Mtazamohalisi

Friday, December 10, 2010

Obama Kupigania Haki Za Mashoga

Rais Barack Obama amesema atahakikisha baraza la seneta la Marekani linafuta sheria inayowabana mashoga kujiunga na jeshi.Obama alitetea kwa kusema"sheria hii inadhoofisha usalama wa taifa,kuondoa utayari jeshini,na ni kinyume cha mfumo wa Marekani  kuhusu usawa ,uadilifu na haki".Amesema "haitakuwa ndiyo mwisho wa juhudi zao, kwani niliahidi kuiondoa sheria hii ya unyanyasaji".

Siku ya Jumatano ,Maseneta wa Republicans walizuia jitihada za kufuta sheria hii ya "usiulize,usiseme" inayowabana mashoga kujiunga katika huduma za wazi za kijeshi.Obama ,siku ya Alhamisi amewataka wajumbe wa seneta kufikiria tena uamuzi huo kabla  ya mwisho wa mwaka .

Matokeo ya kura yalikuwa 57-40,ni uchache wa kura 60 zinazohitajika ambazo chama cha Democratic kingeweza kushinda juhudi za chama cha Republican kuzuia sheria hiyo iliyodumu kwa miaka 17.

Robert Gates,Waziri wa Ulinzi wa Marekani kwenye utawala wa George Bush na Barack Obama aliwataka wajumbe kwa kuwauliza kama "sio sasa hivi? ,ni lini?" na Mike Mullen mwenyekiti wa maafisa jeshini ameunga mkono kufutwa sheria hiyo.

Takribani wanajeshi 13000 wanaume na wanawake walijitoa jeshini kutokana na sheria hii inayowabana mashoga kuto dhihirisha uhalisia wao pindi wakilitumikia jeshi.Tawimu zinaonesha kuna uungwaji mzuri toka jeshini kwa ufutwaji wa sheria hii.

Sheria hii ya "usiulize,usiseme" ilipitishwa rasmi mwaka 1993 na chama cha Democratic wakati wa utawala wa Bill Cliton.

Habari zaidi zinapasha kuwa Rais Obama amefanya makubaliano na chama cha Republican na kukubali kufuata sheria ya kodi ya utawala wa Rais George Bush.Katika makubaliano hayo utawapendelea zaidi watu wenye kipato cha juu kupata punguzo la kodi.

Obama ameonesha kutokubaliana na uendeleaji wa punguzo la kodi kwa watu matajiri,na kusema ni muhimu kutafuta suluhisho litakalo saidia walipa kodi wakipato cha kati wasilipe kodi zaidi ifikapo januari mwakani.

Kwa kufanya  hivyo,Obama anajaribu kuweka hali sawa kwenye ubaya.Maafisa wa serikali wanasema obama anaweka picha ya kuwa kiongozi mwenye kukubaliana na umoja wa vyama kwani ni muhimu katika kipindi hiki cha miaka miwili ijayo ya utawala wake kwani ni juhudi ya kutaka kuchaguliwa kwa mara nyengine.

Maseneta wa Republican wameahidi kutopitisha muswada wowote isipokuwa ule wa kuruhusu fedha serikalini ili kuweza kusaidia mamilioni ya wa amerika  hadi pale sheria ya punguzo la kodi kwa wenye kipato cha juu itakapo maliza muda wake.

Chanzo: aljazeera

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...