Kinyang'anyiro Cha Unaibu Spika ni Ndugai - CCM Na Mustapha Akonay -Chadema
|
Job Ndugai-CCM
|
MBUNGE wa Kongwa, Job Ndugai amechaguliwa na CCM kugombea Unaibu Spika wa Bunge kwa kupata ushindi wa kura 197 za ndiyo kati ya 199 zilizopigwa, huku moja ikiharibikana nyingine ikimkataa. Alipigiwa kura ya ndiyo au hapana kutokana na wagombea wawilikujitoa, hivyo kubaki pekee.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alisema leo kuwa, mkutano wa Kamati ya Wabunge wa CCM imempa ushindi wa kishindo Ndugai, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita.
|
Mustapha Akonay -Chadema |
Kwa upande wake, CHADEMA imemteua Mbunge wake wa jimbo la Mbulu, Mustapha Akonay, kuwania unaibu spika.
Uchaguzi wa Naibu Spika wa Bunge utafanyika Jumanne ijayo, ambapo kesho saa 10 jioni ni siku ya mwisho ya kuwasilisha majina ya wagombea wa nafasi hiyo katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment