Mtazamohalisi

Friday, December 3, 2010

Obama: Qatar Haikustahiki Kuandaa Kombe La Dunia 2022

Rais wa Marekani amesema Fifa wamefanya kosa kuipa Qatar kuandaa kombe la dunia 2022 badala ya nchi yake."Nafikiri ni uamuzi wa makosa"Obama aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani.Amesema alitarajia  ujumbe wa Marekani ungefanikiwa mwishoni.

Fifa wameiteua Qatar dhidi ya Marekani,Japan,Korea na Australia kuandaa kombe la dunia 2022.Na Urusi kufanikiwa kuandaa kombe la dunia 2018.

Shirikisho la soka la Marekani limetumia mamilioni ya dola kupeleka ujumbe wake ili kuishawishi Fifa kuichagua ukiwamo ujumbe mzito unaongozwa na rais wa zamani wa Marekani Bill Cliton ambaye alijumuika kwa juhudi zote hadi siku ya mwisho ya kuwakilisha mapendekezo.

Ujumbe mkuu wa watetezi wa uandaaji wa Marekani ni tumaini la kuandaa tena kombe la dunia badala ya lile la 1994 ili kuinua kiwango cha soka huko Marekani.

Wakati huo huo Qatar imepongeza uamuzi huo wa siku ya alhamisi na kuuita ni ushindi dhidi ya dhana potofu kwa nchi yao kuwa haina sifa ya uandaaji wa kombe la dunia 2022.Mwanzoni Qatar iliwekwa nje ya matarajio kwa kuwa wengi waliiona ni nchi ndogo ambayo haina sifa ya uandaaji wa mashindano makubwa kama hayo.

Na sasa litakuwa taifa la kwanza dogo kuandaa mashindano hayo, baada ya kuweza kuishawishi Fifa juu ya mpango wake wa ujenzi wa viwanja vya kutumia viyoyozi ili kuzuia joto la kipindi cha kiangazi.

Sheikh Mohamed Bin Hamad Al Thani ,kiongozi mkuu wa ujumbe wa Qatar  aliishukuru Fifa kwa kuwa na "mtazamo makini" alisema "Itakumbukwa kulikuwa na mshindano yenye tabia nchi kama Qatar, lakini kwa sababu ya dhana potofu ilikuwa ni vigumu kwao kupambana na hilo kuweza kudhihirisha kuwapo katika kiwango cha dunia"."Moja ya dhana hiyo ni kwa Qatar haiwezi kuandaa kwa kuwa hali ya hewa ni ya joto.Ni muhimu kuwa na imani kama Fifa ilivyofanya Afrika Kusini 2010 na muhimu kuondosha dhana hizi".
Akizungumzia dhana ya wanawake wa mashariki ya kati kutoruhusiwa kucheza mpira na kusema Qatar washaandaa mashindano yakulipwa ya wanawake.alisema"dhana ya unyanyasaji wa wanawake ,hiyo pia ni dhana potofu".

"Tutatimiza kwa shauku ili kuhakikisha kuwa ni hatua katika historia ya mashariki ya kati na Fifa". Sheikh Mohamed alisema uamuzi wa Fifa kuwa " ni kauli ya uaminifu na upenzi wa mchezo huo". Kwa niaba ya mamilioni ya watu wa Mashariki ya kati, shukrani kwa kutuamini,shukrani kwa kuwa na mtazamo makini. Na ahidi hatutawaangusha" alisema. Umuhimu wa yote (kwa watu wa mashariki ya kati) licha ya kuona kombe la dunia toka nje kwa umbali maelfu ya maili, hatimaye yapo mlangoni.....hatimaye tumekubalika kuwa ni kiungo muhimu kwenye ulimwengu wa soka"."Kwa Fifa, tunashukuru kwa kufahamu kuwa ni muda muafaka kwa mashariki ya kati , tuna tarehe kwenye historia" alisema.
Chanzo: Aljazeera English

Hivi ndivyo Qatar walivyoweza kuishawishi Fifa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...