathirika na mabadiliko ya hali ya hali ya hewa ambayo hawakuya sababisha kutokana na usaliti wa viongozi wao.

Mkataba wa Kyoto ndiyo mkataba rasmi unaotambulikana na umoja wa mataifa. na kutofikiwa makubaliano baina ya nchi tajiri na maskini ,mkataba wa Kyoto unaelekea kufa taratibu.
Chanzo:  Conspiracy

Athari ya mabadiliko ya hali hewa(The day after tomorrow)

Rais Sarkozy amemtaka Gbagbo angatuke

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amemtaka kiongozi aliyeng'ang'ania madarakani nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo aondoke kabla ya mwisho wa wiki, la sivyo atakabiliwa na vikwazo vya Muungano wa Ulaya.

Rais Sarkozy
Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy

Bw.Gbagbo amepinga miito ya Kimataifa ya kung'atuka madarakani kufuatia uchaguzi wa Rais uliomalizika mwezi uliopita.


Yeye pamoja na kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara walidai kuwa wameshinda na kuzusha wasiwasi wa uwezekano wa kuzuka mapigano ya nchini.

Wafuasi wa Ouattara wanasema watafanya maandamano mitaani, siku moja baada ya miliyo ya risasi katika mji mkuu Abidjan.

Rais Sarkozy ameonya kwa kusema kuwa majaliwa ya Bw.Gbagbo na mke wake ni jukumu lao kwa sasa. Na ikiwa ifikao mwisho wa wiki hii hawajaachilia hatamu za uongozi wanaoshikilia kinyume cha chaguo la raia wa Ivory Coast, wataorodheshwa jina kwa jina kwenye orodha ya watu waliopigwa marufuku na Muungano wa Ulaya.

Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani naye amenukuliwa akisema kuwa Bw.Gbagbo amepewa mda wa kutosha aondoke la sivyo atawekewa vikwazo vya kusafiri na pia vikwazo vya fedha zake.

Afisa ambaye hakutambulishwa amesema kuwa Gbagbo na familia yake wana nyumba kadhaa katika nchi nyingi ambako angeweza kuhamia lakini asipotii masharti haya huenda akapoteza fursa hiyo na nyumba hizo kuwa marufuku kwake.

Mwandishi wa BBC amesema kuwa hili litawashangaza raia wengi wa Ivory Coast ambao hawakujua siri hiyo wakimuona Gbagbo kama mzalendo anayepigania na kuipenda nchi yake bila kuwa na mali nje.

Watu ishirini waliuawa siku ya alhamisi wakati wafuasi wa Bw Ouattara walipojaribu kuandamana wakielekea kituo cha televisheni ya Taifa na kukabiliana na vikosi vinavyomtii Bw.Gbagbo.

Msemaji wa Bw.Gbagbo alisema kuwa waandamanaji 10 na askari 10 wa jeshi waliuawa.
Maofisa wa kambi ya Bw.Ouattara walitaja idadi ya wafu kuwa 30 na zaidi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa pande zote mbili zitawajibishwa chini ya sheria ya Kimataifa kwa shambulio lolote dhidi ya raia.

Umoja wa Mataifa pamoja na viongozi wa Umoja wa Afrika na nchi za magharibi wamemuunga mkono Bw.Ouattara kama mshindi wa Uchaguzi uliofanywa huko Ivory Coast.

Chanzo: BBC

Larry King Astaafu Baada Ya Miaka 25 ya CNN-Larry King Live

Atakumbukwa kwa kipindi chake cha mahojiano na watu Maarufu
Maswali yake yaliibua siri nyingi zilizofichika.

Katika muda wa miaka 53 ya utangazaji,King amefanya mahojiano 53000 kati ya hizo 6120 zipo kwenye kumbukumbu za CNN.Amepata tuzo mbalimbali za kuendesha mahojiano na miongoni mwao ni tuzo ya GUINESS kwa kushikilia rekodi ya muda  mrefu ya kuendesha kipindi  na kwa kufata muda .

Akikumbushia jinsi mazingira wakati anaanza kufanya kazi alisema"wakati ninaanza miaka 25 iliyopita katika ofisi ndogo katika jiji la Washington sikudhani kama itanichukua muda mrefu au kumaliza kama hivi".

Larry King atakuwa akiwajibika kwenye shughuli muhimu za CNN.

Zaidi: CNN


Kwa heri Larry King Nyayo zako ni ngumu kuzifuta


Mrithi wake ni Mwandishi wa habari za Udaku wa Uingereza Piers Morgan
Maarufu Marekani kama Jaji wa America's Got Talent

Mwinyi:Kwanini Mnaharakia Katiba Mpya?

Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi amesema haoni umuhimu wa katiba mpya kwa sasa,nakuwataka wanaotoa madai ya katiba mpya kueleza maeneo gani ya kurekebishwa kwenye katiba ya sasa.

Rais Mstaafu,Ali Hassan Mwinyi

Alikuwa akijibu swali kwenye mahojiano na waandishi wa habari lililomtaka kujua msimamo wake juu ya kauli za madai ya katiba mpya.Mwinyi alisema"hakubaliani na wazo la kuwa na katiba mpya kwani kwasasa si muda muafaka".

Alisema"kabla ya kubadili katiba ya sasa,Watanzania wajiulize wenyewe ni kwa manufaa ya nani na kwa lengo gani lakutaka mabadiliko ".Hata hivyo,Mwinyi alisema ipo nafasi ya mazungumzo,lakini akapingana na wale wanaotoa madai ya haraka ,kama vile nchi imekosa kitu muhimu.

  Wakati Mwinyi akiyasema hayo, Profesa Lipumba mwenyekiti wa chama cha CUF amewataka watanzania kuungana katika madai ya katiba mpya. Alisema katiba mpya itasaidia kuwa na demokrasia ya kweli itakayo kuwa msingi kwa muelekeo wa maendeleo ya taifa kwani umuhimu wake kwasasa ni kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Habari kamili ,gonga hapa Guardian

Thursday, December 16, 2010

Fainali Za FIFA CWC 2010 Ni TP Mazembe Vs Inter Milan -Mazembe Fahari Ya Afrika

Fainali itachezwa Jumamosi 18/12/2010
Sherehe kama hii tunaitaka tena


Inter milan 3 vs Seongnam Ilhwa Chunma F.C 0


Wakati huo huoTanzania imepanda chati kwa nafasi nane katika viwango vya ubora wa soka kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa vilivyotangazwa jana.

Hii imetokana na kutwaa ubingwa wa Cecafa Tusker Challenge Cup ambayo yanatambulika na Fifa kama ni miongoni mwa mechi za kirafiki za kimataifa.Habari kamili gonga hapa  Mwananchi

John Tendwa Ataka Katiba Mpya Kabla Mambo Hayajaharibika


Msajili wa vyama vya siasa,John Tendwa
Mwangwi wa kudai katiba mpya umezidi kusikika kila kona ya nchi baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa juzi kuvunja ukimya na kusema kuwa iundwe katiba mpya sasa kabla mambo hayajaharibika. Msajili huyo, ambaye ni mwajiriwa wa Serikali, alionyesha ujasiri mkubwa juzi aliposema bila kutafuna maneno kuwa kinyume na katiba iliyopo sasa, katiba mpya inayotakiwa lazima itokane na mapendekezo ya mkutano wa kitaifa wa kikatiba utakaojumuisha watu wa kada mbalimbali.

Kauli hiyo ya mlezi wa vyama vya siasa nchini ni nzito mno, kwa maana ya kutolewa na mtu mwenye mamlaka ya kusimamia shughuli za vyama vilivyoanzishwa kisheria mwaka 1992 kufanya kazi za siasa zenye lengo la kutoa changamoto kwa chama kilicho madarakani. Kauli kama hiyo inapotolewa na kiongozi wa juu serikalini inaifanya serikali yenyewe ione umuhimu wa kutafakari kwa kina madai ya kuwapo katiba mpya ambayo yametolewa na kada mbalimbali nchini mwetu.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TDC), Tendwa alisema kuwa katiba ya sasa ya Tanzania pamoja na nchi nyingine katika Afrika Mashariki bado zina misingi ya kikoloni na akaongeza kuwa maendeleo yaliyopo katika nchi hizo pengine yangekuwa makubwa zaidi iwapo nchi hizo zingekuwa na katiba zinatokana na matakwa ya wananchi wenyewe.

Msimamo huo wa Msajili unakuja siku chache baada ya viongozi wa ngazi za juu, wakiwamo mawaziri wakuu wastaafu, majaji, wanasheria, vyama vya siasa na wanaharakati kusema kuwa katiba iliyopo sasa haikidhi mahitaji ya sasa, hivyo lazima iandikwe upya kwa kuzingatia matakwa ya wananchi walio wengi.

Msimamo wa kiongozi huyo pia umekuja muda mfupi baada ya Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani kusema kuwa serikali haina fedha za kuandika katiba mpya, hivyo zoezi la kuifanyia marekebisho katiba iliyopo litaendelea kufanyika pale tu unapokuwapo umuhimu wa kufanya hivyo. Alisema wanaodai katiba mpya ni watu wa barabarani ambao alidai hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya katiba na sheria.

Ndio maana tunasema kuwa katika mazingira hayo, kauli ya Tendwa ambaye pia ni mwanasheria na mwajiriwa wa serikali hiyohiyo iliyomwajiri Waziri Kombani, ni nzito kiasi cha kuibua maswali mengi kuhusu iwapo Serikali ya Rais Kikwete na chama chake cha CCM vina msimamo wa pamoja juu ya suala hilo, kwani wengi wanajiuliza hivi sasa iwapo kweli msimamo wa waziri huyo kuhusu kuwapo au kutokuwapo umuhimu wa katiba mpya ni wa chama chake na serikali yake au ni wake binafsi.

Utata kuhusu suala hilo umezidishwa na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, John Chiligati ambaye aliliambia gazeti dada la The Citizen juzi kuwa chama hicho kiko tayari kukaa na vyama vya upinzani kuzungumzia suala hilo, lakini akaonya kuwa vyama hivyo vipeleke mapendekezo thabiti badala ya kile alichokiita ‘blabla za kisiasa’ alizodai zinafanywa na vyama hivyo hivi sasa.

Sisi tunadhani kuwa kauli hiyo ya Chiligati inathibitisha kuwapo tatizo moja kubwa ndani ya chama chake. Tatizo hilo ni CCM kudhani kuwa katiba iliyopo hivi sasa ni mali yake na yeyote anayezungumzia kuifuta na kuandika mpya ni adui mkubwa anayekitakia chama hicho maangamizi makubwa. Ni dhana itokanayo na kile Jaji Mark Bomani anachokiita woga usio na msingi wa chama hicho kupoteza madaraka.

Ndio maana tunasema kuwa tunahitaji viongozi katika CCM au Serikali yake kama Msajili John Tendwa asaidie kuwafafanulia na kuwatoa hofu viongozi wa chama hicho kwamba katiba iliyopo ni ya wananchi wote na kwamba kuandika katiba mpya itakayokidhi matakwa ya wakati huu kutaepusha utengano na machafuko katika siku za usoni.
Chanzo:  Mwananchi

Wednesday, December 15, 2010

Sherehe Za Ashura Zageuka Mauaji

Mauaji ya kujitolea Muhanga
Zaidi Ya watu 35 wauawa

Zaidi ya watu 35 wameuawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua wakati waumini wa kishia walipokuwa kwenye shughuli zao kwenye mji wa Chabahar kusini mashariki mwa Iran.

Afisa wa Shirika la Hilali nyekundu Mahamoud Mozafar amesema mshambuliaji huyo alijiripua katika eneo la kati ambapo waumini hao walikuwa wakifanya ibada ya kuadhimisha siku ya mwisho ya Ashura.

Kundi la Jundallah limedai kuhusika na shambulio hilo.Kundi hilo katika kipindi cha muongo mmoja uliyopita limekuwa likihusika na mashambulio kadhaa dhidi ya vikosi vya usalama nchini Iran.

Mkuu wa kamati ya mambo ya Nje ya Bunge la Iran Alaeddin Borujerdi amezishutumu idara za kijasusi za Uingereza na Marekani kuhusika na shambulio hilo.

Mjini London Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Alistair Burt amesema ameshtushwa na shambulio hilo na kwamba inalaani vikali.
Chanzo: Dw

World Club Championship-TP Mazembe Yatinga Fainali

Yaifunga Internacional Ya Brazil 2-0
Timu Ya Kwanza Toka Afrika Kutinga Fainali
Yasubiri Mshindi Baina ya Inter milan na Seongnam Ilhwa(Korea kusini)

Mambo yalijiri kama hivi

ICC yataja watuhumiwa wa ghasia Kenya

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - International Criminal Court (ICC) imetaja majina ya Wakenya sita anaowatuhumu kuhusika kupanga vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu nchini humo mwaka 2007.

Ghasia baada ya uchaguzi mkuu Kenya
 Ghasia baada ya uchaguzi mkuu Kenya
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta, ni mmoja ya waliotajwa.

Takriban watu 1,200 waliuawa na zaidi ya wengine 500,000 walizihama nyumba zao kufuatia ghasia hizo.

Siku ya Jumatatu Rais Mwai Kibaki, alitangaza serikali itaendesha uchunguzi wake, hatua ambayo wapinzani wake wameiona ni sawa na jaribio la kuzuia watuhumiwa kupelekwa The Hague.

Ghasia hizo zilizuka baada ya wafuasi wa Bw Kibaki, kutuhumiwa walijaribu kuvuruga uchaguzi.
Uhasama huo ulimalizika baada ya Bw Kibaki na mpinzani wake kisiasa Raila Odinga walipokubaliana kuunda serikali ya mseto na Bw Odinga akawa Waziri Mkuu.

Waziri wa Viwanda Henry Kosgey, naye ametajwa na Bw Ocampo.
Waziri wa Elimu aliyesimamishwa William Ruto, Mkuu wa uendeshaji wa Radio Kass FM, Joshua Arap Sang, katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kirimi Muthaura na na Mkuu wa zamani wa jeshi la polisi Mohammed Hussein Ali, nao majina yao yametajwa na Bw Ocampo.

Polisi nchini Kenya wamewekwa katika hali ya hadhari iwapo baada ya kutangazwa majina hayo kunaweza kuibuka ghasia mpya.


Kila mmoja kati ya hao sita, watatumiwa hati ya kuitwa mahakamani, lakini wakigoma au wakijaribu kuingilia uchunguzi, mathalan kuwatisha mashahidi, Bw Ocampo amesema ataomba kibali cha hati ya kuwakamata.

Swali lililopo ni iwapo waliotuhumiwa hao watajisalimisha au watawekewa kinga na wanasiasa na kukwepa mkono wa sheria.

Katika taarifa yake baada ya tangazo hilo la Bw Ocampo, Rais Mwai Kibaki amesema ana matumaini Mahakama hiyo ya Kimataifa, mchakato wake utatimiza wajibu wake kwa maslahi ya taifa la Kenya.

Rais Kibaki amesema, kama taifa ni lazima walenge mahitaji ya taifa ya maridhiano na kusameheana.

Amewahakikishia Wakenya kwamba serikali imeimarisha ulinzi nchi nzima.
Chanzo: BBC

Tuesday, December 14, 2010

Sepp Blatter awaasa mashoga Qatar 2022

Rais wa Fifa Sepp Blatter, ametania kwamba mashabiki wa soka ambao ni mashoga watakaokwenda kwenye Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar, hawana budi "kujizuia kufanya mambo yao ya ngono."

Sepp Blatter
Rais wa Fifa,Sepp Blatter

Makundi ya kutetea haki za mashoga, wameshutumu uamuzi wa kupeleka mashindano hayo ya Kombe la Dunia katika nchi ambayo ushoga ni marufuku.

Lakini Blatter, akatania kwa kusema: "Ningependa kusema, mashabiki wa soka walio mashoga, wajizuie na mambo yao watakapokuwa Qatar."


Na katika taarifa ambayo ni kali zaidi, Blatter amesema: "Nina hakika wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia yatakapofanyika Qatar, hakutakuwa na matatizo."

Hata hivyo mchezaji nyota wa zamani wa NBA John Amaechi, ambaye alijitangaza rasmi kuwa shoga mwaka 2007, ameshutumu vikali kauli hiyo ya Blatter.

Qatar ambayo ni nchi ya Kiislamu, ilipata nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2022, wakizishinda Australia, Japan, Korea Kusini n Marekani, wakati wajumbe wa kamati ya utendaji ya Fifa walipopiga kura tarehe 2 mwezi huu wa Desemba.

Tangu wakati huo Fifa imekuwa ikishutumiwa kutokana na uamuzi wao wa kupeleka mashindano hayo kwa mara ya kwanza eneo la Mashariki ya Kati.

Wasiwasi umeibuka kuhusu kuandaa mashindano hayo wakati wa miezi ya kiangazi katika nchi ambayo joto linakuwa la kiwango cha juu cha nyuzi joto 40 vipimo vya centrigrade hadi nyuzijoto 50, huku sheria ikikataza unywaji wa pombe hadharani.

Makundi ya kutetea haki za mashoga na mashoga wenyewe, pia wameonesha wasiwasi wao kuhusiana na kuruhusiwa watu wanaoendekeza vitendo hiyo wanaopenda soka, kwenda Qatar na wamelaani uamuzi wa Fifa na wametangaza kususia shughuli zote zinazohusiana na Kombe la Dunia mwaka 2022.
Chanzo : BBCRais Jakaya Kikwete Ahidi Kuinua Kiwango Cha Michezo Tanzania

Apokea kombe la ubingwa wa tusker challenge cup 2010
Afanya tafrija ya chakula cha mchana na wachezaji na viongozi
wa tff
Atunukiwa tuzo ya TASWA kwa mchango wake katika michezo


Hivi ndivyo Kilimanjaro Stars walivyowapa raha wa Tanzania

Maalim Seif: Pelekeni madai yenu Mahakama ya Afrika


Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
Seif Sharif Hamadi

Watanzania, jumuia za kiraia na mashirika mbalimbali yameaswa kupeleka mashauri yao katika Mahakama ya Afrika inayoshughulika na haki za binadamu iliyoko jijini Arusha, pale wanapohisi kuwa haki zao za kibinadamu zimekiukwa.


Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, alipokuwa akifungua semina ya uhamasishaji wa jumuia za haki za binadamu nchini, iliyoandaliwa na Mahakama ya Afrika kuhusu haki za binadamu kwa kushirikiana na serikali na Jumuia ya wanasheria nchini (TLS).
Alisema mahakama hiyo inapewa mamlaka na protokali yake, kuipa nguvu Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu ili kulinda haki za watu na za makundi Afrika, kwa kutoa hukumu za kukazia na mamlaka ya kutoa ushauri pale inapoombwa na nchi mwanachama,AU yenyewe,chombo chake au chombo inachokitambua.

“Ndiyo maana nasema raia katika ujumla wao,jumuia za watu na ,makundi mbalimbali yawasilishe mashauri yao katika mahakama hii pale wanapohisi kutotendewa haki na mamlaka yeyote ile”alisema.

Hamad alisema kuwa pamoja na mahakama hiyo kuwa tayari kupokea mashauri toka mwaka 2008,inasikitisha kuona kwamba mpaka sasa imeshapokea shauri moja tu,kitu ambacho hakikubaliki.

Naye Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Gerard Niyungeko, aliviasa vyombo vya habari kujikita katika utoaji wa habari zilizo sahihi,kama zilivyo zenye kuhabarisha na zilizotolewa kwa wakati kuhusu matukio na maendeleo ya ulimwengu,kwa kuwa bila ya kufanya hivyo jamii itabaki bila ya kuhabarishwa au ikapata habari zilizopotoshwa.
Chanzo: Nipashe

Monday, December 13, 2010

EPL: Men Against Boys

Man United 1 Vs Arsenal 0


Chelsea held to a Draw by Spurs


Liverpool no comment


Spain Premera division
Barca Threats


Madrid business done

Ahmadinejad amfuta kazi Mottaki

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amemuachisha kazi Waziri wa Mambo ya Nje Manouchehr Mottaki Jumatatu, wakati waziri huyo akiwa kwenye ziara huko Senegal.

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amemuachisha kazi Waziri wa Mambo ya Nje Manouchehr Mottaki Jumatatu, wakati waziri huyo akiwa kwenye ziara huko Senegal.

Bwana Ahmadinejad alimuachisha kazi Mottaki Jumatatu na kumteuwa mkuu wa nyuklia nchini Iran, Ali Akbar Salehi kama waziri mpya wa mambo ya nje kwa sasa. Shirika rasmi la habari la Iran Mehr linaripoti kwamba Bwana Ahmadinejad alituma barua kwa Mottaki akimshukuru kwa kazi yake.

Salehi anajulikana kama mshirika wa karibu wa rais. Zaidi ya mwaka mmoja uliopita vyombo vya habari vya Iran viliripoti mifarakano kati ya Mottaki na wabunge wa Iran. Ripoti hizo zilisema wabunge wa Iran walisema kwamba Mottaki hakuwa mahiri au mwakilishi shupavu kwa Iran kwenye jukwaa la kimataifa.

Walimshinikiza Mottaki kujiuzulu kama vikwazo zaidi vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa vingewekwa katika kujibu program ya nyuklia ya nchini humo, na mzunguko wa nne wa vikwazo hivyo viliwekwa mwezi Juni. Duru za kimataifa zinaonesha vikwazo hivyo vinaharibu mno uchumi wa Iran.

Chanzo: Voa

Zitto,Shibuda Waundiwa Kamati


Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe, akijuliwa hali na mbunge
wa Maswa Magharibi, John Shibuda, wakati alipolazwa katika hospitali
ya Agha Khan jijini Dar es salaam

WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikitarajiwa kutoa msimamo wa chama hicho juu ya masuala mbalimbali ikiwemo hali ya kisiasa nchini na ndani ya chama hicho, imeelezwa kuwa Mbunge wa

Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe ametakiwa kujipima mwenyewe kisha ajiuzulu, baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge wa chama hicho.

Imeelezwa kuwa kura za kutokuwa na imani naye, zilizopigwa wiki iliyopita na wabunge wa CHADEMA katika kikao cha kamati yao, kilichofanyika Mjini Bagamoyo, hakizumwondoa moja kwa moja katika cheo chake cha naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, bali ilikuwa ni ishara ya kuwa watu anaowaongoza bungeni hawana imani naye tena hivyo kumtaka afikirie mwenyewe kisha achukue uamuzi wa kujiuzulu kabla wabunge hao hawajachukua hatua za kinidhamu juu yake.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zimebainisha pia kuwa Kamati Kuu iliyoketi mwisho wa juma katika kikao maalumu, imeunda kamati kwa ajili ya kumshauri Bw. Zitto, baada ya wajumbe kuona kuwa kuna umuhimu wa kumsaidia ushauri nasaha kutokana na mwenendo wake ndani ya chama hicho.Vyanzo mbalimbali vimesema kamati hiyo inajumuisha Profesa Mwesiga Baregu, Dkt. Mkumbo Kitila, Shida Salum na mwanachama mwingine wa chama hicho.

Mbali ya kubainika kwa suala hilo, pia habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika zimeeleza kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA, imeunda kamati nyingine kumchunguza Mbunge wa Maswa Magharibi, Bw. John Shibuda, kutokana na tuhuma zilizowasilishwa na kamati ya wabunge, iliyokutana wiki
iliyopita Mjini Bagamoyo.

"Nafikiri hilo la Zitto waandishi wamwelipotosha kwa kiasi kikubwa, mimi ninavyojua walichofanya wabunge wale ni kupiga kura ya kutokuwa na imani naye (Zitto), kisha mwenyewe apime uzito wa uamuzi huo kuwa watu anaowaongoza hawana imani naye, kisha mwenyewe ajiuzulu, kabla wabunge wenyewe hawajachukua hatua za kinidhamu juu yake.

"Hata hivyo uamuzi huo wa kuchukua hatua za kinidhamu ikiwemo hata kumwondoa katika cheo hicho, imo katika mamlaka ya Kamati ya Wabunge wa CHADEMA, yaani Party Caucus, wanayo mamlaka hayo kabisa wakiona kuna haja ya kufanya hivyo, baada ya yeye kushindwa kuchukua hatua yoyote hasa kujiuzulu maana ni kiongozi wao wenyewe, hivyo haihusiani na chombo kingine ndani ya chama."Kumbuka pia kuwa naye ataitwa kama alivyoitwa wengine kuhojiwa juu ya kutotekeleza maamuzi halali ya kikao ya kuingia ukumbini siku ya ufunguzi wa bunge kama

ilivyokuwa imeamuriwa...lakini cheo hajavuliwa, mwenyewe apime kisha ajiuzulu," kilisema moja ya chanzo chetu cha habari.

Chanzo chetu kikiwa na tahadhari ya kutotaka kufafanua masuala mengi, pia kilisema kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA imeona kuna umuhimu kukaa na Bw. Zitto kisha apatiwe ushauri juu ya mwenendo wake wa kisiasa akiwa kama mmoja wa viongozi waandamizi wa chama hicho, ambapo mbali ya kuwa ni naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni pia ni naibu katibu mkuu wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara.

Nafasi hiyo ya naibu katibu mkuu bara, inamfanya kuwa mmoja wa watu wawili wanaomsaidia Katibu Mkuu Dkt. Willibrod Slaa, mwingine akiwa ni Hamad Mussa Yusuf, kwa Zanzibar, lakini nafasi ya naibu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, inamfanya kuwa msaidizi wa Mkuu wa Kambi, Bw. Freeman Mbowe.

Kwa upande wa suala la Bw. Shibuda, vyanzo vyetu vilieleza kuwa mbunge huyo ambaye alihamia CHADEMA kutoka Chama Cha Mapinduzi, siku chache kabla ya kampeni za uchaguzi kuanza, baada ya kubwagwa katika kura za maoni, atachunguzwa kwa tuhuma kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutotii maagizo na maamuzi kikao halali cha chama, kulaumu na kulalamikia nje ya chama maagizo na maamuzi hayo, kujaribu au kutaka kuleta mgawanyiko ndani ya chama.

"Bw. Shibuda alisema hana kosa wala hana haja ya kuomba msamaha, chanzo hicho kilisema wabunge walikuwa wazi kabisa kwake, wakimwambia asifikiri wanamwogopa, asifikiri kuwa wao hawakushinda uchaguzi...maana amekuwa akijigamba kuwa yeye ametumwa na watu wa Maswa.Juhudi za gazeti hili kuwapata viongozi wa chama hicho kuzungumzia taarifa hizo hazikuzaa matunda jana.

Chanzo: Majira

Raza:Dhambi Ya Ubaguzi Yaitafuna CCM Z'bar


 Mfanyabiashara maarufu na kada wa CCM-Zanzibar
Bw.Mohamed Raza

MFANYABIASHARA maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar, Bw. Mohamed Raza amekitahadharisha chama hicho kuwa kitatoweka visiwani humo endapo hakitarekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa

Oktoba 2010.

Alisema hayo alipokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana wakati akitoa tathmini yake kuwa ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huo haukuwa wa kishindo kama walivyotarajia, kwani asilimia 50 na nukta kidogo walizopata ni dalili mbaya.

Alitoa mfano kuwa miaka ya nyuma CCM kilikuwa na majimbo Pemba, sasa hakuna hata moja na pale Zanzibar hivi sasa majimbo manne yamechukuliwa na wapinzani wao na kuongeza kuwa kama chama hakitakuwa wazi kuelezea yaliyojiri, basi Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 kwa upande wa Zanzibar wasishangae majimbo zaidi yakaangukia upinzani kitendo kitakachofanya chama chao kuambulia nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

"Kwa kuwa Uchaguzi Mkuu ujao hauko mbali, basi ni vyema chama kikakaa chini na kufanya tathmini ya kina na kwa uwazi kikihusisha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ili kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza", alisisitiza Bw. Raza.

Bw. Raza alionesha kushangazwa na kutoshirikishwa kwa viongozi wastaafu wa Zanzibar katika mchakato mzima wa uchaguzi. Alisema tangu ufunguzi wa kampeni za uchaguzi visiwani humo hadi kumalizika hakuna kiongozi aliyepewa nafasi kuhutubia mikutano hiyo.

Alisema hata kiongozi aliyepangwa katika ratiba kuhutubia moja ya mikutano hiyo, ratiba hiyo ilifutwa na viongozi wenyewe wa CCM bila sababu za msingi.

Aliutaka uongozi wa chama hicho visiwani humo kuwaeleza wanachama wao kwa nini walifanya hivyo na kusisitiza kuwa viongozi wastaafu wana nafasi zao.Akizungumzia usawa, Bw. Raza aliitaka CCM na SMZ kutenda haki kwa viongozi wote wastaafu, kinyume cha hivyo kitakuwa kinatayarisha na kuunda matabaka ya viongozi hao.

Alisema haoni sababu kwa nini kati ya viongozi hao wastaafu wengine wawe na magari ya kuwaongoza na wengine wasiwe nayo; wengine wapewe magari aina ya benz na wengine wasipewe.Alisisitiza kuwa katika CCM hakuna bwana mkubwa wala umaarufu wa mtu, bali chama wanachokitumikia na kusisitiza kwamba asingetaka kuiona Zanzibar yenye matabaka ya wastaafu na ili kuondokana na hilo katiba ya nchi na sheria zifuatwe katika kuteleza usawa huo.

Awali, Bw. Raza alitoa shukrani na pongezi kwa ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na hasa Zanzibar ambako baadaye kuliundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyojumuisha Chama cha Wananchi (CUF).Bw. Raza alisema serikali hiyo isibezwe wala kupuuzwa ili kudumisha hali ya amani na utulivu visiwani humo.
Chanzo: Gazeti la Majira

DK. REMMY ONGALLA AFARIKI DUNIA


 Marehemu Ramadhani Mtoro Ongala


Aliyewahi kuwa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchi, na baadaye kuokoka na kuhamia katika muziki wa Injili, Dk. Remmy Ongala, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa amelazwa kwa kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Marehemu Remmy ambaye alikuja nchini mwishoni mwa miaka ya 70 na kujiunga na bendi ya Makasy, amechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa dansi hapa nchini akiwa na bendi hiyo na baadaye Super Matimila.

Wimbo wake wa Pesa ambao alitumia mtindo wa Talakaka, ulivuma sana mwanzoni mwa miaka ya 80 na baadaye wimbo wa Tembea Ujionee.

Mwanamuziki huyo alipata sifa kubwa na kupata mwaliko wa kwanza kutumbuiza katika tamasha la Womad nchini Uingereza.

Dk. Remmy atatakumbukwa sana na nyimbo zake nyingine kama safari siyo kifo, Kifo, Dodoma, kipenda roho na nyinginezo nyingi.

Maandalizi ya mazishi yanaendelea kufanyika nyumbani kwake, Sinza kwa Remmy. Mungu amlaze mahali pema, Amen.

Dk.Che mponda akiongea na mke wa Dk.Remmy Ongalla alipokweda
kumtembelea.Mumewe,Dk Remmy naye alilazwa hapo Mwaisela.
(ilikuwa tar.3/desemba/2010,Dk Remmy aliruhusiwa kutoka hospital)

Sunday, December 12, 2010

Kilimanjaro Stars Bingwa Mpya Kombe La Tusker Chalenge 2010

Yaifunga Ivory Coast 1 Nunge
Sasa Si Kichwa Cha Mwendawazimu
Hongera Kocha Mpya Jan Poulsen
Hongera TanzaniaKikosi cha ushindi cha Kilimanjaro stars

 Kikosi Cha Ivory Coast

Nahodha wa Kili Stars,Shadrack Nsajigwa akifunga bao la penalti.
Bao la ushindi,bao la Tanzania mpya katika ulimwengu wa soka

Tupo pamoja tukikirudi kiduku-licha ya kutocheza kwa kuwa na kadi
mbili za njano Mrisho Ngasa alijumuika kunyimwaga na wenzake

Kipa wa Kilimanjaro Stars Juma Kaseja akionesha tuzo yake ya
kipa bora wa Tusker challenge 2010


Kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars,Jan Poulsen akimshika mwari
pamoja na nahodha wake Shadrick Nsajigwa.Kikosi kizima cha
Kilimanjaro Stars bingwa mpya kombe la Tusker Challenge 2010
katika picha ya pamoja.Stars wameibuka na kombe na kitita cha
US$ 30000/= -hongera Kilimanjaro Stars,Hongera Tanzania.

Picha kwa hisani ya
(Michuzi na Sufiani Mafoto).
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...