Kiongozi wa Kiroho Wa Kanisa Katoliki Papa Benedict XVI |
Papa Benedict XVI amesema ana wasiwasi wa mgogoro wa kiuchumi kwa mataifa tajiri kufanya ushirikiano utakao athiri mataifa maskini.Alikuwa akielezea ni makosa gani yaliyotikisa uchumi wa dunia na jinsi ya mataifa yatakavyo ondokana na mgogoro huo, alisema hayo mbele ya umati wa watu katika Viwanja vya Mtakatifu Petro siku ya Jumapili.Benedict alitoa kauli hiyo baada ya kilele cha mkutano wa G20 uliokuwa Seoul, ambao ulikuwa umetingwa na tofauti juu ya fedha na biashara.Anasema anafadhaishwa kwa pengo kubwa kati ya nchi matajiri na maskini, na kwamba mataifa yenye viwanda vingi huhamasisha utumiaji wa mfumo wa maisha wenye kuathiri mazingira na watu maskini..Benedict ameshauri uwiano mpya katika sekta ya kilimo, sekta ya viwanda na sekta ya huduma ili kufikia maendeleo endelevu hivyo hakutakuwa na ukosefu wa ajira au chakula
Chanzo: http://www.wtol.com/Global/story.asp?S=13503953
No comments:
Post a Comment