Mtazamohalisi

Saturday, November 13, 2010

Kesi ya Ghailani yaendelea kusikilizwa mjini New York

Wakili wa Ghailani azisuta hoja za upande wa mashtaka na kuhoji mteja wake hakuwa akijua chochote kuhusu mashambulio ya kigaidi ya mwaka 1998
Ahmed Khalfan Ghailani akiwa mahakamani

Mawakili wa Mtanzania Ahmed Khalfan Ghailani, anaetuhumiwa kushiriki katika mashambulio dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mnamo mwaka 1998 wanahoji mtuhumiwa huyo hana hatia.
Mnamo siku ya pili ya kusikilizwa hoja za mwisho mwisho katika kesi hiyo, iliyoanza kusikilizwa October 12 mwaka huu,wakili Peter Quijano amehakikisha kwamba mteja wake "hakuwa akijua chochote na kwamba alidanganywa."
Wakili huyo amekosoa pia ushahidi uliotolewa na serikali, akisema "ni dhaifu na wa kutiliwa shaka."
Amekanusha pia hoja kwamba Ghailani alikwenda Pakistan kabla ya mashambulio hayo kutokea.
"Ingekua Ahmed alikuwa ndani ya ndege iliyokuwa ikielekea Pakistan, mngemsikia japo shahidi mmoja. Hakujakuwa na hata mmoja. Ahmed hajakuwemo ndani ya ndege hiyo na nyaraka zilizotolewa ni za bandia." Ameshadidia wakili Peter Quijano.
Mashambulio ya Agosti saba mwaka 1998 dhidi ya ofisi za ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya yaligharimu maisha ya watu 224 na zaidi ya 5000 kujeruhiwa.
Mwenyewe mtuhumiwa, Ahmed Khalfan Ghailani, mwenye umri wa miaka 36 hivi sasa, alikuwepo katika ukumbi wa mahakama akivalia shati rangi ya buluu na tai ya rangi hiyo hiyo.
Anatupiwa lawama ya kuhusika na visa 286 vya uhalifu, ikiwa ni pamoja na "njama ya kutaka kuwauwa Wamarekani."
Wakili wa upande wa mashtaka, Michael Farbiarz, anasema "hoja hizo hazina msingi." Anasema:" Siku ya mashambulio, Ahmed Ghailani aliacha kila kitu alichokuwa nacho maishani mwake, marafiki zake, familia yake, kazi yake na jina lake. Ghailani ni muongo, hakuna maana kwa hivyo kudai amedanganywa."
Wadadisi wanajiuliza kama kisheria ni sawa kesi hiyo kusikilizwa nchini Marekani katika wakati ambapo mashambulio yametokea Afrika mashariki.
Baada ya kusikilizwa hoja za pande zote mbili, na jaji Lewis Kaplan kutoa neno lake, jopo la majaji litaanza kushauriana hii leo.

Mjue Lucas Radebe


Lucas Radebe





 Na Rashid Seif:
katika lugha ya kiswahili unasoma kama lucas Ghadebe,
lucas radebe amekulia katika familia ya watoto 11 katika maisha magumu ya moja ya sehemu zilizokuwa na machafuko makubwa ya kisiasa za ubaguzi wa rangi huko soweto(south western townships).hii ilimpelekea kuja kuwa mmoja katika wachezaji walioheshimika katika ligi kuu ya uingereza na kuwa muafrika kusini wa kwanza kucheza mechi nyingi kuliko wote kwenye timu ya taifa bafana bafana akiwa ameichezea mara 70.
Radebe alinyanyukia kuwa mchezaji muhimu na maarufu mara baada ya kuchaguliwa kuwa nahodha wa timu ya leeds united mwaka 1998.akichukuwa jukumu la kuiongoza timu yenye vijana na wachezaji wengine wenye uzoefu wa ligi kuu.
chini ya uongozi wake radebe leeds united kutoka yorkshire ilinyanyukia kuwa moja ya timu kali katika ligi ya uingereza .Radebe mchango wake haukuwa tu katika uongozi wake bali pia usakataji wake safi wa kandanda usio na utata dhidi ya washambuliaji wa timu pinzani ambao ulimfanya aheshimike duniani na wanasoka wenzake.
HAPO MWANZONI
alikulia katika ukanda wa 4 wa mji wa DIEPKLOOF katika kitongoji cha soweto nje ya jiji la johannesburg.Radebe akishuhudia machafuko ya kisiasa akiwa na umri wa miaka 15 wazazi wake walimpeleka akaishi katika mji wa BOPHUTHASWANA ambao ni mmoja kati ya miji iliyotengwa kwa ajili ya watu weusi katika kipindi cha siasa za ubaguzi wa rangi.alianza kucheza mpira kama sehemu ya kujishughulisha akianza kama mlinda mlango kabla hajabadili kuchezea nafasi ya kiungo na kujiunga na timu ya ICL iliyokuwa ikichezea ligi iliyojulikana kama ligi ya boputhaswana .
mwaka 1989 kipaji chake kilgundulika na timu na moja ya timu kongwe barani afrika ijulikanayo kama kaizer chiefs ambayo alitia mkataba nayo.wakimtaka achezee kama mlinzi wa kati badala ya kiungo....inaendelea

Daw Aung San Suu Kyi (Mother of True Burma), released



The Burmese military authorities have released the pro-democracy leader, Aung San Suu Kyi, from house arrest.
Appearing outside her home in Rangoon, Ms Suu Kyi told thousands of jubilant supporters they had to "work in unison" to achieve their goals.It is not yet clear if any conditions have been placed on her release.

Like the South African leader Nelson Mandela, Aung San Suu Kyi has become an international symbol of heroic and peaceful resistance in the face of oppression. For the Burmese people, Ms Suu Kyi, 64, represents their best and perhaps sole hope that one day there will be an end to the country's military repression. As a pro-democracy campaigner and leader of the opposition National League for Democracy party (NLD),she has spent more than 11 of the past 19 years in some form of detention under Burma's military regime In 1991 she was awarded the Nobel Peace Prize for her efforts to bring democracy to Burma. At the presentation, the Chairman of the Nobel Peace Prize Committee, Francis Sejested, called her "an outstanding example of the power.

For more about  her, listen her documentary of " freedom from fear".
http://www.bbc.co.uk/iplayer/episode/b00sq2n1/Freedom_from_Fear_Aung_San_Suu_Kyi

Haile Gebrselassie Atangaza Kustaafu Mbio

Haile Gebrselassie
                                                                                                                                                              
Usain Bolt akiwa na Haile Gebrselassie
Haile Gebrselassie ,nguli wa mbio ndefu duniani atangaza kustaafu, kwa kushindwa kumalizia mbio na kuishia umbali  wa maili 16 baada ya maumivu ya kuwa na maji kwenye goti la kulia. Alikuwa akishiriki mbio za nyika za jiji la Newyork.

Amesema "hakufikiria kustaafu" "lakini kwa mara ya kwanza leo hii imebidi.Imefika wakati wa kuangalia shuguli nyengine".Aliongezea kwa kusema" Nimeona wana michezo wengi wakipanga muda wa kustaafu. Anasema  haiwi hivyo. Siku ambayo umetangaza kustaafu, basi ndiyo tayari umestaafu kwenye akili yako".

Haile Gebrselassie ameweza kuvunja rekodi za dunia 27, zikiwamo mbio za nyika za mita 5000 na mita 10000. Ameshinda medali ya dhahabu mwaka 1996 katika mbio za mita 10000 huko Atlanta na mwaka 2000 Sydney Olympics.

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 10000 toka 1993- 1999, kwa muda wa miaka minne mfululizo.
Ni mkimbiaji mwenye kasi kwa umbali wowote  kwenye kumbukumbu za mbio, toka dakika 3:31.76 sekunde kwenye umbali wa mita 1500 hadi masaa 2 na dakika 3 na sekunde 59 kwa mbio za nyika. Mwaka 1999 hadi 2000 hajawahi kushindwa katika mbio zozote alizoshiriki kwa muda wa miaka 2 mfululizo.

Hakika, utakumbukwa kwa kuliletea bara la Afrika heshima. Uzoefu unaonesha, itachukua muda kupata mrithi wako. Hata Tanzania , hadi leo hii hawajapata wanariadha walioliletea Taifa heshima kama Filbert Bayi na Juma Ikangaa.

Friday, November 12, 2010

Malikia Elizabeth ajiunga na facebook, na kukutana na kashfa

Malikia Elizabeth wa Uingereza
Hivi karibuni, Queens Elizabeth II alijiunga na facebook na siku moja baada ya kujiunga katika tovuti hii ya jamii ukurasa wake ulijaa maoni machafu kutoka kwa watu . Walengwa wakuu walikuwa Carmilla na Charles na picha zao zilishambuliwa kwa maoni ya matusi.
Ukurasa  huu wa Familia ya Kifalme ya Uingereza, ulizinduliwa Novemba 8 pamoja na akaunti ya Twitter na Flickr. Wakati watu zaidi ya 220,000 "waliipenda", picha 28 katika albamu zilishambuliwa kwa maoni ya aibu na matusi.Familia ya kifalme ina wafuasi zaidi ya 75,500 kwenye Twitter na huweka picha mpya katika akaunti yake  ya Flickr kila siku. Pia ina channel kwenye Youtube

Saudi Arabia yaimarisha ulinzi Mecca

Mecca-Saudi Arabia

Kiasi ya mahujaji wa Kiislamu millioni mbili na nusu wanaanza kumiminika katika mji wa mtakatifu wa Makkah, huko Saudi Arabia, huku ulinzi ukiimarishwa kwenye mji huo ambao umewekwa vifaa vipya vya kisasa, ukiwemo usafiri wa treni kurahisisha zoezi hilo la Hijja.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia, mwanamfalme Nayef bin Abdul Aziz, amesema hawawezi kulipuuza tishio la kundi la kigaidi la Al-Qaida kushambulia wakati wa Hijja hiyo ya siku tano inayoanza kesho kutwa, Jumapili, ijapokuwa kundi hilo halijawahi kufanya shambulio lolote dhidi ya hijja hapo kabla.
Hapo siku ya Jumatano, waziri huyo wa ndani wa Saudi Arabia alielezea kitisho cha  kundi la Al-Qaida kushambulia, lakini hata hivyo akasema uwezekano ni mdogo wa kufanya hivyo.

Dar-es- Salaam, Tanzania
MAHUJAJI 20 waliokuwa wasafiri kwa ndege ya Shirika la Eggypt na Ethiopia kwenda Hijja Meccah na Madina wamekwama uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wa Dar es Salaam baada ya kutapeliwa fedha zao. Abiria hao ambao walieleza kuwa walipanga safari hiyo kupitia taasisi ya Taibah ya jijini Dar es Salaam, wamekwama kuondoka baada ya taasisi hiyo kuwakana.
Baadhi ya abiria hao waliozungumza na Mwananchi katika ofisi za Taibah jana walisema walilalamikia kitendo hicho na kukiita cha kikatili kwa kuwa hata fedha zao hawajalipwa. Salma Abedi alisema alilipa Sh5.5 milioni kwa ajili ya safari hiyo kwenda na kurudi, chakula na malazi kwa juma moja.

“Kwa kifupi la kusema sina kwani nikikumbuka jinsi nilivyohangaika kuipata hii safari sitaki kuamini eti leo naambiwa hakuna safari wakati Paspoti ninayo na nilikuwa katika listi ya watu wanaoondoka,”alisema Abedi. “Leo hadi muda huu hawajafungua ofisi inavyoonekana haitofunguliwa hebu niambie huu si utapeli huu.

“Nimetoa dola elfu tatu na mia moja kugharamikia safari hii,nimetokea Kongo na nimelipia katika shirika hili nikitegemea kuondoka na ndege iliyoondoka tangu juzi, lakini cha ajabu nimeambiwa safari hakuna na viongozi siwaoni,”alisema Abdalah Abeidi ambaye ni raia wa Kongo.

“Hapa unaponiona nimekuja tangu Oktoba 25, mwaka huu, nimefikia hotelini ambako mpaka leo hii muda wangu wa kukaa pale umekwisha na sina tena fedha za kulipia na mimi hapa ni mgeni sina ndugu nitaenda wapi?sina la zaidi ninachotaka nipewe fedha zangu tu,”alisema Abeidi. Mwenyekiti wa NGO Mkoa wa Tanga Saida Sharifu ambaye nae ni mmoja wa mahujaji alisema amesikitishwa na kitendo cha Taasisi hiyo kwa kudhulumu haki yake.

“Mimi nilitoka Tanga kwa madhumuni ya kwenda katika Hijja na nililipia fedha katika taasisi hii ya Taibah,kitendo cha wao kukimbia ni kitendo kibaya na kinachoumiza kwani kuna watu walifika hadi uwanja wa ndege ila wakarudishwa wengine hawana fedha, kifupi tumedhalilishwa sana,”alisema Sharifu. Aliiomba serikali kufuatilia taasisi hiyo na kuichukulia hatua kwani ni aibu kubwa kwa taasisi ya dini kufanya jambo kama hilo.


Safari hiyo ya kwenda kuhiji Makka na Madina ilikuwa inagharimu Sh 55 milioni ambayo inajumuisha malazi,chakula na usafiri wa kwenda na kurudi. Mbali na hayo, taasisi hiyo ilitoa hati feki ya kusafiria kwa watu na kusababisha mtu mmoja kuwekwa rumande katika uwanja wa ndege wa kimataifa kwa kukutwa na hati hiyo.

Mweka hazina wa taasisi ya Taibah iliyoandaa safari hiyo, Ali Momba alisema taasisi hiyo haiwatambui mahujaji hao kwa kuwa walilipa fedha zao nje ya ofisi. "Hawa walilipa fedha nje ya ofisi zetu na sisi hatuna majina yao," alisema Momba.
  
Ningependa kuwapa pole kwa usumbufu mahujaji waliopatwa na kadhia hii, na kutoa wito kwa serikali kuchukua hatua muafaka za kudhibiti makampuni ya uwakala wa hijja ili aibu kama hii isijirudie.
Hii si mara ya kwanza kwa mahujaji kujikuta katika usumbufu kama huu ,mwaka 2007 ili wachukua zaidi ya wiki na kuilazimu serikali kuingilia kati .

Spika wa Zamani Mh.Samuel Sitta akila kiapo cha Ubunge

Spika Mstaafu Samuel Sitta


Mheshimiwa Samuel Sitta ,Mbunge wa Urambo Mashariki akila kiapo cha Mbunge mbele ya Naibu wake wa zamani na mrithi wake wa kiti cha Uspika Bi.Anna Makinda.

Hongera kwa kuonesha ukomavu, Mheshimiwa Sitta sauti yako dhidi ya ufisadi kwa Taifa letu tungali tukiihitaji.Kwa kuwa mchezo wa siasa  ni kitendawili ikiwa utateuliwa kuwa waziri bado tunakuomba uendelee kuwa mpiganaji hadi pumzi yako ya mwisho.

Anna Makinda Kama Nancy Pelosi

Spika Mpya wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Bi.Anna Makinda

Ameshinda Uspika kwa kura 265 dhidi ya 53 za Mabere Marando.
Kwa ushindi huo, anafungua ukurasa mpya katika siasa za Tanzania kwa kuwa Mwanamke wa kwanza
kukalia kiti hicho cha uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Marekani ni miongoni mwa wanawake wa chache waliyo bahatika kushika nyadhifa nyeti kama ya Uspika.

Mheshimiwa Anna Makinda ,mbunge toka Njombe kusini kama Spika wa kwanza
Mstaafu Chifu Adam Sapi Mkwawa anaweka  historia kwa mkoa wa Iringa kwa  mara ya pili kuweza kutoa Spika.

Tunakutakia mafanikio mema katika majukumu yako ya kulifikisha Taifa mbele kwa salama na amani,
kwa uzoefu wako pamoja na hekima na maarifa tunatarajia utakabiliana vyema na changamoto za muhimili huu muhimu wa dola.Mungu atakusaidia, hongera.

Thursday, November 11, 2010

Freeman Mbowe atangazwa kiongozi wa upinzani bungeni



Mh.Freeman Mbowe ndio kiongozi wa upinzani bungeni
Naibu wake ni Mh.Zitto Kabwe
na Mh. Tundu Lissu anakuwa ni mnadhimu mkuu.

Awali nafasi hiyo ya kiongozi wa upinzani bungeni ilikuwa ikishikiliwa na Mh.Hamad Rashid wa CUF na
naibu wake alikuwa Mh. Willbrod Slaa wa Chadema katika bunge lililopita .

Viti maalumu,CCM YAVUNA 65, CHADEMA 23, CUF 10

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeidhinisha majina 88 ya wabunge wateule wa viti maalumu wa vyama vya CCM na Chadema  na kutenga viti kumi kwa Chama cha wananchi (CUF) ambacho hakuwasilisha mapendekezo ya wanaowania nafasi hizo.Katika hatua hiyo Nec imeacha nafasi nyingine sita wazi kusubiri chaguzi za ubunge katika majimbo saba ambayo upigaji kura uliahirishwa. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana Jijini Dar es Salaam jana  chama cha CUF bado hakijawasilisha orodha ya majina ya wanawake watakaowania viti maalumu, lakini orodha hiyo ya Nec inaonyesha kuwa baadhi ya wabunge waliokuwemo wako hatarini kuachwa huku waliko katika nafasi za kwanza katika vyama vyote wakiwa na matumiani ya kupeta.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,  Jaji Lewis Makame aliliambia Mwananchi jana kwamba baada ya kukokotoa uwiano wa viti hivyo maalumu, CCM iliongoza kwa kupata viti 65, ikifuatiwa na Chadema viti 23 wakati CUF kimeambulia viti 10 pekee. Jumla ya viti vyote ni 104.
Katika bunge lililopita ambalo lilikuwa na viti 75 maalumu CCM ilikuwa na viti 58, CUF viti 11 na Chadema viti sita na safari hii vimeongezwa hadi kufikia 104 na mgowanyo wake ukiwa kama ulivyoonyeshwa kwa kuingazia uwiano wa wingi wa kura za ubunge.
Akizungumzia namna Nec ilivyokokotoa mgawanyo wa viti hivyo na kupata uwiano kwa kila chama, Jaji Makame alisema kisheria walivigawanya kutokana na wastani wa kura za wabunge. Kura hizo ni zile ambazo kila chama kilizipata kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote Oktoba 31.
Kwa mujibu wa Makame, tayari Nec imeishawaandikia CUF barua mbili kwa nyakati tofauti kuitaka ipeleke orodha hiyo bila mafanikio.
 “Tumeshawaandikia barua mbili kuwakumbusha juu ya hatua hiyo ya kwanza Agosti na ya pili Novemba mwaka huu lakini hawakutujibu,” alibainisha Jaji Makame akisema viti hivyo vitabakia wazi hadi CUF itakapowasilisha orodha hiyo.
Kuhusu viti sita vilivyoachwa wazi, Makame alisema vinasubiri matokeo ya majimbo saba ambayo uchaguzi wake haujafanyika.
Majimbo ambayo uchaguzi wake uliahirishwa ni Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini na Nkenge, yote ya Tanzania Bara na mengine manne ya Tanzania visiwani ambayo ni Mwanakwerekwe, Mtoni, Magogoni na Wete.
Alisema vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo, havikupata wabunge hao wa viti maalum kutokana na kushindwa kufikisha asilimia tano ya kura za urais.
“Sheria inasema, ili chama kipate wabunge wa viti maalum, kinatakiwa angalau kipate asilimia tano ya kura za urais hali ambayo vyama vingine havikutimiza,” alisema Makame.
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zilieleza kwamba Nec itatangaza majina ya wabunge wateule wa viti maalumu kwa vyama vya CCM na Chadema leo.
Hata hivyo, Mwananchi lilifanikiwa kupata orodha za majina zinazodaiwa kuwasilishwa Nec na vyama hivyo.
Orodha hizo zinadawa kupangwa kulingana na uzito wa nafasi ya kuteuliwa.
Kutokana na Nec kuitengea CCM nafasi 65, majina ya wanawake ambao wana nafasi kubwa kuwa kwenye orodha ya uteuzi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba, Gaudentia  Kabaka, Ummi Mwalimu, Agness Hokororo, Martha Umbulla, Lucy Mayenga, Faida Mohamed Bakari, Felista Bura, Kidawa Hamid Saleh na Stella Manyanya.
Wengine ni Maria Hewa, Hilda Ngoye, Josephine Genzabuke, Esther Midimu, Maida Hamad Abdalla, Asha Mshimba Jecha, Zarina Madabida, Namalok Sokoine, Munde Abdallah na Benardetha Mushashu.

Pia wamo Vick Kamata, Pindi Chana, Fatuma Mikidadi, Getrude Rwakatare, Betty Machangu, Diana Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Vulu, Abia Nyabakari na Pudenciana Kikwembe.
Lediana Mng’ong’o, Sarah Msafiri Ally, Catherine Magige, Tauhida Galos Cassian, Asha Mohamed Omari, Rita Mlaki, Anna Abdallah, Fenella Mukangara, Terezya Huvisa na Al-Shaymaa Kwegir.
Margreth Mkanga, Angellah Kairuki, Zainab Kawawa, Mwanakhamis Said, Riziki Lulida,  Devotha Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Mfaki, Margreth Sitta na  Subira Mgalu.
Rita Kabati, Martha Mlata, Dk Maua Daftari, Elizabeth Batenga, Azza Hamad, Mary Mwanjelwa, Josephine Chengula, Bahati Abeid, Kiumbwa Mbaraka na Roweete Kasikila.

Anastazia Wambura, Mary Chatanda, Rosemary Kirigini,
Mariam Kisangi na Kemilembe  Lwota.
Walioko katika hati hati ya kutokuwapo kwenye orodha hiyo ni Tinner Chenge, Mwandishi wa habari, Kaslida Mgeni, Mboni Mhita na Janet Masaburi.
Kwa upande wa Chadema, 23 wenye nafasi kubwa ya kuwepo ni Lucy Owenya, Ester Matiko, Mhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekuli na Conchesta Rwamlaza.
Wengine ni Suzan Kiwanga, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu, Regia Mtema, Christowaja Mkinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Chiku Abwao.
Pia wamo Naomi Kaihula, Grace Kiwelu, Rose Kamili, Christina Lissu Mughiwa, Raya Ibrahim, Philipa Mturano, Miriam Msabaha, Rachel Mashishanga.
Source: Mwananchi

Spika Mpya ni Anna Makinda au Mh Mabere Marando



Baada ya kushinda kwa kishindo na kuwa acha mbali wagombea wenzake katika kinyang'anyiro cha kiti cha Uspika, kama kura zinavyojionesha:-
Makinda kura 211

Anna Abdalah 14

Kate kamba 15
Mh. Bi Anna Makinda  wa CCM atapambana na Mh. Mabere Marando wa Chadema.

Wednesday, November 10, 2010

Si Mh.Sitta si Mh. Chenge

Kamati Kuu ya CCM imependekezea majina yafuatayo kugombea Uspika:

1. Anna Makinda
2. Anna Abdallah
3. Kate Kamba

Kwa hivyo Mzee wa Vijisenti out, Sitta out!!!

Source: Channel 10 News Bulletin 3 minutes ago

Kimuelekeo inaonesha CCM inataka kujijenga upya, kutokana na nyufa zilizosababisha kupoteza viti vingi bungeni. Na hii imetokana na kuwa na kambi kuu mbili za Spika Mstaafu Mh.Samuel Sitta na ile kambi ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa nawashirika wake Mh. Andrew Chenge.

Spika ajaye kama picha inavyo jionesha, atakuwa ni Mwanamke kwa maana Tanzania itafungua ukurasa mpya wa kuwa na kiongozi wa  kwanza Mwanamke kuongoza muhimili muhimu wa dola.

Kwa moyo mkunjufu, tunakaribisha changamoto hii mpya kama ishara ya kuiambia dunia ya kuwa Tanzania tumekomaa kidemokrasia na tupo tayari kuondokana na mtazamo wa kihafidhina unaopendelea mfumo dume.

Dodoma Nani ni Nani?

Vinara wa wanagombea nafasi ya Uspika  Mh.Samuel Sitta na Mh.Andrew Chenge.

Viongozi wa Kitaifa wawasili Dodoma

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza na kumpa mapokezi ya furaha katika uwanja wa ndege wa Dodoma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimu  wananchi wa mkoa wa Dodoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma leo Nov 10, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufanya mkoani hapa tangu apate wadhifa huo. Kiongozi huyo atakuwa mkoani hapa kuhudhuria mikutano ya CCM katika ngazi za Kamati Kuu na Halmshauri Kuu na kisha sherehe za kuapishwa wabunge sambamba na uteuzi wa Waziri Mkuu. Picha na Muhidin Sufiani


Tuesday, November 9, 2010

Maisha ya Kila Siku Vijijini

Mama na mzigo wa kuni









Dunia ya masikini,yaponzwa na yake njaa
nitumie kuni gani?, nisije pata fadhaa.
sishi kuzichanja kuni, na bado nazisha saa
majasho tele usoni, kama ni ndoo hujaa.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa".

Kuni za kilimanjaro, nilianza kutumia
kwa njia za uchochoro, kuni zilinifikia
na sasa nina kihoro,theluji ya angamia
limekuwa ni gogoro, na maji yanapotea.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa"

Nikageukia mkoko, maarufu kule pwani
kwa kuivunja miiko, kumegeuka wangwani
mawimbi sasa kiboko, miji ipo tafrani
ya vunja huko nahuko, na nyumba zipo majini.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa"

Kwa kuitaka nafuu, naagiza visiwani
kuni za mkarafuu, zilo katwa mashambani
majuto ni mjukuu, nimetiwa mikononi
sheria ndiyo mkuu, najikuta hatiani.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa"

Nikafanya marejeo, fikira kuzi tembeza 
Amani ni mulekeo, kijiji pale lunguza
misitu waliyo nayo ,kuni tulimaliza
Ajira ya vipepeo, vijana wamepoteza.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa"

Ikiwa mafuta ya taa, kwa jiko lake la tambi
nalo lataka wasaa,kulimudu ni kivumbi
nahisi bora mkaa, bei yake haigombi
japo kidogo lafaa, kwa sisi watu wa kambi.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa"

Nishati nzuri umeme, hilo tunali tambua
yapasa mtu uzame, huduma kujipatia
huenda mimi niseme, kheri umeme wa jua
lakini pesa ukame, kuni nime zichagua.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa"

Mwisho jamani nahisi, jibu muta nipatia
msije nambia gesi, ni endane na dunia
kipato changu halisi, siwezi kufikiria
ikiwa hamto pasi, kuni nitaji katia.
"nishati ipi jamani?, mimi kwangu inafaa"
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...