Kamati Kuu ya CCM imependekezea majina yafuatayo kugombea Uspika:
1. Anna Makinda
2. Anna Abdallah
3. Kate Kamba
Kwa hivyo Mzee wa Vijisenti out, Sitta out!!!
Source: Channel 10 News Bulletin 3 minutes ago
Kimuelekeo inaonesha CCM inataka kujijenga upya, kutokana na nyufa zilizosababisha kupoteza viti vingi bungeni. Na hii imetokana na kuwa na kambi kuu mbili za Spika Mstaafu Mh.Samuel Sitta na ile kambi ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa nawashirika wake Mh. Andrew Chenge.
Spika ajaye kama picha inavyo jionesha, atakuwa ni Mwanamke kwa maana Tanzania itafungua ukurasa mpya wa kuwa na kiongozi wa kwanza Mwanamke kuongoza muhimili muhimu wa dola.
Kwa moyo mkunjufu, tunakaribisha changamoto hii mpya kama ishara ya kuiambia dunia ya kuwa Tanzania tumekomaa kidemokrasia na tupo tayari kuondokana na mtazamo wa kihafidhina unaopendelea mfumo dume.
No comments:
Post a Comment