Mtazamohalisi

Monday, November 15, 2010

Tujikumbushe, Omar Rashid Nundu


Mhandisi Omari Nundu(Akipokea zawadi toka kwa mwenyekiti wa bodi ya TCCA   Mh.Mwantumu Malale baada ya kuteuliwa kwa mara ya kwanza) amechakwa mara ya pili kuwa Rais wa tume ya Ufundi ya Shirika la  kimataifa la  usafiri wa anga Duniani.

 Tukio hili lilitokea  mwaka 2007  na baadae mwaka 2008 akateuliwa tena kukalia kiti hicho, na amekuwa mwafrika wa kwanza kupata nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 29 iliyopita.
Kwa kuchaguliwa kwa mara ya pili kwa nafasi hiyo,Mhandisi anavunja kawaida ya miaka mingi kwamba nafasi hiyo inashikwa kwa kipindi kimoja tu.

Omari Nundu, Mbunge mteule toka jimbo la Tanga Mjini  katika kipindi hiki  cha mpito kuelekea kuteuliwa baraza la mawaziri kwa sifa zake hizo anafaa kuingia katika baraza jipya la mwaziri.
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, huyo ni miongoni mwa waziri watakao kusaidia sana katika uongozi wako hasa katika marekebisho ya uendeshaji wa shirika la ndege ATCL.

Desemba 9 mwaka huu Taifa litatimiza miaka 49 ya Uhuru  tukiwa tunajivunia amani na utulivu, tunaomba changamoto ya kuwa na shirika la ndege lenye nguvu kuweza kushindana na mataifa jirani ya Kenya  na Rwanda.

1 comment:

  1. ni kweli kabisa, mzee wetu si kuwa tu anatokaa tanga bali pia ni mtu aliesafiri na kupata uzoefu mwingi ambao akiamua kuutumia kuindeleza jamii ya kitanzania hakika tutafika mbali.

    hasa katika kipindi hiki cha maendeleo ya teknolojia itafaa sana kupata mtu ambae amekutaa na watu wengi, wasomi na wenye kujua namna ya kuishi na jamii zinazohitaji maendeleo. Rais Kikwete tafadhali lioe hilo. Hafidh Kido.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...