Mtazamohalisi

Saturday, November 13, 2010

Haile Gebrselassie Atangaza Kustaafu Mbio

Haile Gebrselassie
                                                                                                                                                              
Usain Bolt akiwa na Haile Gebrselassie
Haile Gebrselassie ,nguli wa mbio ndefu duniani atangaza kustaafu, kwa kushindwa kumalizia mbio na kuishia umbali  wa maili 16 baada ya maumivu ya kuwa na maji kwenye goti la kulia. Alikuwa akishiriki mbio za nyika za jiji la Newyork.

Amesema "hakufikiria kustaafu" "lakini kwa mara ya kwanza leo hii imebidi.Imefika wakati wa kuangalia shuguli nyengine".Aliongezea kwa kusema" Nimeona wana michezo wengi wakipanga muda wa kustaafu. Anasema  haiwi hivyo. Siku ambayo umetangaza kustaafu, basi ndiyo tayari umestaafu kwenye akili yako".

Haile Gebrselassie ameweza kuvunja rekodi za dunia 27, zikiwamo mbio za nyika za mita 5000 na mita 10000. Ameshinda medali ya dhahabu mwaka 1996 katika mbio za mita 10000 huko Atlanta na mwaka 2000 Sydney Olympics.

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 10000 toka 1993- 1999, kwa muda wa miaka minne mfululizo.
Ni mkimbiaji mwenye kasi kwa umbali wowote  kwenye kumbukumbu za mbio, toka dakika 3:31.76 sekunde kwenye umbali wa mita 1500 hadi masaa 2 na dakika 3 na sekunde 59 kwa mbio za nyika. Mwaka 1999 hadi 2000 hajawahi kushindwa katika mbio zozote alizoshiriki kwa muda wa miaka 2 mfululizo.

Hakika, utakumbukwa kwa kuliletea bara la Afrika heshima. Uzoefu unaonesha, itachukua muda kupata mrithi wako. Hata Tanzania , hadi leo hii hawajapata wanariadha walioliletea Taifa heshima kama Filbert Bayi na Juma Ikangaa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...