Mtazamohalisi

Friday, December 3, 2010

Rais Jakaya Kikwete Akabidhi Uenyekiti Wa Afrika Mashariki Kwa Rais Nkurunzinza Wa Burundi


Mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki anayemaliza muda wake,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakati wa mkutano wa kumi na mbili wa kilele wa wakuu wa nchi ya jumuiya hiyo uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana jioni.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki aliyemaliza muda wake,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo,Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi mara baada ya kumkabidhi uenyekiti huo(Picha:Freddy Maro)

Kweli Madaraka Matamu-Bagbo Ahujumu Ushindi Wa Upinzani Ivory Coast

Matokeo ya Rais wa Ivory Coast yapo kwenye hatihati baada ya tamko la baraza la katiba la nchi hiyo kutaka kutangaza matokeo yao,punde tu tume ya uchaguzi ilipomtangaza kiongozi wa upinzani kuwa mshindi.

Wafuasi wa Rais aliyeshindwa Laurent Bagbo wameita tangazo la siku ya alhamisi kuwa ni "mapinduzi yaliyoshndwa".Mipaka yote ya nchi jirani za Afrika Magharibi imefungwa siku ya ijumaa,television na radio za kigeni pamoja na ujumbe mfupi wa simu kufungiwe kwa muda usiojulikana huku nchi ikiwa katika hali ya tahadhari.Uwezekano wa  wananchi kupata taarifa ni kwa njia ya satelite tv.

Upigaji kura kwa nchi hii ni kurudisha hali ya amani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002-2003 ambavyo vililigawa taifa hili maarufu kwa zao la kokoa pande mbili, lakini hali tete siku ya ijumaa imekuwa kama makali ya kisu.Marekani imezitaka pande zote zinazohusika kukubaliana na matokeo yaliyompa kiongozi wa upinzani Alasane Ouattara ushindi.

Rais Obama ametilia uzito matokeo hayo na kumpa pongezi Alasane Outtara kwa ushindi,na kumtaka rais aliyeshindwa Laurent Bagbo kukubaliana na matokeo ambayo yamethibitisha na umoja wa mataifa.

Taarifa ya matokeo zimeleta utata mkubwa,na kutangazwa kwa rais wa sasa Laurent Bagbo kuwa mshindi na baraza la katiba la nchi hiyo kumewaacha wananchi kutoelewa nini kinaendelea kwa kuwa matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi inayokubalika na Umoja wa Afrika ,Umoja wa Mataifa na Marekani yalionesha kuwa  Alasane Ouattara 54.1% na Laurent Bagbo 45.9%  .

Matokeo mapya yaliyotangazwa na baraza la katiba limempa ushindi  rais wa sasa Laurent Bagbo kwa 51% ,huku akiibukia kupata kura 500000 kwenye ngome ya Ouattara ambayo ni 10% ya wapiga kura na kubatilisha matokeo ya  majimbo 7 kati ya 19 kwa madai ya wafuasi wa Bagbo walipokea vitisho toka kwa wahuni.

Mara ya matokeo hayo Umoja wa mataifa umeyakataa matokeo hayo ya baraza la katiba nakuyaita ni batili huku ikibaki na msimamo wa kuyatambua matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yaliyompa ushindi Alasane Ouattara.
Chanzo: Associated Press

Obama: Qatar Haikustahiki Kuandaa Kombe La Dunia 2022

Rais wa Marekani amesema Fifa wamefanya kosa kuipa Qatar kuandaa kombe la dunia 2022 badala ya nchi yake."Nafikiri ni uamuzi wa makosa"Obama aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani.Amesema alitarajia  ujumbe wa Marekani ungefanikiwa mwishoni.

Fifa wameiteua Qatar dhidi ya Marekani,Japan,Korea na Australia kuandaa kombe la dunia 2022.Na Urusi kufanikiwa kuandaa kombe la dunia 2018.

Shirikisho la soka la Marekani limetumia mamilioni ya dola kupeleka ujumbe wake ili kuishawishi Fifa kuichagua ukiwamo ujumbe mzito unaongozwa na rais wa zamani wa Marekani Bill Cliton ambaye alijumuika kwa juhudi zote hadi siku ya mwisho ya kuwakilisha mapendekezo.

Ujumbe mkuu wa watetezi wa uandaaji wa Marekani ni tumaini la kuandaa tena kombe la dunia badala ya lile la 1994 ili kuinua kiwango cha soka huko Marekani.

Wakati huo huo Qatar imepongeza uamuzi huo wa siku ya alhamisi na kuuita ni ushindi dhidi ya dhana potofu kwa nchi yao kuwa haina sifa ya uandaaji wa kombe la dunia 2022.Mwanzoni Qatar iliwekwa nje ya matarajio kwa kuwa wengi waliiona ni nchi ndogo ambayo haina sifa ya uandaaji wa mashindano makubwa kama hayo.

Na sasa litakuwa taifa la kwanza dogo kuandaa mashindano hayo, baada ya kuweza kuishawishi Fifa juu ya mpango wake wa ujenzi wa viwanja vya kutumia viyoyozi ili kuzuia joto la kipindi cha kiangazi.

Sheikh Mohamed Bin Hamad Al Thani ,kiongozi mkuu wa ujumbe wa Qatar  aliishukuru Fifa kwa kuwa na "mtazamo makini" alisema "Itakumbukwa kulikuwa na mshindano yenye tabia nchi kama Qatar, lakini kwa sababu ya dhana potofu ilikuwa ni vigumu kwao kupambana na hilo kuweza kudhihirisha kuwapo katika kiwango cha dunia"."Moja ya dhana hiyo ni kwa Qatar haiwezi kuandaa kwa kuwa hali ya hewa ni ya joto.Ni muhimu kuwa na imani kama Fifa ilivyofanya Afrika Kusini 2010 na muhimu kuondosha dhana hizi".
Akizungumzia dhana ya wanawake wa mashariki ya kati kutoruhusiwa kucheza mpira na kusema Qatar washaandaa mashindano yakulipwa ya wanawake.alisema"dhana ya unyanyasaji wa wanawake ,hiyo pia ni dhana potofu".

"Tutatimiza kwa shauku ili kuhakikisha kuwa ni hatua katika historia ya mashariki ya kati na Fifa". Sheikh Mohamed alisema uamuzi wa Fifa kuwa " ni kauli ya uaminifu na upenzi wa mchezo huo". Kwa niaba ya mamilioni ya watu wa Mashariki ya kati, shukrani kwa kutuamini,shukrani kwa kuwa na mtazamo makini. Na ahidi hatutawaangusha" alisema. Umuhimu wa yote (kwa watu wa mashariki ya kati) licha ya kuona kombe la dunia toka nje kwa umbali maelfu ya maili, hatimaye yapo mlangoni.....hatimaye tumekubalika kuwa ni kiungo muhimu kwenye ulimwengu wa soka"."Kwa Fifa, tunashukuru kwa kufahamu kuwa ni muda muafaka kwa mashariki ya kati , tuna tarehe kwenye historia" alisema.
Chanzo: Aljazeera English

Hivi ndivyo Qatar walivyoweza kuishawishi Fifa

Thursday, December 2, 2010

'Afrika Yaweza Kujilisha'

Afrika ina uwezo wa kujilisha yenyewe na pia ikazalisha chakula cha kutosha kuuza nje.
Hayo ni kwa mujibu wa kitabu kipya kilichozinduliwa hii leo na professa wa chuo kikuu cha Havard Calestous Juma.

Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais Mwai Kibaki wa Kenya(shoto)
               na Pierre Nkurunziza wa Burundi kwenye mkutano wa usalama wa
chakula na mabadiliko ya hali ya hewa,leo Arusha.
 (Picha na Freddy Maro)
Kitabu hicho, The New Harvest, kinatoa wito kwa viongozi wa Afrika kutilia mkazo upanuzi wa kilimo kupitia sera na mikakati yao ya kitaifa. Kuafikia hilo, viongozi wa Afrika watahitaji kuboresha miundo mbinu, kutumia teknologia ya kisasa pamoja na kuhimiza kilimo cha mazao ya kufyatua kisayansi, yaani GM.
Ripoti hiyo itawasilishwa kwa viongozi wa Afrika siku ya Ijumaa nchini TanzaniaMarais wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanafanya kikao kuzungumzia usalama wa chakula pamoja na suala la mabadiliko ya hali ya anga.
Akizungumza na BBC kabla ya mkutano huo, Professa Juma alisema viongozi wa Afrika hawana budi kutambua uhusiano wa kilimo na uchumi wa Afrika.
''Ni jukumu la viongozi wa Afrika kuuboresha uchumi wao na hiyo inamaanisha kuanza kutumia teknonologia ya kisasa katika kilimo'', alisema.
Kwa mujibu wa Professa Juma, uzalishaji wa chakula duniani unaendelea kuongezeka lakini katika maeneo mengi ya Afrika hali ni tete licha ya kuwepo na ardhi ya kutosha ya kilimo.
Chanzo: BBC Swahili

Na Hatimaye Ni Urusi 2018 na Qatar 2022

Na hivi ndivyo ilivyokuwa
Russia 2018


Qatar 2022

Siku Ya Ukimwi Kama Ilivyokuwa Duniani


                Taiwan

                              India

worldaidslights
     U. S.A

Wednesday, December 1, 2010

Miradi Ya Kupambana Na Ukimwi Yapata Fedha Zaidi Duniani

Leo ni Siku Ya Ukimwi Duniani
Ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu hali ya ukimwi duniani: mataifa tajiri yatoa fedha zaidi.

Ripoti ya iliyotolewa jana kuhusu hali ya ugonjwa wa ukimwi na maambukizi ya virusi vya HIV duniani imesema kuwa , mataifa tajiri yameimarisha utoaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya afya katika nchi masikini , zaidi ya mara nne kati ya mwaka 1990 na 2010 , na hii inatokana kwa kiasi kikubwa na hali ya kutambua mahitaji ya kupambana na ugonjwa huo wa ukimwi.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya afya na tathmini ya chuo kikuu cha Washington , umegundua kuwa hatua ya upatikanaji wa fedha zaidi kwa miradi ya afya imeongezeka , kutoka dola bilioni 5.66 katika mwaka 1990 hadi kiwango kinachokadiriwa kufikia dola bilioni 26.87 mwaka huu.

Miradi inayohusiana na ukimwi na HIV inapata kiasi cha dola bilioni 6.16, ama karibu robo ya kiasi chote cha fedha zinazotolewa.

Ugonjwa huo wa ukimwi ambao umesababisha watu milioni 25 kupoteza maisha yao tangu pale ugonjwa huo uliporipotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1981, ni moja ya sababu ambazo zimesababisha fedha nyingi zaidi kupatikana kutoka katika mataifa tajiri kwa ajili ya mipango ya afya duniani, mwandishi wa ripoti hiyo kuhusu ukimwi duniani, Chris Murray, amesema .

Ongezeko la utoaji wa fedha kwa ajili ya afya katika mataifa yanayoendelea umechochewa kwa sehemu fulani na hisia za ubinadamu ambazo watu wengi wa mataifa ya Magharibi wamekuwa nazo , kwamba iwapo una fedha unaweza kupata matibabu ya dawa dhidi ya HIV, lakini matibabu kama hayo hayapatikani katika mataifa masikini. Hali hiyo pamoja na wanaharakati wanaopambana na ukimwi pamoja na makundi ya kutoa ushauri limekuwa ni suala kuu linalosukuma hali ya kuongezeka upatikanaji wa fedha kwa ajili ya afya duniani katika mataifa yanayoendelea.

Nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, sehemu ya dunia ambayo imeathirika sana na ukimwi, imepata kiasi kikubwa cha fedha hizo katika mwaka 2008, ambapo ilipokea kiasi cha dola bilioni 6.92, ama asilimia 29 ya jumla ya fedha zote zilizotolewa. Sehemu kubwa ya fedha hizo imekwenda kwa miradi ya ukimwi na HIV.

Wakati huo huo, watoto wengi wanaweza pia kuzaliwa bila ya maambukizi ya ukimwi iwapo jumuiya ya kimataifa itaongeza juhudi katika upatikanaji wa huduma ya matibabu ya HIV, pamoja na kuilinda jamii, ripoti hiyo ya umoja wa mataifa imesema.

Ripoti hiyo iliyotolewa na shirika la kuwahudumia watoto UNICEF limegundua kuwa mamilioni ya wanawake na watoto , hususan katika mataifa masikini wanakosa kupatiwa huduma ya upatikanaji wa dawa za kuwakinga dhidi ya maambukizi, ama na kutokana na jinsia yao ama hadhi yao ya kiuchumi katika jamii ama maeneo watokayo ama elimu yao.

Wakati watoto wamefaidika na maendeleo makubwa yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya ukimwi, ripoti hiyo imesema , hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa kuhakikisha kuwa wanawake wote na watoto wanauwezo wa kupata dawa pamoja na huduma za afya ambazo zinalenga katika kumkinga mama kumwambukiza mtoto virusi vya HIV.
Chanzo:  http://www.dw-world.de/

Ukimwi na Waendao "Dago"

Leo ni siku ya Ukimwi Duniani ili kukumbushana athari ya gonjwa hili katika jamii kwa kushauriana na kuonyesha kujali kwa waathirika wa Ukimwi.Ukimwi umeenea kwa kiasi kikubwa na takwimu zinaonesha kila jamii imepoteza wapendwa wao kutokana na ugonjwa huu na hata kuuguza waathirika.

Ishi kwa matumaini na ukinionesha kidole kimoja vitatu vinakutizama ni kauli mbiu ya wanaharakati wa kupigania haki na kuwatambua waathirika kama sehemu katika jamii yetu na wana haki ya kuishi kama mtu mwengine hadi hapo uhai wake utakapo kwisha.

Ukimwi ni gonjwa ambalo huenezwa kwa njia nyingi lakini leo nimependelea kuangalia ukimwi na waendao "dago". Dago ni kitendo cha wavuvi kutoka sehemu moja kwenda kuweka kambi sehemu nyengine kwa ajili ya kufata mavuno ya samaki. Mara nyingi kambi hiyo haingaliwi muda wala umbali muhimu kinachotizamwa ni muelekeo wa upatikanaji wa samaki(soma kilio cha kina mama juu ya waume zao wanapokwenda dago: http://www.mzalendo.net/habari/zanzibar-women-miss-husbands, )

Kutokana na mabadiliko ya maisha na msukumo wa mahitaji ya kibanadamu,jamii imejikuta ikiwa mbali na wapendwa wao kwa sababu nguvu ya uchumi imewatenganisha na kuwapelekea kukubaliana na ugumu huo.Kawaida safari moja huanzisha nyengine na ndilo hilo hupelekea kuweka dhana ya tahadhari kwani ni wengi wetu tumejikuta kusahau tuliyoyaacha kwa ahadi ya nitawakumbuka nitawajali.

Wakati nikiandika haya, takwimu zinaonesha kuwa wengi wa waathirika wa ukimwi wamepata toka kwa wapenzi wao kwa kutokuwa waaminifu. Umbali na muda wa kutokuwa pamoja umepelekea kutovumilia na kufata vishawishi vya hisia za kimwili bila tahadhari na umakini nakujikuta furaha ya muda kupelekea kugharimu maisha ya wana ndoa.

Msisitizo wa serikali ni kwa wachumba kufanya vipimo vya ukimwi kabla ya kufunga ndoa ni mzuri na umezuia maambukizi ya ukimwi kuenea kwa kiasi kikubwa. Lakini mara baada ya kupima kwa ajili ya kufata sheria mara nyingi zoezi hili haliwi endelevu ukizingatia waendao "dago" ni wengi na warudiapo nyuma kwa wapenzi wao hupokewa kwa shangwe na hamu.

Tabaani, siwezi kuamrisha watu kutumia njia za vizuizi kwani jambo hilo lina wataalamu wake na kuna mitizamo yenye kutofautiana kuhusu uhalalishwaji wake na athari yake katika jamii. Unaweza kuona migongano ya fikra mara baada ya kiongozi mkuu wa kanisa katoliki papa benedict vi aliporuhusu utumiaji wa kondomu kwa kupitia link hii: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2010/11/101120_pope_condoms.shtml

Hivyo basi ,kiushauri na kimtazamo wa kuonesha kujali itakuwa jambo la busara na hekima kama wana ndoa watachukua uamuzi wa kutizama afya zao kwani jambo hili litajenga tabia kwa wana ndoa kuwa waaminifu na hata pia kuzuia maambukizi si tu kwa mpenzi wako bali pia kiumbe kitakachopatikana kutokana na kutocheza salama.

Takwimu za maambukizo ya ukimwi zinaonesha 68% ya watu walioathirika na ukimwi duniani ni kutoka kusini mwa jangwa la sahara . Ili kuweza kushinda vita hivi lazima tukubali kubadilika lazima zoezi la kupima afya liwe endelevu- ahsante.

Video hapo chini inaelezea jinsi watoto wasio na hatia walivyo athirika na janga hili la ukimwi, endelea......

Tuesday, November 30, 2010

No Retreat No Surrender(Federer Vs Nadal)-Barclays ATP Tours 2010

Don King katikati akiwa na miamba ya Tennis Duniani
kushoto ni Roger Federer na Kulia ni Rafael Nadal
Hatimaye Roger Federer atoka mrithi mwaka huu mbele ya Rafael Nadal kwenye mashindano ya Barclays ATP Tour 2010


Monday, November 29, 2010

Nani Zaidi-Heshima

Muorinho No Comment


Ligi Kuu Ya Uingereza

Manchester United Sherehe


ArsenalFc Yatoa Nuksi


Chelsea Yavutwa Shati


Liverpool mh!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mheshimiwa Sitta Nakugeukia Okoa Kambi Ya Upinzani Bungeni

Mheshimiwa Samwel Sitta
Waziri Afrika Mashariki
Mdahalo wa juzi  kuhusu mustakbali wa kambi ya upinzani bungeni baina ya Mheshimiwa Freeman Mbowe  wa Chadema na Mheshimiwa Hamadi Rashid wa CUF umeniacha na jibu la matumaini.Kwa mujibu wa serikali kivuli ya upande wa upinzani kambi ya Chadema inadai ina haki ya kuwakilisha wapinzani hali pia CUF kwa upande wake inadai mamlaka hayo kwani inawakilisha sauti ya vyama vyengine vya upinzani vyenye wabunge.

Ni katika mdahalo huo tulipata sura ya kambi hizi mbili za upinzani na misimamo yao,Mheshimiwa Freeman Mbowe alisema alimtaka Mheshimiwa Hamad Rashid waunde serikali kivuli ya kambi ya upinzani na ikatokea tofauti ya kimtazamo kwani Chadema walitaka vyama vyengine visishirikishwe wakati CUF walisimama kwa kusisitiza ushirikishwaji wa vyama vyengine vyenye wabunge.

Hebu Tujikumbushe kidogo kwa maneno ya Mheshimiwa Hamad Rashid aliposema kuwa ni aliyekuwa Spika Mheshimiwa Samwel Sitta ndiyo aliyoasisi kwa kuwa kutanisha Mheshimiwa Hamad Rashid na Mheshima Wilbrod Slaa lakuwataka kuunda serikali kivuli ya kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa kambi ya upinzani haikuwa na sauti ya umoja.

Kwanini Mheshimiwa Sitta wa CCM tena Spika wa Bunge alichukua uamuzi huo nakuwataka wapinzani wa CCM kujiunga pamoja kuelekeza mashambulizi bungeni,hali mashambulizi yenyewe yata hatarisha uhai wa chama chake. Hayo yote aliyafanya kwa makusudi kwa sababu ya mapenzi ya nchi yake kwani kutokana na sauti ya upinzani japokuwa ni wachache wakishirikiana na vilio vya wananchi(Peoples Power) vita dhidi ya ufisadi vitafanikiwa.Ni ishara njema ya kiongozi mwenye hekima na kiukweli bunge lile la tisa lilitetemesha vigogo na kuamsha hisia za kizalendo kwa wananchi,matokeo yake si tu Chadema kuibuka na viti vingi bungeni hata CUF wamefanikiwa kupata viti viwili vya Ubunge Tanzania bara hii imevunja kawaida na kuipa homa chama tawala.

Leo narudi kwako ukiwa kama Waziri wa Afrika Mashariki nikijua fika utapokea pole toka kwa majirani zetu kwa kutofanikiwa kutetea kiti chako cha uspika. Na ndio huko pia kutakako kukumbusha kazi yako ya kuitaka Tanzania iwe nchi safi dhidi ya ufisadi na katiba mpya kuwa hujaimaliza. Kwani ni tegemeo lako kuwaambia nchi nyengine za Afrika mashariki licha ya kuanguka katika uspika nina fahari ya kuwa mafisadi wamefikishwa mahali hawana pa kujificha nakwamba nchi yangu ina katiba mpya kama wenzetu wa KENYA.Na kwamba leo hii unasimama mbele yao kifua mbele, ukiwatamkia Tanzania ina utawala wa sheria na kuwataka majirani zako ili kufikia lengo la soko la pamoja lazima muige toka Tanzania.

Hayo yote yanawezekana kwa kuwa siri ya umoja wa kambi ya upinzani uliyo uasisi imefungua macho wa Tanzania basi ndiyo wewe  unaeweza kuikoa kambi hii. Kwani bunge hili  tunategemea kutoa changamoto zitakazolifikisha Taifa katika muelekeo mzuri hasa pale kambi ya upinzani kwa idadi ya wabunge wao wa mwaka huu na wale wa CCM wanaopendelea mabadiliko watakapo ungana na kuwashinda mahafidhina.

Jeshi La Brazil Latangaza Ushindi Dhidi Ya Magenge Ya Madawa ya Kulevya

Lakini yasisitiza operesheni inaendelea

Kuuawa Mwanasayansi wa Nyuklia-Iran Yazishutumu Marekani na Israel


Mashambulio mawili ya bomu la Kuegeshwa kwenye gari nchini Iran
limeua mwanasayansi wa nyuklia na kujeruhi mwengine.

Mahmoud Ahmednajad,Rais wa Iran amezishutuma nchi za Marekani na Israel kuwa zipo nyuma ya mashambulio mwawili yaliotokea leo na kuua mwanasayansi mmoja wa myuklia na kujeruhi mwengine.
Amesema"Pasi shaka kuna mkono wa wazayuni na mataifa ya magharibi uliohusika" katika mauaji haya. Lakini amesisitiza mashambulizi ya kushtukiza hayata izuia Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia.
Mohamed Reza Rahimi,Makamu wa Rais wa Iran ameishutumu israel nakuwaita kuwa "wamebeba silaha za ugaidi".Mwaka huu Iran imeshuhudia ikiuawa wanasayansi wake wawili wa nyuklia

Wakati hayo yakijiri, leo tena imetolewa kashfa ya simu ikimuhusisha Mfalme Abdullah  wa Saudi Arabi pamoja na chi za Ghuba kuishawishi Marekani kuishambulia Iran kuharibu mpango wake wa nyuklia.Kasjfa hiyo imetolewa na Jarida la WIKILEAKS.
Rais wa Iran,Mahmoud Ahmednajad amesema" hawatilii  nyaraka hizo maanani, kwa kuwa hazina uzito wa kisheria .Iran na majirani zake ni marafiki.Kitendo hicho kiovu hakina athari za mahusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi". Aliendelea kusema"hizi nyaraka zimeandaliwa na kutolewa na serikali ya marekani kwa ajili ya mpango maalumu ili kutekeleza azima yake.Ni sehemu ya vita vya ujasusi na hiyo haina athari ya kisiasa kama wanavyotaka".
Chanzo: http://english.aljazeera.net/news/middleeast/2010/11/20101129131235776706.html

Sunday, November 28, 2010

Kombe La Chalenji Zanzibar Heroes Na Rwanda Zaanza Vizuri


Salum Shimboli wa Zanzibar Heroes akishangilia baada ya
kufumania nyavu mara ziloipa ushindi wa mabao 2-0 dhidi
ya Sudan.

Wachezaji Wa Zanzibar heroes wakishangilia baada ye mechi kuisha

Golikipa Wa Rwanda, Jean Ndayishimiyei akiokoa hatari.
Timu ya Rwanda waliibuka kidedea kwa goli 2- 1 dhidi ya
Ivory Coast.

Mgogoro Wa Uongozi Waibuka Katika Chama cha soka cha Zambia (FAZ)

Kalusha Bwalya
Kalusha Bwalya
Kundi hilo limesema kamati inayoongozwa na Rais wa FAZ Kalusha Bwalya, haishiki tena hatamu za uongozi.
Wamesema kamati iliyopita imejiondoa yenyewe baada ya wajumbe wake wanne kujiuzulu siku ya Jumamosi.Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia, Kalusha Bwalya, aliwarejesha baadhi ya wanachama wa kamati yake baada ya wengine kujiondoa, ili kuweza kuwa na wajumbe wanaohitajika.
Mkutano wa siku ya Jumamosi ni wa kuidhinisha hatua hiyo na mwakilishi wa Fifa atahudhuria.
Lakini wajumbe watatu kati ya wanne waliowekwa na Bwalya wamekataa uteuzi huo
Kundi hilo la upinzani linajumuisha maafisa waandamizi kwa mchezo wa soka nchini Zambia, wakiwemo mkuu wa chama wa cha waamuzi na wawakilishi wa vilabu kadhaa.
Kamati hiyo mpya imesema wajumbe wake wamechaguliwa kwa ajili ya kufanya kazi kwa muda tu na uchaguzi mpya unatakiwa kufanyika ndani ya siku 90.
Chanzo:BBC-Swahili

Wakati hayo yakiendelea ,Timu ya ya Tanzania The Kilimanjaro Stars imeanza vibaya mashindano ya chalenji baada ya kufungwa bao moja kwa nunge dhidi ya Zambia.Rais Jakaya Kikwete, akipiga mpira ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi michuano ya CECAFA Tusker Challenge Cup, yaliyoanza jijini Dar es Salaam jana jioni katika Uwanja wa Taifa kati ya Timu ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania na Zambia, Kilimanjrao imefungwa bao 1-0.Kiungo mshambuliaji wa Kilimanjaro, Mrisho Ngasa akimnyanyasa beki wa Zambia wakati wa mchezo huo .

Baadhi Ya Picha za Sherehe Ya Kuapishwa Mawaziri Na Naibu Mawaziri Ikulu


Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Maria Nagu
akifurahi jambo na Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Mwinyi katika viwanja vya Ikulu.

Mh. Benard Membe akisalimiana na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh.Shamsi
 Vuai Nahodha katika viwanja vya Ikulu

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete
katika picha ya pamoja na Baraza lake Jipya baada ya shughuli za kuapisha
Mawaziri na Manaibu wake.

Mdahalo wa Freeman Mbowe(Chadema) na Hamad Rashid(CUF)-Kuhusu Kambi Ya Upinzani Bungeni

Sehemu ya Kwanza

Sehemu Ya Pili

Sehemu Ya Tatu

Sehemu Ya Nne
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...