Mtazamohalisi

Friday, November 12, 2010

Anna Makinda Kama Nancy Pelosi

Spika Mpya wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Bi.Anna Makinda

Ameshinda Uspika kwa kura 265 dhidi ya 53 za Mabere Marando.
Kwa ushindi huo, anafungua ukurasa mpya katika siasa za Tanzania kwa kuwa Mwanamke wa kwanza
kukalia kiti hicho cha uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Marekani ni miongoni mwa wanawake wa chache waliyo bahatika kushika nyadhifa nyeti kama ya Uspika.

Mheshimiwa Anna Makinda ,mbunge toka Njombe kusini kama Spika wa kwanza
Mstaafu Chifu Adam Sapi Mkwawa anaweka  historia kwa mkoa wa Iringa kwa  mara ya pili kuweza kutoa Spika.

Tunakutakia mafanikio mema katika majukumu yako ya kulifikisha Taifa mbele kwa salama na amani,
kwa uzoefu wako pamoja na hekima na maarifa tunatarajia utakabiliana vyema na changamoto za muhimili huu muhimu wa dola.Mungu atakusaidia, hongera.

1 comment:

  1. hilo ni chaguo la wote. afadhali watanzania tumepiga hatua, na kuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na mwanamke spika... kido.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...