Mtazamohalisi

Saturday, January 29, 2011

Sauti Ya Amerika na Mabadiliko Misri


Waandamanaji wakionesha hasira zao kwa Utawala wa Mubarak

Ilikuwa ni Ijumaa nzito kwa kipindi cha miaka  30 cha utawala wa Hussein Mubarak(82), siku ambayo wingu la mabadiliko ya siasa ulipofunga na kusababisha mpasuko wa radi uliotingisha si tu utawala wa Misri bali na tawala nyengine duniani.

Haikuwahi Mji wa Cairo kuwa moto tangu mapinduzi ya mwaka 1952,lakini mshuko wa Ijumaa wa january 28,2011 ulithubutu kuvunja duru za usalama za nchi hiyo na kuonesha dunia kile ambacho wanakipigania yaani mabadiliko.

Imetosha, ni kauli kuu ya waandamanaji kuashiria kukata tamaa na mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa na kijamii. Hali mbaya ya maisha kutokana na ukosefu wa ajira,gharama za maisha kupanda na uhuru wa kujieleza,rushwa na uasimu ndio vichocheo vilivyoamsha umma wa Misri na kumtaka Mubarak kuondoka madarakani.

Mwezi desemba Misri ilifanya uchaguzi wa wabunge wa duru ya pili na chama tawala cha National Democratic Party (NDP)   kujipatia ushindi mnono wa 80% na upinzani kujipatia 20%.Hata hivyo kelele za kubatilisha matokeo hayo ambayo upinzani ulisusia toka duru ya kwanza ya uchaguzi mwezi novemba linalifanya bunge hilo kuwa ni la chama kimoja bila mwakilishi toka upinzani.

Hapo jana utawala wa Marekani  ambao ni mshirika mkuu wa utawala wa Mubarak ambayo hutoa kiasi cha Dola 1.5 bilioni kila mwaka, umeitaka Misri kuheshimu uhuru wa kujieleza na kuruhusu maandamano,pamoja na kuwaacha huru waandamanaji na kuruhusu mitandao kufanya kazi huku ikiisisitiza Misri kusikiliza kilio cha Umma na kukubali mabadiliko.

Kutokana na shinikizo la ndani na nje ya nchi,Rais Mubarak ametangaza kulivunja baraza lake la Mawaziri na kuunda jipya hali yeye akiwa bado kiongozi mkuu atakae endeleza mabadiliko ya nchi katika muelekeo wa Misri Mpya.

Septemba,2011 kutakuwa na uchaguzi wa Rais wa Misri ambao kwa hali ilivyo upepo wa siasa unaelekea kuwa mbaya kwa Mubarak na chama chake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...