Nahodha wa Leeds Lucas Radebe |
ASHAMBULIWA
wakati nafasi ya kwenda kucheza mpira uingereza ilipokujamwaka 1994, Radebe aliipokea kwa mikono miwili. na uamuzi wake uhuo ulishinkizwa na tukio lilitokea miaka mitatu iliyopita katika maisha yake.
Radebe akiwa njiani kwenda kumnunulia mama yake vitu mbalimbali madukani,huku akishindikizwa na kaka zake ,,mmoja kati ya dada zake na mtoto wakike wa dada huyo walisikia mlio wa bunduki (bastola) ukilia , lakini kwakuwa ni kawaida katika kitongoji cha soweto kusikia mlio wa bunduki iliwafanya wasitilie maanani.kilichofuatia Radebe alisikia maumivu makali mgongoni ,huku akiona damu zikimchuruzika na mguu akichuchumia .Wazo la kwanza lililomjia mwanasoka huyu ni kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wake wa kusakata kabumbu.Radebe alikimbizwa hospitali na chakushangaza zaidi hakukuwa na kiungo chochote muhumu ambacho kiliadhirika ila risasi ilikuwa imengia mgongoni na kutokea sehemu ya kati ya kiuno chake.Haikujulikana ni nani aliyefanya shambulio hilo ila inasemekana kitendo chake cha kuhama timu ya ICL ya BOPHUTWASANA na kwenda kaizer chiefs kilihisiwa ndio sababu kuu.
' THE CHIEF' (jina alilopewa akiwa leeds united)
mwezi wa tisa mwaka 1994 ,radebe na PHILEMON ''chippa ''Masinga walihamia Leeds united .Radebe aliuzwa kwa paund za uingereza 250,000 kama msindikizaji tu wa Philemon ,sio kutokana nakipaji cha soka bali kuwa pamoja na philemon ili asijihisi upweke.
Kocha wa leeds kipindi hicho Howard Wilkinson kwa haraka aligundua kipaji cha Radebe kutokana na uwezo wake wa kutumia nguvu na akili na akamuhamishia nafasi ya mlinzi wa kati akitokea kama kiungo .
radebe alisumbuliwa na kuumia mara kwa mara kipindi alipojiunga Leeds na usumbufu mwingine ulitokana na kutoelewana na kocha Howard .mara tu alipofunzwa kocha Howard ,kocha mpya George Graham alimpa nafasi nyota huyu wa afrika ya kusini ang'are . nahii ilikuwa ni nafasi radebe alikuwa akiisubiri kwa hamu.
''THE Chief'' kama wanavyomwita washabiki wa leeds united kwa haraka alijiwekea jina na kuonyesha mchezo mzuri na kipaji cha hali ya juukwa ufahamu wake wa mfumo wa uchezaji wa leeds ,uwezo wake wa kukaba adui na jinsi gani alivyokuwa na utulivu pale anapopandana na adui wa timu pinzani.
mwaka 1998/1999 radede alichaguliwa kuwa nahondha wa leeds united na kocha george Graham (kuna wanao sema kocha Graham alimpenda radebe kutokana na uwezo wake wa kucheza kama mlinda mlango pale wanapokuwa na tatizo hilo katika mechi za ligi kuu).
Graham aliondoka Elland ambapo timu hiyo ina makao yake makuu na kocha mpya David O'leary alichukua nafasi yake mwezi wa nane mwaka 1998.Kocha huyu mpya kwanza alichofanya ni kuiomba bodi ya klabu ya Leeds kumpa Radebe mkataba wa kudumu mpaka atakapokuwa kipaji chake kimekwisha ,kocha huyu alikuwa msaidi wa kocha George Graham hivyo alijua ni jinsi gani muafrika kusini huyu mchango wake katika klabu na katika kauli yake alioielezea bodi ya Leeds ''Lucas anatakiwa awekwe kwenye jiwe na asiruhusiwe kuhama ''aliongeza.
""The Chiefs ''alitia mkataba wa miaka minne kuichezea timu ya leeds
na msimu wa 1998/1999 leeds ilifikisha mafanikio ya ke ya juu kumaliza nafasi ya nne katika ligi kuu ya uingereza hivyo kufaulu kuchezea kombe la bara la ulaya.na mwaka uliofuatia Leeds ilishika nafasi ya tatu na kufanikiwa kufika nusu fainali ya kombe la bara la ulaya .Mwaka 2000 radebe aliumia goti na kifundo cha mguu tattizo lililomfanya asicheze mpira kwa zaidi ya miaka miwli ...inaeendelea

Soma sehemu ya kwanza: http://mtazamojamii.blogspot.com/2010/11/mjue-lucas-radebe.html
No comments:
Post a Comment