Baba Mtakatifu amekuwa akifanya mkutano usio wa kawaida, kwa kukutana na zaidi ya makadinali 100 kutoka kote duniani, ili kuzungumzia juu ya masuala mbalimbali kuhusiana na sera.
Kati ya masuala yanayojadiliwa ni uhuru wa kidini, kukandamizwa kwa Wakristo katika baadhi ya mataifa, na vile vile ugomvi dhidi ya Uchina.
Vile vile kashfa ya watoto kunyanyaswa kimapenzi ni jambo ambalo limo katika orodha ya yale yanayozungumzwa katika mkutano huo.Suala la kualikwa kwa maaskofu kutoka kanisa la Anglikana na kujiunga na kanisa Katoliki pia litajadiliwa.Mkutano huo utakamilishwa kwa Papa Benedict kuwaidhinisha makadinali 24 wapya, siku ya Jumamosi.
Kuna makadinali ambao wamesinywa sana na suala la kashfa ya ngono inayowahusisha watoto kuzungumziwa katika mkutano huo."Mimi nimechoswa kulizungumzia suala hili, linaniudhi mno", alielezea kadinali Javier Lozano Barragan kutoka Mexico, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Aliongezea kusema kwamba: "hii ni dhoruba kabisa katika vyombo vya habari".Msemaji wa Vatikana, Federico Lombardi, amesema hakuna matazamio ya habari kuu ambazo zitajitokeza katika mkutano wa Ijumaa.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2010/11/101119_cardinals.shtml
No comments:
Post a Comment