Mtazamohalisi

Thursday, February 10, 2011

Wasanii na Upepo wa Siasa

Mabadiliko ya kisiasa huacha wasanii  katika hali ngumu ya kuamua ikiwa wakumbatie utawala uliopo au kuunga mkono wnaaodai mabadiliko.

Msanii kama kioo cha jamii huacha athari pale anapounga mkono upande mmoja dhidi ya mwengine. Na hilo humuweka katika hali ya sintofahamu hasa pale upande anaoupigia debe ukiwa haukubaliki na wengi.

Wapo walionufaika na hilo wapo waliohatarisha maisha yao, nakupelekea kuanguka kimvuto na kazi zao kutothaminika.

Uchaguzi mkuu wa rais na wabunge ulifanyika oktoba ,2010 na kuwagawanya wasanii wetu kugawanyika pande mbili .Kambi ya Chama tawala CCM licha yakuwa na bendi yao ya TOT walikuwa na wasanii wengine kama Marlow na kwa upande wa upinzani hasa Chadema walikuwa na wasanii kama MR II maarufu kama Joseph Mbilinyi  ,Mbunge wa Mbeya Mjini na Fred Maliki maarufu Mkoloni.

Wapo waliokuwa  watazamaji na wapo waliobadili upepo mwishoni kama Nakaaya Sumari yaani muhimu uelewe ya kuwa kwa njia moja au nyengine upepo wa siasa unawaathiri sana wasanii kuliko mwananchi wa kawaida.

Hayo yakijiri nyumbani hali hiyo imewakuta hata wasanii wa nje,huko Misri ambako vuguvugu la siasa la kudai mabadiliko dhidi ya rais Hosni Mubarak umewaacha wasanii wakiwa ni wahanga wa upepo wa siasa.

Ni hivi karibuni msanii maarufu wa nchi hiyo Tamer Hosny ambaye alitumia nafasi yake kuwashawishi vijana kuilinda Misri kwa kuacha maandamano na kurudia maisha ya kawaida.Amejikuta kwenye hali ngumu mara upepo wa mabadiliko ulipomvuta hadi uwanja maarufu wa Ukombozi  yaani Tahrir Square (Liberization Square) nakujikuta akipata kichapo huku akijitetea kuwa alilanguliwa na Television ya Misri nakuwa hakuwa na nia mbaya na ameshatunga nyimbo ya Mapinduzi kuashiria kuunga mkono mabadiliko.

Tamer Hosny alivyo chezea kibano

Tamer Hosny moja ya nyimbo zake

Marlow na pipi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...