Mtazamohalisi

Friday, November 5, 2010

Hongera Rais Jakaya M.Kikwete na Dk.Ali Shein


                               Dk Jakaya Kikwete Pichani akipongezana na Dk Ali Mohamed Shein.

Katik hafla ya kutangaza matokeo ya Urais iliyomalizika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Lewis Makame, ameweza kutoa majumuisho ya matokeo hayo na kutangaza rasmi kuwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, ameibuka mshindi kwa kupata Asilimia 67.17 na n ameteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano. Makame alisema kuwa Rais Kikwete ameibuka mshindi baada ya kupata jumla ya kura Milioni 5, 276, 827 ambayo ni sawa na asilimia 61.17 % ya watu wote waliopiga kura, na kufuatiwa na mpinzani wake Dk Willbroad Slaa kupitia chama cha CHADEMA, ambaye ameibuka na jumla ya kura Mil.2, 271, 941 ambayo ni sawa na asilimia 20% ya wapiga kura. Ambapo jumla ya watu waliojiandikisha kupiga kura ilikuwa ni Milioni 20, 137, 303, wakati walijitokeza kupiga kura walikuwa ni Milioni 8, 6261.283 ambayo ni 42% ya waliopiga kura.
Tunategemea toka kwenu kupunguza changamoto zinazolikabili taifa kama vile Umaskini,Ujinga na Maradhi bila kusahau Ufisadi.Usafiri wetu ni ule ule, ila aina ya gari hubadilika kutokana na mazingira na hali ya barabara.

Dk.Slaa Historia ni Mwalimu


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema Dk.Willbrod Slaa

Historia inatufundisha kuwa katika mbio za ushindani kuna kushinda na kushindwa na kutokukata tamaa kufikia lengo ulilokusudia.
Unaweza kukubali lakini usikache,kwani hii inasaidia sana katika kujipanga upya kwa kutizama nini sababu yakutofikia lengo.

Kwanza kabisa nadiriki kukupongeza kama ni kiongozi pekee wa Vyama vya Siasa  aliyeweza kufanikiwa kuleta idadi kubwa ya wabunge toka Tanzania Bara ,kwani hili litasaidia kutoa changamoto kwa chama tawala CCM. Kwa kweli unastahiki sifa kubwa, kwa kuwa si mkamilifu ningependa kukumbusha historia ili kuepusha maswali juu yako ya kuwa ni mchanga kisiasa au unaendeleza chuki zisizokwisha.

Nisingependa kusema kuwa una uchanga wa kisiasa, kwa kuwa umelitumikia Taifa katika ngazi mbali mbali na hasa kiti cha Ubunge katika wilaya ya Karatu kwa muda wa miaka 15 ni kuwa unakubalika.
Hapo naweza kusema Mheshimiwa Dk.Slaa ni mpiganaji aliyekomaa bila kushindwa kwa muda wa miaka 15 na mwaka huu kuingia kwake katika mbio za Urais kumeleta muamko mpya na kuzoa viti vya ubunge  24 kwa chama chake cha Chadema, lengo ni mabadiliko na kwa hilo hajakosa kwani "Roma haikujengwa siku moja".

Nikiwa nina mifano ya kutosha ya hapa hapa nyumbani toka kambi ya vyama vya siasa hasa kupitia chama cha wanachi CUF na wagombea wao wa urais Maalim Seif S.Hamad na Prof.Ibrahim H. Lipumba toka mwaka 1995 hadi 2010.



Nikianza na Z'bar ni Maalim Seif aliyeshindaana na Marais wa 3 wa VISIWANI (Dk.Salmin,Dk.Karume na hatimaye Dk.Ali.M.Shein) kwa muda miaka 15.Kwa kipindi kirefu amekuwa ni alama ya upinzani Z'bar licha ya chaguzi zenye mizengwe mingi,hatimaye kutokubaliana na matokeo.
Mwaka huu 2010 ,Maalim Seif S. Hamad kafungua ukurasa mpya wa siasa za visiwani kwa kukubali matokeo.
 
Tanzania Bara ni Prof.Ibrahim H. Lipumba amegombea Urais kwa muda wa miaka 15,1995 alikuwa wa 3 kwa 6.43%,2000 alikuwa 2  kwa 16.26% nyuma ya Rais Mstaafu Benjamin W. Mkapa . Mwaka 2005 alikuwa 2  kwa 11.68 nyuma ya Rais Jakaya M.Kikwete. Katika hali zote amekubali matokeo,akiendelea kujiimarisha zaidi kisiasa licha ya kupandikizwa chuki za udini kwa chama chake na hatimaye kumkosesha kura za kutosha.
Uchaguzi Mkuu  2010, Dr.Jakaya Kikwete 61.17 %, Dr.Slaa 26.34 %, Lipumba 8.06 % , kufikia hapo nakupa hongera kwani ni asilimia ambayo kambi ya upinzani haijwahi kuifikia. Hii inaonesha kuna muamko mkubwa wa Watanzania na ni wito kwa watawala wote kuwa "ahadi ni deni" mtu ukikope lazima ulipe.
 
Nilichojifunza toka uchaguzi huu kama Mheshimiwa Dk.Slaa ataweza kusoma alama za nyakati, akubali matokeo na ajipange upya kwani analo somo toka kwa walio mtangulia. Waswahili wana msemo usemao "lisemwalo lipo kama halipo laja" , kashifa ulizo tuhumiwa imekuwa silaha kubwa ya kukumaliza.

Ikiwa si wewe  au ni nia mbaya ya wapinzani wako lazima ukemee vurugu na pia suala zima la udini, CCM inajivunia kwa kuwa inakubalika na waumini wa dini zote.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...