TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeidhinisha majina 88 ya wabunge wateule wa viti maalumu wa vyama vya CCM na Chadema na kutenga viti kumi kwa Chama cha wananchi (CUF) ambacho hakuwasilisha mapendekezo ya wanaowania nafasi hizo.Katika hatua hiyo Nec imeacha nafasi nyingine sita wazi kusubiri chaguzi za ubunge katika majimbo saba ambayo upigaji kura uliahirishwa. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana Jijini Dar es Salaam jana chama cha CUF bado hakijawasilisha orodha ya majina ya wanawake watakaowania viti maalumu, lakini orodha hiyo ya Nec inaonyesha kuwa baadhi ya wabunge waliokuwemo wako hatarini kuachwa huku waliko katika nafasi za kwanza katika vyama vyote wakiwa na matumiani ya kupeta.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame aliliambia Mwananchi jana kwamba baada ya kukokotoa uwiano wa viti hivyo maalumu, CCM iliongoza kwa kupata viti 65, ikifuatiwa na Chadema viti 23 wakati CUF kimeambulia viti 10 pekee. Jumla ya viti vyote ni 104.
Katika bunge lililopita ambalo lilikuwa na viti 75 maalumu CCM ilikuwa na viti 58, CUF viti 11 na Chadema viti sita na safari hii vimeongezwa hadi kufikia 104 na mgowanyo wake ukiwa kama ulivyoonyeshwa kwa kuingazia uwiano wa wingi wa kura za ubunge.
Akizungumzia namna Nec ilivyokokotoa mgawanyo wa viti hivyo na kupata uwiano kwa kila chama, Jaji Makame alisema kisheria walivigawanya kutokana na wastani wa kura za wabunge. Kura hizo ni zile ambazo kila chama kilizipata kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote Oktoba 31.
Kwa mujibu wa Makame, tayari Nec imeishawaandikia CUF barua mbili kwa nyakati tofauti kuitaka ipeleke orodha hiyo bila mafanikio.
“Tumeshawaandikia barua mbili kuwakumbusha juu ya hatua hiyo ya kwanza Agosti na ya pili Novemba mwaka huu lakini hawakutujibu,” alibainisha Jaji Makame akisema viti hivyo vitabakia wazi hadi CUF itakapowasilisha orodha hiyo.
Kuhusu viti sita vilivyoachwa wazi, Makame alisema vinasubiri matokeo ya majimbo saba ambayo uchaguzi wake haujafanyika.
Majimbo ambayo uchaguzi wake uliahirishwa ni Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini na Nkenge, yote ya Tanzania Bara na mengine manne ya Tanzania visiwani ambayo ni Mwanakwerekwe, Mtoni, Magogoni na Wete.
Alisema vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo, havikupata wabunge hao wa viti maalum kutokana na kushindwa kufikisha asilimia tano ya kura za urais.
“Sheria inasema, ili chama kipate wabunge wa viti maalum, kinatakiwa angalau kipate asilimia tano ya kura za urais hali ambayo vyama vingine havikutimiza,” alisema Makame.
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zilieleza kwamba Nec itatangaza majina ya wabunge wateule wa viti maalumu kwa vyama vya CCM na Chadema leo.
Hata hivyo, Mwananchi lilifanikiwa kupata orodha za majina zinazodaiwa kuwasilishwa Nec na vyama hivyo.
Orodha hizo zinadawa kupangwa kulingana na uzito wa nafasi ya kuteuliwa.
Kutokana na Nec kuitengea CCM nafasi 65, majina ya wanawake ambao wana nafasi kubwa kuwa kwenye orodha ya uteuzi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba, Gaudentia Kabaka, Ummi Mwalimu, Agness Hokororo, Martha Umbulla, Lucy Mayenga, Faida Mohamed Bakari, Felista Bura, Kidawa Hamid Saleh na Stella Manyanya.
Wengine ni Maria Hewa, Hilda Ngoye, Josephine Genzabuke, Esther Midimu, Maida Hamad Abdalla, Asha Mshimba Jecha, Zarina Madabida, Namalok Sokoine, Munde Abdallah na Benardetha Mushashu.
Pia wamo Vick Kamata, Pindi Chana, Fatuma Mikidadi, Getrude Rwakatare, Betty Machangu, Diana Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Vulu, Abia Nyabakari na Pudenciana Kikwembe.
Lediana Mng’ong’o, Sarah Msafiri Ally, Catherine Magige, Tauhida Galos Cassian, Asha Mohamed Omari, Rita Mlaki, Anna Abdallah, Fenella Mukangara, Terezya Huvisa na Al-Shaymaa Kwegir.
Margreth Mkanga, Angellah Kairuki, Zainab Kawawa, Mwanakhamis Said, Riziki Lulida, Devotha Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Mfaki, Margreth Sitta na Subira Mgalu.
Rita Kabati, Martha Mlata, Dk Maua Daftari, Elizabeth Batenga, Azza Hamad, Mary Mwanjelwa, Josephine Chengula, Bahati Abeid, Kiumbwa Mbaraka na Roweete Kasikila.
Anastazia Wambura, Mary Chatanda, Rosemary Kirigini,
Mariam Kisangi na Kemilembe Lwota.
Walioko katika hati hati ya kutokuwapo kwenye orodha hiyo ni Tinner Chenge, Mwandishi wa habari, Kaslida Mgeni, Mboni Mhita na Janet Masaburi.
Kwa upande wa Chadema, 23 wenye nafasi kubwa ya kuwepo ni Lucy Owenya, Ester Matiko, Mhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekuli na Conchesta Rwamlaza.
Wengine ni Suzan Kiwanga, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu, Regia Mtema, Christowaja Mkinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Chiku Abwao.
Pia wamo Naomi Kaihula, Grace Kiwelu, Rose Kamili, Christina Lissu Mughiwa, Raya Ibrahim, Philipa Mturano, Miriam Msabaha, Rachel Mashishanga.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment