Mtazamohalisi

Thursday, February 10, 2011

Wasanii na Upepo wa Siasa

Mabadiliko ya kisiasa huacha wasanii  katika hali ngumu ya kuamua ikiwa wakumbatie utawala uliopo au kuunga mkono wnaaodai mabadiliko.

Msanii kama kioo cha jamii huacha athari pale anapounga mkono upande mmoja dhidi ya mwengine. Na hilo humuweka katika hali ya sintofahamu hasa pale upande anaoupigia debe ukiwa haukubaliki na wengi.

Wapo walionufaika na hilo wapo waliohatarisha maisha yao, nakupelekea kuanguka kimvuto na kazi zao kutothaminika.

Uchaguzi mkuu wa rais na wabunge ulifanyika oktoba ,2010 na kuwagawanya wasanii wetu kugawanyika pande mbili .Kambi ya Chama tawala CCM licha yakuwa na bendi yao ya TOT walikuwa na wasanii wengine kama Marlow na kwa upande wa upinzani hasa Chadema walikuwa na wasanii kama MR II maarufu kama Joseph Mbilinyi  ,Mbunge wa Mbeya Mjini na Fred Maliki maarufu Mkoloni.

Wapo waliokuwa  watazamaji na wapo waliobadili upepo mwishoni kama Nakaaya Sumari yaani muhimu uelewe ya kuwa kwa njia moja au nyengine upepo wa siasa unawaathiri sana wasanii kuliko mwananchi wa kawaida.

Hayo yakijiri nyumbani hali hiyo imewakuta hata wasanii wa nje,huko Misri ambako vuguvugu la siasa la kudai mabadiliko dhidi ya rais Hosni Mubarak umewaacha wasanii wakiwa ni wahanga wa upepo wa siasa.

Ni hivi karibuni msanii maarufu wa nchi hiyo Tamer Hosny ambaye alitumia nafasi yake kuwashawishi vijana kuilinda Misri kwa kuacha maandamano na kurudia maisha ya kawaida.Amejikuta kwenye hali ngumu mara upepo wa mabadiliko ulipomvuta hadi uwanja maarufu wa Ukombozi  yaani Tahrir Square (Liberization Square) nakujikuta akipata kichapo huku akijitetea kuwa alilanguliwa na Television ya Misri nakuwa hakuwa na nia mbaya na ameshatunga nyimbo ya Mapinduzi kuashiria kuunga mkono mabadiliko.

Tamer Hosny alivyo chezea kibano

Tamer Hosny moja ya nyimbo zake

Marlow na pipi

Saturday, January 29, 2011

Sauti Ya Umma Wa Misri

Cliton on Egypt ptotest


OBAMA ON EGYPT PROTEST


Mubarak avunja baraza la Mawaziri na kutangaza Mabadiliko

Sauti Ya Amerika na Mabadiliko Misri


Waandamanaji wakionesha hasira zao kwa Utawala wa Mubarak

Ilikuwa ni Ijumaa nzito kwa kipindi cha miaka  30 cha utawala wa Hussein Mubarak(82), siku ambayo wingu la mabadiliko ya siasa ulipofunga na kusababisha mpasuko wa radi uliotingisha si tu utawala wa Misri bali na tawala nyengine duniani.

Haikuwahi Mji wa Cairo kuwa moto tangu mapinduzi ya mwaka 1952,lakini mshuko wa Ijumaa wa january 28,2011 ulithubutu kuvunja duru za usalama za nchi hiyo na kuonesha dunia kile ambacho wanakipigania yaani mabadiliko.

Imetosha, ni kauli kuu ya waandamanaji kuashiria kukata tamaa na mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa na kijamii. Hali mbaya ya maisha kutokana na ukosefu wa ajira,gharama za maisha kupanda na uhuru wa kujieleza,rushwa na uasimu ndio vichocheo vilivyoamsha umma wa Misri na kumtaka Mubarak kuondoka madarakani.

Mwezi desemba Misri ilifanya uchaguzi wa wabunge wa duru ya pili na chama tawala cha National Democratic Party (NDP)   kujipatia ushindi mnono wa 80% na upinzani kujipatia 20%.Hata hivyo kelele za kubatilisha matokeo hayo ambayo upinzani ulisusia toka duru ya kwanza ya uchaguzi mwezi novemba linalifanya bunge hilo kuwa ni la chama kimoja bila mwakilishi toka upinzani.

Hapo jana utawala wa Marekani  ambao ni mshirika mkuu wa utawala wa Mubarak ambayo hutoa kiasi cha Dola 1.5 bilioni kila mwaka, umeitaka Misri kuheshimu uhuru wa kujieleza na kuruhusu maandamano,pamoja na kuwaacha huru waandamanaji na kuruhusu mitandao kufanya kazi huku ikiisisitiza Misri kusikiliza kilio cha Umma na kukubali mabadiliko.

Kutokana na shinikizo la ndani na nje ya nchi,Rais Mubarak ametangaza kulivunja baraza lake la Mawaziri na kuunda jipya hali yeye akiwa bado kiongozi mkuu atakae endeleza mabadiliko ya nchi katika muelekeo wa Misri Mpya.

Septemba,2011 kutakuwa na uchaguzi wa Rais wa Misri ambao kwa hali ilivyo upepo wa siasa unaelekea kuwa mbaya kwa Mubarak na chama chake.

Friday, January 28, 2011

Mganda Atumia Kigezo cha Ushoga Kudai Haki Ya Ukimbizi

Hatua kali ya sheria ya ushoga nchini Uganda kumempelekea Brenda Namigadde,mwanamama wa kiganda kuiomba serikali ya Uingereza kumfikiria kupata haki ya ukimbizi kuliko kurudishwa nchini Uganda.

Kwa mujibu wa mwanamama huyo ambaye amedai ni Msagaji na kwamba ni uvunjaji wa sheria nchini kwake kuwa na uhusiano wa jinsia moja hivyo kurejeshwa kwake kutahatarisha maisha yake.

Kwa mujibu wa sheria ya Uganda, ni marufuku kuwa na uhusiano wa mapenzi na mtu wa jinsia moja na yeyote atakae vunja sheria hukumu yake ni miaka 14 licha ya juhudi kubwa kugonga ukuta kwa baadhi ya wabunge waliofika mbali nakutaka "hukumu ya kifo" itumike.

Wiki hii nchini Uganda imeshuhudia mtetezi mkuu wa haki za mashoga David Kato  akiuawa na mtu asiyejulikana mara baada ya kuvamiwa nyumbani kwake,nakifo chake kimeibua hisia za watetezi wa haki za binadamu na wapenzi wa haki za mashoga kuhofia usalama wao.

Kwa mujibu wa hukumu ya Bi.Brenda Namigadde, wizara ya mambo ya ndani imeshindwa kujiridhisha na ushahidi alioutoa kwa kuwa hana vidhibitisho kuwa yeye ni Msagaji.Hivyo madai yake batili.

Hata hivyo Bi Breanda Namigadde amekata rufaa na kupeleka vielelezo zaidi ili kuiridhisha idara ya mambo yandani ya Uingereza ambayo imevipokea na kuanza kuvipitia.

Ikiwa ushahidi hautotesheleza vigezo kwa mujibu wa sheria ya Uingereza ,basi muhusika itampasa kufunga virago.

Umoja wa mataifa kupitia kamishna wake wa masuala ya wakimbizi Bw.Antonio Guterres amenukuliwa akizitaka mamlaka za kimataifa kuwapokea wakimbizi toka Uganda waliokimbia kutokana na maisha yao kuwa hatarini.
Chanzo:  BBC

Video ya David Kato kabla na baada ya Mauaji yake

Thursday, January 27, 2011

Mlinzi wa Hitler Bado Wamo


Rochus Misch mlinzi wa Hitler kwa muda wa miaka 5 alishuhudia
Hitler akijiua.

Zaidi ya miaka 65 tangu kwisha kwa vita ya pili ya dunia mlinzi wa mwisho wa Hitler anasema kwa hivi sasa hawezi kujibu e-mails kutokana na umri wake.

Rochus Misch,miaka 93 alishuhudia Hitler akijiua mara baada ya kuona kifaru cha jeshi la Urusi kimkaribia.Aliwahi kubadilishana uzoefu na Christopher McQuarrie,mwandishi aliyetengeneza Valkyrie filamu ya mwaka 2008 ikielezea jinsi Hitler alivyojiua.

Mcheza sinema wa Hollywood ,Tom Cruise ambaye aliigiza katika filamu hiyo hakutaka kukutana na Misch na kuliambia gazeti la Los Angeles Times kuwa"shetani ni shetani,haijalishi umri aliokuwa nao".

Amenukuliwa na gazeti la Berliner Kurier ya kwamba hawezi kujibu barua pepe anazotumiwa kutokana na umri aliokuwa nao.

Mwezi January 16 ,1945 kufuatia Ujerumani kushindwa vitani Misch na wasaidizi wa karibu wa Hitler walikimbilia F├╝hrerbunker katika jiji la Berlin. Nakujitokeza kwake mara baada ya vita, alijikuta akitiwa mikononi na Jeshi Jekundu . Aliachiwa huru mwaka 1954, na tangu wakati huo na hadi sasa Misch anaishi katika jiji la Berlin.

Kwakujua alivyokutana na Hitler na majukumu yake endelea......Hitler

Watch Valkyrie Trailer

Hitler Private resident

Wednesday, January 26, 2011

Waarabu Wataka Mabadiliko

        Tunisia yataka Ben Ali akamatwe          
Waziri wa sheria wa Tunisia amesema nchi hiyo imetoa hatia ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais aliyekimbia Zine al-Abidine Ben Ali na familia yake.


Lazhar Karoui Chebbi alisema Tunisia imeiomba shirika la polisi la kimataifa Interpol kumkamata Ben Ali, aliyekimbilia Saudi Arabia mapema mwezi huu kufuatia maandamano makubwa nchini humo.

Bw Chebbi alisema Bw Ben Ali ashtakiwe kwa wizi wa mali na kuhamisha patoa la taifa la fedha za kigeni.

Aliyasema hayo huku maandamano ya kuipinga serikali yakiendelea.

Chanzo: BBC

Maandamano Tunisia
Nyumba Ya Familia Ya  Rais Ben Ali  Yavamiwa


Mitandao imerahisisha sauti ya Umma


Misri kwafuka Moto Licha Vitisho Vya Serikali
kwa kuweka waandamanaji 500 kizuizini nakuua 4
 Marekani  Yaitaka Misri kuruhusu Maandamano
 

Palestina yajibu kuhusu 'nyaraka za siri'

Maafisa wa Palestina wameishutumu al-Jazeera kwa kupotosha, baada ya kutoa taarifa za siri zilizokusudia kuonyesha nchi hiyo kuwa na maridhiano makubwa na Israel.

Rais Mahmoud Abbas alisema siri hizo zimechanganya kwa makusudi misimamo ya Palestina na Israel.

Nyaraka hizo zinasema kuwa Palestina iliikubalia Israel kubaki na eneo kubwa la mashariki mwa Israel wanalomiliki kinyume cha sheria- jambo ambalo Israel imelikataa.

BBC imeshindwa kuthibitisha binafsi nyaraka hizo.

Al-Jazeera ilisema ina rekodi 16,076 za siri za mikutano, barua pepe, na mawasiliano baina ya Palestina, Israeli na viongozi wa Marekani, baina ya mwaka 2000-2010.

soma zaidi....... BBC

Kupitia Nyaraka zenyewe gonga hapa http://english.aljazeera.net/palestinepapers/

Maoni Ya Wachambuzi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...