Mtazamohalisi

Saturday, January 29, 2011

Sauti Ya Umma Wa Misri

Cliton on Egypt ptotest


OBAMA ON EGYPT PROTEST


Mubarak avunja baraza la Mawaziri na kutangaza Mabadiliko

Sauti Ya Amerika na Mabadiliko Misri


Waandamanaji wakionesha hasira zao kwa Utawala wa Mubarak

Ilikuwa ni Ijumaa nzito kwa kipindi cha miaka  30 cha utawala wa Hussein Mubarak(82), siku ambayo wingu la mabadiliko ya siasa ulipofunga na kusababisha mpasuko wa radi uliotingisha si tu utawala wa Misri bali na tawala nyengine duniani.

Haikuwahi Mji wa Cairo kuwa moto tangu mapinduzi ya mwaka 1952,lakini mshuko wa Ijumaa wa january 28,2011 ulithubutu kuvunja duru za usalama za nchi hiyo na kuonesha dunia kile ambacho wanakipigania yaani mabadiliko.

Imetosha, ni kauli kuu ya waandamanaji kuashiria kukata tamaa na mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa na kijamii. Hali mbaya ya maisha kutokana na ukosefu wa ajira,gharama za maisha kupanda na uhuru wa kujieleza,rushwa na uasimu ndio vichocheo vilivyoamsha umma wa Misri na kumtaka Mubarak kuondoka madarakani.

Mwezi desemba Misri ilifanya uchaguzi wa wabunge wa duru ya pili na chama tawala cha National Democratic Party (NDP)   kujipatia ushindi mnono wa 80% na upinzani kujipatia 20%.Hata hivyo kelele za kubatilisha matokeo hayo ambayo upinzani ulisusia toka duru ya kwanza ya uchaguzi mwezi novemba linalifanya bunge hilo kuwa ni la chama kimoja bila mwakilishi toka upinzani.

Hapo jana utawala wa Marekani  ambao ni mshirika mkuu wa utawala wa Mubarak ambayo hutoa kiasi cha Dola 1.5 bilioni kila mwaka, umeitaka Misri kuheshimu uhuru wa kujieleza na kuruhusu maandamano,pamoja na kuwaacha huru waandamanaji na kuruhusu mitandao kufanya kazi huku ikiisisitiza Misri kusikiliza kilio cha Umma na kukubali mabadiliko.

Kutokana na shinikizo la ndani na nje ya nchi,Rais Mubarak ametangaza kulivunja baraza lake la Mawaziri na kuunda jipya hali yeye akiwa bado kiongozi mkuu atakae endeleza mabadiliko ya nchi katika muelekeo wa Misri Mpya.

Septemba,2011 kutakuwa na uchaguzi wa Rais wa Misri ambao kwa hali ilivyo upepo wa siasa unaelekea kuwa mbaya kwa Mubarak na chama chake.

Friday, January 28, 2011

Mganda Atumia Kigezo cha Ushoga Kudai Haki Ya Ukimbizi

Hatua kali ya sheria ya ushoga nchini Uganda kumempelekea Brenda Namigadde,mwanamama wa kiganda kuiomba serikali ya Uingereza kumfikiria kupata haki ya ukimbizi kuliko kurudishwa nchini Uganda.

Kwa mujibu wa mwanamama huyo ambaye amedai ni Msagaji na kwamba ni uvunjaji wa sheria nchini kwake kuwa na uhusiano wa jinsia moja hivyo kurejeshwa kwake kutahatarisha maisha yake.

Kwa mujibu wa sheria ya Uganda, ni marufuku kuwa na uhusiano wa mapenzi na mtu wa jinsia moja na yeyote atakae vunja sheria hukumu yake ni miaka 14 licha ya juhudi kubwa kugonga ukuta kwa baadhi ya wabunge waliofika mbali nakutaka "hukumu ya kifo" itumike.

Wiki hii nchini Uganda imeshuhudia mtetezi mkuu wa haki za mashoga David Kato  akiuawa na mtu asiyejulikana mara baada ya kuvamiwa nyumbani kwake,nakifo chake kimeibua hisia za watetezi wa haki za binadamu na wapenzi wa haki za mashoga kuhofia usalama wao.

Kwa mujibu wa hukumu ya Bi.Brenda Namigadde, wizara ya mambo ya ndani imeshindwa kujiridhisha na ushahidi alioutoa kwa kuwa hana vidhibitisho kuwa yeye ni Msagaji.Hivyo madai yake batili.

Hata hivyo Bi Breanda Namigadde amekata rufaa na kupeleka vielelezo zaidi ili kuiridhisha idara ya mambo yandani ya Uingereza ambayo imevipokea na kuanza kuvipitia.

Ikiwa ushahidi hautotesheleza vigezo kwa mujibu wa sheria ya Uingereza ,basi muhusika itampasa kufunga virago.

Umoja wa mataifa kupitia kamishna wake wa masuala ya wakimbizi Bw.Antonio Guterres amenukuliwa akizitaka mamlaka za kimataifa kuwapokea wakimbizi toka Uganda waliokimbia kutokana na maisha yao kuwa hatarini.
Chanzo:  BBC

Video ya David Kato kabla na baada ya Mauaji yake

Thursday, January 27, 2011

Mlinzi wa Hitler Bado Wamo


Rochus Misch mlinzi wa Hitler kwa muda wa miaka 5 alishuhudia
Hitler akijiua.

Zaidi ya miaka 65 tangu kwisha kwa vita ya pili ya dunia mlinzi wa mwisho wa Hitler anasema kwa hivi sasa hawezi kujibu e-mails kutokana na umri wake.

Rochus Misch,miaka 93 alishuhudia Hitler akijiua mara baada ya kuona kifaru cha jeshi la Urusi kimkaribia.Aliwahi kubadilishana uzoefu na Christopher McQuarrie,mwandishi aliyetengeneza Valkyrie filamu ya mwaka 2008 ikielezea jinsi Hitler alivyojiua.

Mcheza sinema wa Hollywood ,Tom Cruise ambaye aliigiza katika filamu hiyo hakutaka kukutana na Misch na kuliambia gazeti la Los Angeles Times kuwa"shetani ni shetani,haijalishi umri aliokuwa nao".

Amenukuliwa na gazeti la Berliner Kurier ya kwamba hawezi kujibu barua pepe anazotumiwa kutokana na umri aliokuwa nao.

Mwezi January 16 ,1945 kufuatia Ujerumani kushindwa vitani Misch na wasaidizi wa karibu wa Hitler walikimbilia Führerbunker katika jiji la Berlin. Nakujitokeza kwake mara baada ya vita, alijikuta akitiwa mikononi na Jeshi Jekundu . Aliachiwa huru mwaka 1954, na tangu wakati huo na hadi sasa Misch anaishi katika jiji la Berlin.

Kwakujua alivyokutana na Hitler na majukumu yake endelea......Hitler

Watch Valkyrie Trailer

Hitler Private resident

Wednesday, January 26, 2011

Waarabu Wataka Mabadiliko

        Tunisia yataka Ben Ali akamatwe          
Waziri wa sheria wa Tunisia amesema nchi hiyo imetoa hatia ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais aliyekimbia Zine al-Abidine Ben Ali na familia yake.


Lazhar Karoui Chebbi alisema Tunisia imeiomba shirika la polisi la kimataifa Interpol kumkamata Ben Ali, aliyekimbilia Saudi Arabia mapema mwezi huu kufuatia maandamano makubwa nchini humo.

Bw Chebbi alisema Bw Ben Ali ashtakiwe kwa wizi wa mali na kuhamisha patoa la taifa la fedha za kigeni.

Aliyasema hayo huku maandamano ya kuipinga serikali yakiendelea.

Chanzo: BBC

Maandamano Tunisia
Nyumba Ya Familia Ya  Rais Ben Ali  Yavamiwa


Mitandao imerahisisha sauti ya Umma


Misri kwafuka Moto Licha Vitisho Vya Serikali
kwa kuweka waandamanaji 500 kizuizini nakuua 4
 Marekani  Yaitaka Misri kuruhusu Maandamano
 

Palestina yajibu kuhusu 'nyaraka za siri'

Maafisa wa Palestina wameishutumu al-Jazeera kwa kupotosha, baada ya kutoa taarifa za siri zilizokusudia kuonyesha nchi hiyo kuwa na maridhiano makubwa na Israel.

Rais Mahmoud Abbas alisema siri hizo zimechanganya kwa makusudi misimamo ya Palestina na Israel.

Nyaraka hizo zinasema kuwa Palestina iliikubalia Israel kubaki na eneo kubwa la mashariki mwa Israel wanalomiliki kinyume cha sheria- jambo ambalo Israel imelikataa.

BBC imeshindwa kuthibitisha binafsi nyaraka hizo.

Al-Jazeera ilisema ina rekodi 16,076 za siri za mikutano, barua pepe, na mawasiliano baina ya Palestina, Israeli na viongozi wa Marekani, baina ya mwaka 2000-2010.

soma zaidi....... BBC

Kupitia Nyaraka zenyewe gonga hapa http://english.aljazeera.net/palestinepapers/

Maoni Ya Wachambuzi

Undugu Wamtoa Machozi Oprah Winfrey


Kwa muda wa miaka 25,mwanamama  Oprah Winfrey amebahatika kuwaunganisha watu mbali mbali katika kipindi chake maarufu cha Oprah show .

Lakini safari hii imekuwa kwa upande, katika hali ya kushangaza amejikuta anakutana na dada yake wa mama mmoja ambaye alichukuliwa kimalezi wakati yeye akiwa miaka 8.

Kwa kiasi fulani tukio hili litamliwaza Mama huyu kwani kwa kipindi kirefu alikuwa ana dai yakuwa ana asili ya Kizulu kutokana na vipimo vya DNA, hali wakuu wa kabila hilo lililopo nchini Afrika kusini wakikanusha kwa vizazi vyao kuchukuliwa utumwa kwenda Marekani.

Monday, January 24, 2011

Aljazeera kama Wikileaks Yatoa Waraka Wa Mazungumzo Baina Ya Israel Na Palestina

Mbowe; Nitawapa CCM shida ambayo hawataisahau


Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa ana usongo na CCM na mwaka huu atawapa shida ambayo hawataisahau.


Mbowe alisema hayo jana wakati akizindua tawi na kukabidhi kadi zaidi ya 200 kwa wanachama wapya wa Chuko Kikuu Kishiriki cha Tumaini Tawi la Makumira , mkoani Arusha.

“Kwa kweli nina usongo na CCM, mwaka huu watapata shida sana kwa kuwa hivi karibuni tutafanya zaidi ya operesheni sangara, tutahakikisha tunapita kila kijiji kilichopo Tanzania bara na Visiwani kuwahamaisha watu juu ya dhana nzima ya ukombozi wa nchi hii” alisema Mbowe na kuongeza.

“Jamani CCM ni walaini kuliko embe bovu, pamoja na kutumia polisi na mabomu yao, risasi za moto, usalama wa taifa na rushwa zao lakini hawa tukipambana nao tunawapiga goli 10 asubuhi asubuhi tu,” alisema.

Alisema CCM wasifikiri Chadema wamebweteka na wabunge 48, madiwani wengi na halmashauri wanazoziongoza,hivi sasa ndiyo kazi ya kuchukua madaraka ya nchi imeshaanza kutokana na kuhakikisha kila pembe ya nchi inafikiwa na ujumbe wa ukombozi.

Akiwahutubia kundi la wanachuo wa chuo hicho tawi la Makumira katika Hoteli ya kitalii ya Ndoro nje kidogo ya Jiji la Ausha, alisema wasomi wa vyuo vikuu wakichukua kadi za Chadema bila ya kupiga vita ufisadi na kutetea haki za Watanzania wanyonge ni kazi bure.

“Sisi Chadema tunasema, unatakiwa uhubiri kitu ambacho unakifanya na unachokifanya ndicho unachotakiwa kukihubiri, ndio maana hata ndani ya Chadema tunapiga vita ufisadi na maovu mengine yote yanayofanywa na serikali ya CCM, hata sisi Chadema tunajisafisha wanaofanya vibaya tunawaondoa, hatuoneani aibu,”alisema Mbowe.

Aliwaasa wanavyuo hao kuwa makini na matendo yao na kuongeza kuwa yoyote hata akichakachua kadi za wananchama wa Chadema hatakuwa nafasi ndani ya chama chake.

“Jiungeni kwa wingi tukomboe nchi, kwa taarifa yenu fursa za uongozi Chadema ziko nyingi kwa wasomi kama nyie na chama hiki kinakua kwa kasi sana hapa nchini baaada ya tukio la Januari 5 baada ya serikali kuona kuwa wanaikomesha Chadema kwa kutupiga mabomu na kutuweka ndani,"alisema.

Alisema kila mkoa hivi sasa wanataka kuandamana na kupigwa risasi kama Arusha ili waingie kwenye kumbukumbu ya ukombozi wa Taifa na wameshaanza kuonekana hata jana vyombo vya habari vimeonyesha ya Dodoma na Songea. Mbowe alisema leo baada ya kutoka katika uzinduzi wa tawi hilo ataenda jimboni kwake Hai na baadaye jijini Dar es salam kwenda kupanga mikakati mizito ya kwa ajili kuimarisha chama.

Akigusia kitendo cha polisi siku ya maandamano ya Januari 5, Mbowe alisema viongozi wa Chadema walikuwa tayari kwa lolote hata kupoteza maisha kwa ajili ya kizazi kinachokuja.

“Ndugu zangu ile siku haikuwa ya mchezo, tulianza maandamano yetu pale Hoteli ya Mt. Meru na tulipofika Tangi la maji polisi walifika na bunduki za kivuta na mabomu ya mchozi wakiwa wameshakoki, tukawaambia tupigeni vifuani tuko tayari kufa kwa ajili ya Taifa” Alisema

Naye Mwenyekiti wa muda wa Tawi la Chadema chuoni hapo Mwalimu, Restituta Kayombo akielezea kuwa mwamko wa kuunda tawi chuoni hapo ilikuwa ni changamoto ya uchaguzi wa mwaka jana wakati matokeo yalipokuwa yakitangazwa na kuonyesha Chadema kuongoza katika sehemu nyingi za nchi.
Chanzo: Mwananchi

Sunday, January 23, 2011

Kula Wadudu Kuokoa Mazingira


Mifugo ikitaabika kutokana na ukame ulosabibisha kukosa lishe
na maji.

Utafiti uliofanyika toka Discover Magazine umegundua ya kuwa kutokana na tatizo la chakula duniani,ukame wa ardhi,maji na uharibifu wa mazingira ili kuokoa mazingira hatua mbadala zinapaswa kuchukuliwa ikiwamo kubadili aina ya maakuli yetu.

Utafiti umegundua ya kuwa ufugaji wa wadudu kama senene,kumbi kumbi,barare na aina za minyoo hauhitaji mradi mkubwa wa ardhi,maji, kwani upatikanaji wake hauhitaji uangalizi mkubwa kama ule wa mifugo ya ng'ombe,mbuzi ,kondoo,nguruwe ambao wanahitaji ardhi na maji ya kutosha hali inayopelekea uhaba wa ardhi na maji hivyo kusababisha ukame na uhaba wa chakula.

Ripoti ya umoja mataifa ya mwaka 2006 inasema kuwa sekta ya ufugaji huchangia 18% ya uchafuzi wa mazingira  duniani kwa kuzalisha kaboni kuliko sekta ya usafirishaji na ndio chanzo kikuu cha kusababisha ukame wa ardhi na maji.Katika utafiti huo wametahadharisha ya kuwa ifikapo mwaka 2050 uzalisha wa wanyama hao utafikia tani 465 maradufu ya takwimu ya mwaka 2000.

Katika toleo hilo umemalizia kwa kuelezea ya kuwa wadudu wanakiasi kidogo cha protini na mlo mzuri kuliko nyama kwani wanyama wana mafuta mengi ambayo ni hatari kwa afya.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...