Mtazamohalisi

Sunday, November 14, 2010

Chelsea Yalala 3 Kwa Nunge Dhidi Ya Sunderland

Siku chache baada ya kuvunja ndoa na kocha msaidizi Ray Wilkins,timu ya Chelsea imejikuta ikipata kichapo cha mbwa mwizi kwa kufungwa mabao 3 na sunderland bila majibu.
Wakicheza uwanja wa nyumbani,chelsea imeshindwa kufurukuta mbele ya watazamaji 42,072.


Ray Wilkins
Hata hivyo ,Chelsea inaendelea kushika usukani wa ligi  kuu ya uingereza kwa pointi 28 ikifuatiwa na Arsenal pointi 26 na Manchester United pointi 25.Wakati huo huo,Westham inaendelea kushika mkia ikiwa ina pointi 9 sawa na wolverhampton ila kwa tofauti ya goli  moja huku  Birmingham ikiwa na pointi 13 nakuwacha kwa pointi 4.

Matokeo ya mechi za wikiendi hii ni Chelsea 0- Sunderland 3, Everton1-Arsenal 2 , Aston Villa 2- Manachester United 2, Man City 0- Birmingham 0, Newcastle 0- Fulham 0, Stoke 2- Liverpool 0, Totenham 4- Blackburn 2, Westham 0- Blackpool 0, Wigan 1- West Brom, Wolverhampton 2- Bolton 3.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...