Mtazamohalisi

Saturday, November 20, 2010

Ligi Kuu Ya Uingereza, Heshima

Kocha wa Arsenal
Arsene Wenger
                                                                       
Ni wikiendi chungu kwa vigogo wa ligi ya Uingereza pale Chelsea ilipofungwa bao moja bila majibu dhidi ya Birmingham, washika bunduki wa London  Arsenal wameshangazwa  kwa kufungwa bao tatu kwa mbili dhidi ya wapinzani wao jadi Totenham Hotspur na kujikuta wakishuka nafasi ya tatu .Msimu huu Uwanja wa Emirates unaonekana kama Arsenal si uwanja wake wa nyumbani, mashetani wekundu Manchester United wamekamata nafasi ya pili baada ya kuifunga Wigan bao mbili bila majibu.

Kwa matokeo hayo Chelsea inaendelea kushikilia usukani wa ligi kuu ya Uingereza kwa pointi 28 sawa na Manchester United  inayokamata nafasi ya pili kwa pointi 28,Chelsea ina magoli 6 zaidi ya Manchester United.Arsenal ni ya tatu kwa pointi 26 nyuma kwa pointi mbili dhidi ya kinara wa ligi Chelsea.

Wakati huohuo,Bwawa la maini Liverpool imefanya kweli baada ya kuanza vibaya msimu huu kwa kuifunga West ham bao tatu bila majibu na kwa matokeo hayo Westham inashika mkia,ikifuatiwa na Wolves zote zina pointi 9 na Wigan yenye pointi 14.

Matokeo ya mechi za leo katika ligi kuu ya Uingereza yalikuwa kama hivi; Arsenal 2-Totenham 3, Birmingham 1-Chelsea 0, Blackpool 2- Wolves 1, Bolton 5-Newcastle 1, Liverpool 3- Westham 0, Man United 2- Wigan 0, West Brom 0- Stoke 3.
Kesho Jumapili kuna pambano kati ya Blackburn -Aston Villa & Fulham - Man City.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...