Mtazamohalisi

Tuesday, November 23, 2010

Uongozi wa Chadema Kuweni Makini

Mara nyingi nimetokea kupenda kile ninachokiita mabadiliko ya kisiasa Tanzania,kwa sababu mabadiliko hayo yatamsaidia Mtanzania mnyonge kwa sauti yake kusikika. Ni miaka takribani 19 toka mwaka 19991 uliporuhusiwa mfumo wa vyama vingi. Wakati asilimia 20 ilikubali kuanzishwa kwa vyama vingi asilimia 80 ilipinga suala hilo,hayo ni kwa mujibu wa matokea ya Tume ya Jaji Nyalali.Lakini kwa kuendana na mabadiliko ya dunia ,Serikali kwa wakati huo chini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi iliamua kwa moyo mmoja kuruhusu mfumo wa vyama vingi nakumbuka Rais Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa aliwahi kudokezea kuwa kutakuja utitiri wa vyama lakini hivyo vyote vitajichuja vyenyewe kutokana na sera zao kwa wananchi nakuita utitiri huo wa vyama kuwa ni "riziki dudu"  kwani kuwepo kwake kuna watakopata kula humo humo.

Nikija kwenye mada yangu nina wasiwasi na baadhi ya wanasiasa kwa  kutupa wakati mgumu hasa linapokuja suala la kiongozi wa chama kuhama chama kimoja kwenda chengine na huku nyuma akitoa kashfa nzito za kwanini amehama na wakati huo huo mwengine anatoka chama hicho na kuhamia chengine na kutoa kashfa kama hizo.Ni haki ya kiraia kuamua kuwa mfuasi wa chama unachokipenda lakini haingii akilini kuwa ni mtu makini unapokuwa ni mtu wa kuhama hama.

Hivi karibuni, baada ya Uchaguzi mkuu na kwa mara ya kwanza vyama vya upinzani hasa Chadema kupata viti vingi bungeni kwa kweli ni jambo la kujifahari. Ila nina patwa na wasi wasi kwanini kuna malalamiko kwa baadhi ya viongozi waliokuwa wa Chadema kulalamikia Uongozi Mkuu unawatupa mkono linapokuja suala la kuwasaidia wakati wanapokabiliwa na matatizo. Wiki hii Mwenyekii wa Chadema mkoa wa Mbeya  Bwana Sambwee Shitabala ametangaza  kujiuzulu ili kupisha uchunguzi ufanyike wa madai ya kupokea mlungula wa milioni 600 ili kukihujumu chama."Nimeamua kuachia ngazi kwa hiari yangu, nimetuhumiwa kuhujumu chama. Nimeambiwa nimehongwa mamilioni ya fedha na CCM ili nikikoseshe ushindi chama changu, naachia ngazi ili uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi ufanyike," alisema Bw. Shitambala. Aliendelea kwa kusema inaonesha chuki hii imepandwa kwa wanachama wa ngazi ya mkoa hadi Taifa nakutoatela mfano wa mwenyekiti wake Bwana Freeman Mbowe kutpokea simu yake"Inaonesha mbegu hii imepandwa na kukubalika kwa wanachama….nimempigia simu mwenyekiti wangu wa Taifa mara kadhaa lakini hapokei simu yangu, hili si jambo la kawaida, bora niachie ngazi," alisisitiza Bw. Shitambala.

Tukiachana na huyo leo hii Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema Bi Leticia Ghati Mosore ametangaza kujiuzulu kwa kile anachodai kutotahaminiwa cheo chake.Akizungumza na waandishi wa habari waliofika leo katika makao makuu ya  chama cha NCCR-Mageuzi  kumsikiliza akitangaza nia yake ya kukihama chama cha CHADEMA na kujiunga na NCCR-Mageuzi kwa madai kwamba amechoshwa  na taratibu nzima za uongozi wa juu wa chama hicho na kutopewa umuhimu wa cheo chake katika shughuli mbali mbali za kichama zikiwemo za baraza la wanawake ambalo yeye ndio mwenyekiti wake.
Hivyo basi ningeomba kwa uongozi mkuu wa Chadema kujiangalia tena kabla ya kushutumu kuwa kina hujumiwa kwani badala ya kujijenga na kuwa imara kisije tokea kama yale yaliyosababisha kusambaratika kwa chama kama NCCR-Mageuzi.Hakuna adui anaefurahia adui wake kufanikiwa lakini kabla huja toka nje hebu tizama ndani kwako au wewe mwenyewe kuwa hakuna makosa yatakayopelekea adui yako kutumia mwanya huo kukusambaratisha.

 Video hapo chini inaonesha mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Muheza alipojiunga na CCM,JE! Uongozi wa Chadema kuna nini nyuma ya pazia?.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...