Mtazamohalisi

Sunday, November 21, 2010

Wafurahia Papa Kuruhusu Kondomu

Wapenda mabadiliko katika Kanisa Katoliki na makundi ya kupambana na UKIMWI yamefurahia matamshi ya Papa Benedikt kuwa matumizi ya kondomu sio mara zote ni ya nia mbaya.
Papa
Ruksa... Ingawa katika mazingira fulani tu.

Papa amesema matumizi ya mipira hiyo ya kiume inaweza kuhalalishwa kutokana na hali ilivyo, ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya HIV/UKIMWI.
Matamshi hayo yanayotarajiwa kuchapishwa katika kitabu wiki ijayo, yanaashiria kulegeza msimamo wake mkali wa zamani dhidi ya matumizi wa kondomu kupambana na HIV.
Vatikana kwa muda mrefu imekuwa ikipinga matumizi ya kondomu, kama njia ya kupanga uzazi.
Condom
Wanaharakati wamefurahishwa na uamuzi wa Papa

Hatua hiyo ilizua shutuma kali, hasa kutoka kwa wanaharakati wa kupambana na UKIMWI, ambao wanasema kondomu ni moja ya njia ambazo zimethibitishwa katika kupambana na maambukizi ya HIV.
Papa Benedikt katika ziara yake nchini Cameroon mwaka jana alisema kugawa kondomu kunaweza kuchochea maambukizi ya HIV, matamshi ambayo yalizua shutuma kutoka kwa nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo, katika matamshi yake ya hivi karibuni, amesema matumizi wa kondomu yanaweza kuhalalishwa katika mazingira fulani ya kipekee.
Ametoa mfano wa makahaba wa kiume, ambapo amesema matumizi wa kondomu kuzuia maambukizi ya UKIMWI yanaweza kuonekana kama kitendo cha mtu kuwa na majumuku, ingawa amesema kondomu "sio njia halisi ya kupambana na uovu wa kuambukiwa HIV".

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...