Mtazamohalisi

Thursday, November 18, 2010

Viongozi Wakuu wa Mihimili Ya Dola Tanzania

                                Mheshimiwa Mizengo Pinda aapishwa
                                           
   Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino leo Dodoma.

Wakuu wa Dola
 Toka shoto mbele ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais Serikali ya Muungano wa Dk.Mohamed Gharib Bilal,Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk.Jakaya Kikwete,Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mh.Seif Sharif Hamad.Toka shoto nyuma ni Jaji Mkuu wa Serikali ya Muungano Mh.Augustino Ramadhani,Spika wa Bunge laJamhuri ya Muungano Mh.Anne Makinda,Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mh.Idd Seif,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Jaji Fredrick Werema na Katibu Mkuu Kiongozi Mh.Philemon Luhanjo.

Viongozi wa Sasa na Wastaafu
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia mstari wa kwanza) baada ya kumwapisha,Ikulu ya Chamwino-Dodoma pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya pili Alli Hassan Mwinyi (wa kwanza kulia) na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Garib Billal (wa kwanza kushoto mstari wa kwanza), wengine ni kutoka kushoto mstari wa pili ni Mawaziri wakuu wastaafu John Samwel Malecela, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...