Mtazamohalisi

Friday, December 3, 2010

Kweli Madaraka Matamu-Bagbo Ahujumu Ushindi Wa Upinzani Ivory Coast

Matokeo ya Rais wa Ivory Coast yapo kwenye hatihati baada ya tamko la baraza la katiba la nchi hiyo kutaka kutangaza matokeo yao,punde tu tume ya uchaguzi ilipomtangaza kiongozi wa upinzani kuwa mshindi.

Wafuasi wa Rais aliyeshindwa Laurent Bagbo wameita tangazo la siku ya alhamisi kuwa ni "mapinduzi yaliyoshndwa".Mipaka yote ya nchi jirani za Afrika Magharibi imefungwa siku ya ijumaa,television na radio za kigeni pamoja na ujumbe mfupi wa simu kufungiwe kwa muda usiojulikana huku nchi ikiwa katika hali ya tahadhari.Uwezekano wa  wananchi kupata taarifa ni kwa njia ya satelite tv.

Upigaji kura kwa nchi hii ni kurudisha hali ya amani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002-2003 ambavyo vililigawa taifa hili maarufu kwa zao la kokoa pande mbili, lakini hali tete siku ya ijumaa imekuwa kama makali ya kisu.Marekani imezitaka pande zote zinazohusika kukubaliana na matokeo yaliyompa kiongozi wa upinzani Alasane Ouattara ushindi.

Rais Obama ametilia uzito matokeo hayo na kumpa pongezi Alasane Outtara kwa ushindi,na kumtaka rais aliyeshindwa Laurent Bagbo kukubaliana na matokeo ambayo yamethibitisha na umoja wa mataifa.

Taarifa ya matokeo zimeleta utata mkubwa,na kutangazwa kwa rais wa sasa Laurent Bagbo kuwa mshindi na baraza la katiba la nchi hiyo kumewaacha wananchi kutoelewa nini kinaendelea kwa kuwa matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi inayokubalika na Umoja wa Afrika ,Umoja wa Mataifa na Marekani yalionesha kuwa  Alasane Ouattara 54.1% na Laurent Bagbo 45.9%  .

Matokeo mapya yaliyotangazwa na baraza la katiba limempa ushindi  rais wa sasa Laurent Bagbo kwa 51% ,huku akiibukia kupata kura 500000 kwenye ngome ya Ouattara ambayo ni 10% ya wapiga kura na kubatilisha matokeo ya  majimbo 7 kati ya 19 kwa madai ya wafuasi wa Bagbo walipokea vitisho toka kwa wahuni.

Mara ya matokeo hayo Umoja wa mataifa umeyakataa matokeo hayo ya baraza la katiba nakuyaita ni batili huku ikibaki na msimamo wa kuyatambua matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yaliyompa ushindi Alasane Ouattara.
Chanzo: Associated Press

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...