Mtazamohalisi

Monday, December 13, 2010

DK. REMMY ONGALLA AFARIKI DUNIA


 Marehemu Ramadhani Mtoro Ongala


Aliyewahi kuwa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchi, na baadaye kuokoka na kuhamia katika muziki wa Injili, Dk. Remmy Ongala, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa amelazwa kwa kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Marehemu Remmy ambaye alikuja nchini mwishoni mwa miaka ya 70 na kujiunga na bendi ya Makasy, amechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa dansi hapa nchini akiwa na bendi hiyo na baadaye Super Matimila.

Wimbo wake wa Pesa ambao alitumia mtindo wa Talakaka, ulivuma sana mwanzoni mwa miaka ya 80 na baadaye wimbo wa Tembea Ujionee.

Mwanamuziki huyo alipata sifa kubwa na kupata mwaliko wa kwanza kutumbuiza katika tamasha la Womad nchini Uingereza.

Dk. Remmy atatakumbukwa sana na nyimbo zake nyingine kama safari siyo kifo, Kifo, Dodoma, kipenda roho na nyinginezo nyingi.

Maandalizi ya mazishi yanaendelea kufanyika nyumbani kwake, Sinza kwa Remmy. Mungu amlaze mahali pema, Amen.

Dk.Che mponda akiongea na mke wa Dk.Remmy Ongalla alipokweda
kumtembelea.Mumewe,Dk Remmy naye alilazwa hapo Mwaisela.
(ilikuwa tar.3/desemba/2010,Dk Remmy aliruhusiwa kutoka hospital)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...