Mtazamohalisi

Tuesday, November 16, 2010

Rais Amteua Mh.Mizengo Pinda Kuwa Waziri Mkuu

Mbunge wa Jimbo La Katavi-Mh.Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mteule


Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mh.Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu .
Kwa mujibu wa sheria ya nchi, inasubiriwa bunge kuthibitisha uteuzi  wake hii  leo .
Wakati huo huo, leo ndio siku ya kumchagua naibu spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wagombea wa nafasi ya Unaibu spika ni Mh.Job Ndugai kwa tiketi ya CCM na Mh.Mustapha Akonay toka CHADEMA.
Ikiwa bunge litampitisha Mh.Mizengo Pinda ,Waziri Mkuu ataapishwa kesho ikulu ndogo ya Chamwino.
Na mchakato wa kupata baraza la mawaziri utafuata baada ya mashauriano baina ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Baraza la Mawaziri linatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...