Osman Mohamud,19
Mohamed Osman Mohamud,mzaliwa wa somalia mwenye uraia wa Marekani amekamatwa na makachero wa FBI akiwa katika harakati za kulipumua bomu kwenye gari aliloliegesha karibu kabisa na mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiwasha taa katika mti wa Krismasi.
Taarifa za kijasusi ziliwafikia majasusi wa FBI toka kwa mtu wa karibu wa mtuhumiwa huyo nakufatilia nyendo zake kwa ushahidi zaidi,Mohamed aliwekwa kizuizini baada ya jaribio lake la kutumia simu kulipulia gari aliloliegesha kufeli kwa kujikuta amejilengesha kwa makachero wa FBI.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakama kuu ya Portland huko Oregon siku ya Jumatatu kwa mashtaka ya utumiaji wa silaha za maangamizi.Kwa mujibu wa sheria huenda mtuhumiwa akahukumiwa maisha na kulipa faini ya dola 250'000.
Wakati huo huo ,Waziri wa mambo ya nje wa somalia Mohamed Abdullahi Omaar amesema "serikali yake ipo tayari kutoa ushirikiano ili tukio kama hilo lisiweze kujitokeza tena.kwani tukio hilo si tu limeiathiri familia ya Mohamud bali pia bali hata wahanga waliokusudiwa kushambuliwa.
Maelfu ya wasomali wamepata hifadhi nchini Marekani tangu mwaka 1991 wakati utawala wa sheria ulipoanguka.
Chanzo: http://www.msnbc.msn.com/id/40389899/ns/us_news-security/
Full story Video