Mtazamohalisi

Thursday, January 6, 2011

Mchezo wa Argentina - Benki Zetu Ziwe Macho

Licha ya kuwa na kamera na viashiria sauti hilo halikuweza kuwazuia majambazi kutojichotea zaidi ya Dola milioni 6 katika tawi la Belgrano la benki ya Provincia Bank ,Argentina.

Majambazi hao walikodisha jengo ambalo limeambatana pamoja na benki hiyo,na ndipo walipotumia nyenzo mbali mbali za ujenzi na kufanikiwa kupasua ndani kwa ndani hadi kufikia chumba cha kuhifadhi fedha.
Ili chukua muda wa miezi 6 kwa majambazi hao kufanikisha zoezi hilo lilitokelezeka siku ya mkesha wa mwaka mpya.
Habari zadi............Argentina

Misri yaitega CECAFA

BARAZA la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), sasa linapita katika kipindi kigumu baada ya Misri kusema itajisikia raha kama litaanzishwa Shirikisho la Soka kwa Nchi za Bonde la Mto Nile.

Kauli hiyo ya Misri ni nyepesi, lakini yenye uzito mkubwa kwani inaweza kupunguza msisimko wa mashindano ya CECAFA na hata kuyaua kabisa na badala yake yale ya nchi za Bonde la Mto Nile kuwa yapo juu, hasa katika suala la zawadi.

Juzi Chama cha Soka cha Misri (EFA) kilitangaza zawadi ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa bingwa wa michuano ya soka kwa nchi za Bonde la Mto Nile iliyoanza jana mjini hapa ikishirikisha nchi saba.
Zawadi hiyo ni zaidi ya mara tano ya ile ambayo Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' ilichukua baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya Chalenji mwezi uliopita katika mashindano yaliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo Stars ilitwaa dola za Marekani 30,000 ambazo ni karibu Sh milioni 43 za Tanzania.

Kutokana na mwitikio mzuri wa nchi zinazoshiriki michuano ya Mto Nile mwaka huu, Misri imesema ipo katika mazungumzo na nchi ambazo bonde hilo lipo, ili kuzishawishi lianzishwe shirikisho hilo ambalo Misri inaamini litakuwa kitovu cha vipaji vya soka Afrika na duniani kwa ujumla.

Rais wa EFA, Samir Zahir alisema juzi kuwa kama nchi zote zitakubaliana kuanzisha shirikisho hilo itakuwa hatua moja kubwa ambayo imepigwa kwa maendeleo ya soka Afrika
Lakini EFA inaona ugumu ulio mbele juu ya kuanzishwa kwa shirikisho hilo kwa vile baadhi ya nchi tayari zipo katika vyama mbalimbali vinavyosimamia soka kwa kanda zao.

Alisema zaidi ya nusu ya nchi zinazoshiriki mashindano hayo ya Bonde la Mto Nile ni wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ukiacha Misri na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo ni mwalikwa katika michuano hiyo.

Nchi zinazoshiriki michuano hiyo ambazo ni wanachama wa CECAFA ni Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan na Burundi na zimekuwa zikishiriki mashindano yanayoandaliwa na baraza hilo karibu kila mwaka.

"Tumepeana changamoto ya namna bora ya kuanzisha shirikisho letu, uwezo wa kufanya hivyo tunao maana dhamira yetu ni kuendeleza soka," alisema.

Nchi nyingine wanachama wa CECAFA ambazo hazijashiriki michuano ya Mto Nile ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Rwanda na Somalia.

Misri imegharamia usafiri wa kuja Misri na kurudi nyumbani kwa kila timu pamoja na posho za wachezaji na waamuzi, zawadi mbalimbali kwa washindi.

Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa zaidi ya Sh milioni 200 za Tanzania. Pia Rais huyo wa EFA, alieleza kuwa michuano yao ni maalumu kuhamasisha soka na haihusiani na masuala ya kisiasa na kwamba mambo yanayohusiana na siasa ni jukumu la wahusika wenyewe.

"Kwangu mimi ukiniuliza michuano ya soka kwa nchi za Bonde la Mto Nile ina madhumuni gani, nitakwambia ni kuinua soka. Hilo ndilo jibu langu na ndicho ninachokiamini," alisema.

Alieleza kuwa mwaka huu mashindano hayo yamefanyika Misri, hivyo nafasi ipo wazi kwa nchi nyingine ambayo itakuwa tayari kuyaandaa na kwamba Misri itatoa msaada wa karibu zaidi ili kuyafanikisha.
Chanzo: HabariLeo

Wakati huohuo,ufunguzi wa michuano ya soka kwa nchi za bonde la mto mto Nile yaliyofunguliwa jana,kati ya wenyeji Misri na Tanzania yalikuwa kama hivi.

Monday, January 3, 2011

Tunaelekea Kula Kwa Kushiba Moshi

Muelekeo wa dunia kwa sasa kila mamlaka inalia hali,ukweli hakuna nafuu ila tutarajie kuumizana ili kufikia malengo ya kiutawala na uchumi.

Mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka wa serikali za nchi za ulaya kufunga mkanda kwa kubana matumizi ili kukabiliana na anguko la uchumi, msukumo uliopelekea kufanya hivyo ni kuweza kutunisha mfuko wa kulipa madeni yanayo yakabili mataifa hayo.

Sijui kama tushapata picha kuwa mwaka huu mpya 2011 mlango unaelekea kufungwa na nchi zetu changa haja zetu hatuziwezi tunategemea muhisani mwenye funguo.

Kwa taarifa , wahisani wanahaha kuweka serikali zao sawa maana wanajua wananchi waliowaweka wasipotimiziwa haja zao basi kura itakuwa fimbo.

Kesho wakaazi wa Uingereza  wataanza kukamuliwa kwa kulipa kodi ya ongezeko la thamani(VAT) toka 17% hadi 20% ,athari ya ongezeko la kodi ni kupungua mauzo ya bidhaa sokoni nakutokana na hilo Makampuni yatabidi kupunguza wafanyakazi na kuathiri soko la ajira.

 India inakabiliwa na ongezeko la bei ya vyakula,nchi ambayo soko kubwa la mazao yake lipo Mashariki ya kati . Kwa hali hiyo bei za vyakula kwa nchi za Mashariki ya kati zinatarajiwa kupanda na kupelekea wakaazi wake ambao wengi wao ni wageni toka nchi za nje kuzama zaidi mfukoni .

Hatua muhimu ambazo serikali inatakiwa kuzichukua kabla "hatujaelekea kula kwa kushiba moshi" ni kubana matumizi yake hasa posho za vikao na misafara ya wakubwa.Mfano mzuri ni matukio ya hivi karibuni kwa Waziri Mkuu(Mtoto wa mkulima)  kukataa gari la kifahari na kitendo cha waziri wa fedha Mustafa Mkullo kufanya ubadhirifu kwa kukodi ndege na kuagiza kupelekewa gari lake Dodoma .

Kilimo kwanza lazima kutiliwa mkazo wa hali ya juu kwani ongezeko la bei ya chakula linahatarisha amani ya wananchi.Mara nyingi tunapoona ndiyo tunapopata fundisho, siku za hivi karibuni nchi ya  Tunisia imejikuta ikikabiliwa na maandamano kutokana na halingumu ya maisha iliyotokana na ongezeko la watu  kukosa ajira.
Nathubutu kusema hivyo kutokana na kuwa "njaa ikiingia mlangoni ,amani hutokea dirishani" uvumilivu una kiasi chake nacho nikupatiwa ufumbuzi ili nafuu ya maisha ipatikane.

Serikali inatakiwa kujipanga vizuri ilikujikwamua kiuchumi bila kutarajia huruma za wahisani kufanikisha bajeti zetu, ni kwa kutumia vyema raslimali zetu kama bandari,viwanja vya ndege, vivutio vya utalii ,ardhi yenye rutuba,madini na gesi.

Hayo yote yakiwezekana Tanzania haitakuwa tena ikitembeza kikapu kwa wahisani zetu, kwani dunia ya sasa "Tunaelekea kula kwa kushiba Moshi" .Sunday, January 2, 2011

Matokeo Ya Ligi kuu Ya Uingereza Wikiendi Hii

Sat 01/01/11 West Bromwich 1 - 2 Manchester United
Liverpool 2 - 1 Bolton Wanderers
Manchester City 1 - 0 Blackpool
Stoke City 2 - 0 Everton 
Sunderland 3 - 0 Blackburn Rovers 
Tottenham Hotspur 1 - 0 Fulham
West Ham United 2 - 0 Wolverhampton
Birmingham City 0 - 3 Arsenal

Sun 02/01/11 Chelsea 3 - 3 Aston Villa

Msimamo wa kila timu baada ya mechi 5 za mwisho
1 Manchester United 19 11 8 0 41 18 +23 41 W D W W W
2 Manchester City 21 12 5 4 33 16 +17 41 W W W L W
3 Arsenal 20 12 3 5 42 22 +20 39 W D W L W
4 Tottenham Hotspur 20 10 6 4 30 23 +7 36 W W W D D
5 Chelsea 20 10 5 5 36 18 +18 35 D W L D D
6 Sunderland 21 7 9 5 24 22 +2 30 W L L W D
7 Bolton Wanderers 21 7 8 6 33 28 +5 29 L L W L W
8 Stoke City 20 8 3 9 25 24 +1 27 W L W L D
9 Liverpool 19 7 4 8 23 24 -1 25 W L L W L
10 Newcastle United 20 7 4 9 29 31 -2 25 W L L W L
11 Blackpool 18 7 4 7 26 30 -4 25 L W W D W
12 Blackburn Rovers 21 7 4 10 26 34 -8 25 L W L D L
13 Everton 20 4 10 6 21 24 -3 22 L D W D D
14 West Bromwich … 20 6 4 10 26 36 -10 22 L L L L W
15 Aston Villa 20 5 6 9 23 37 -14 21 D L L W L
16 West Ham United 21 4 8 9 22 33 -11 20 W D W D L
17 Wigan Athletic 20 4 8 8 17 32 -15 20 L D W D D
18 Fulham 20 3 10 7 19 24 -5 19 L W L D L
19 Birmingham City 19 3 10 6 18 24 -6 19 L D L D D
20 Wolverhampton … 20 5 3 12 20 34 -14 18 L W L W L

Ubalozi Wagoma Kutoa Viza Kwa Tajiri Wa Chelsea-Roman Abramovich

Tajiri wa klabu ya Chelsea ,Roman Abramovich jitihada zake
 za kuwaombea viza vijana wa Kitanzania zimegonga ukuta.
Roman Abramovich, the owner of Chelsea football club, attempted to reward African porters who helped him on his failed attempt to climb Mount Kilimajaro by flying them to London to watch a Chelsea game only to be thwarted by red tape.
Roman Abramovich,kushoto akiwa na Mpenzi wake
Daria Zukhova,walifanya ziara ya kupanda mlima Kilimanjaro
mwaka jana.
Mwezi septemba mwaka jana,Abramovich na ujumbe wake wa watu 6 ulifanya ziara ya Tanzania kwa ajilii ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa 19,330ft ndio mlima mrefu kuliko yote Afrika, kwenye kuupanda mlima huo Abramovich alifikia urefu wa  15,100ft nakushindwa kupumua kutokana hali ya hewa kuwa nzito hivyo kupatiwa msaada na Wapagazi nakumuwezesha kufika chini salama.

Kufuatia kitendo cha kiutu cha wapagazi hao,Abramovich aliwaahidi kuwalipa hisani kwa kuwapa mualiko kwenda London kuangalia timu ya Chelsea itakapokuwa uwanjani kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Lakini jitihada zake hazikufanikiwa kufuatia Ubalozi wa Uingereza kuwakatalia vijana hao Viza mara mbili kwa shaka ya kutoroka pindi watakapo kuwa nchini Uingereza.

Licha ya timu ya Chelsea kutoa mualiko na kutayarisha mazingira ya ujio wao kwa kuandaa usafiri wa kwenda na kurudi,malazi na vyakula,juhudi zote hazikuweza kubadilisha msimamo wa Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania kubadili msimamo wake.
Chanzo: Telegraph

Wakati huo huo Chelsea imepokwa ushindi Dakika ya lala salama
Na matokeo ya kawa Chelsea 3 Vs Aston Villa 3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...