Mtazamohalisi

Friday, November 26, 2010

Jeshi la Brazil Lapiga Hatua Katika Vita Dhidi Ya Madawa Ya Kulevya

Baada ya siku tano za operesheni dhidi ya makundi yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya,hatimaye jeshi la Brazil limefanikiwa kuutia mkononi kitongoji cha Vila Cruzeiro katika jiji la Rio De Janeiro.Jeshi la polisi la nchi hiyo lilipeleka vifaru,helikopta,jeshi la utunguaji na wanajeshi wenye silaha nzito,wanajeshi wa majini na pia kikosi cha  akiba cha wanajeshi 17'500 .

 Katika operesheni hiyo washukiwa 30 wa usafirishaji wa madawa ya kulevya waliuawa .Hali hii imesababisha makundi ya wahalifu wa madawa ya kulevya kurudi nyuma,na huku likitolewa tangazo kwa wakaazi wa vitongoji vya Vila Cruzeiro kutotoka nje.Wengi wa wakaazi wanasema haijawahi kutokea operesheni nzito kama hiyo na imewapelekea kuhisi kuwa wamo katika uwanja wa vita.

Wakati huohuo msemaji wa jeshi la Brazil wanasema operesheni hiyo haitakoma kwani lengo halijafikiwa la kurudisha hali kuwa kama kawaida,kwani vitongoji vya Vila Cruzeiro ni maarufu kwa kutawaliwa na ghasia na biashara haramu za madawa ya kulevya.

Mwaka 2012, Brazil inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michezo ya olimpiki na pia mwaka 2014 wanatarajia kuwa wenyeji wa kombe la dunia.
Mwezi Oktoba 2009 kundi la wahalifu  wa madawa ya kulevya lilitungua ndege ya polisi jirani na uwanja wa Maracana, moja ya viwanja vitakavyotumika katika kombe la dunia 2014,nakuua maafisa wa tatu.
Chanzo:Aljazeera
            

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...