Mtazamohalisi

Thursday, December 23, 2010

Umuhimu wa Vyeti Vya Kuzaliwa

Mara nyingi,umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa hauji mpaka kuwe na jambo la kisheria linalokukabili. Kutokana na umuhimu wake ni vyema wazazi na vijana mliofikia umri wa kujitegemea kuanza kulifikiria, kwani athari yake unaweza kupoteza haki zako za msingi kama raia na hata kutiliwa shaka uraia wako.

Naandika haya kwa ushahidi mkubwa wa mambo yalivyojitokeza nyuma hasa ukiwa unakumbuka kunyang'anywa uraia wa Jenerali Twaha Ulimwengu na Marehemu Ali Nabwa.

Kuhifadhi cheti cha kuzaliwa ni muhimu kwani ushahidi wake unatambulika kisheria,kumbuka wakati wa mchakato wa kutafuta wagombea wa ubunge wa CCM kulijitokeza mgogoro baada ya Mgombea toka Nzega kukataliwa na chama chake kwa madai ya kutokuwa raia.

 Hussein Bashe ilimlazimu si tu kumuhatarisha uanachama wake katika CCM bali kubwa kuliko yote ni haki nzima ya uraia kama Mtanzania, kwa kuwa alithibitisha uraia wake wa kuzaliwa kwa kigezo hicho Idara ya Uhamiaji ilijiridhisha kuwa ni raia halali.

Leo hii,licha ya uthibitisho wa kuzaliwa ,masomo na nyadhifa mbali mbali alizopitia Marekani, Rais Barack Obama wapo watu wanaodai kutaka uthibitisho wake wa kuzaliwa huko Honolulu,Hawaii.

Picha inayonijia ni kuwa kuhifadhi vyeti vya kuzaliwa ni muhimu kwa ajili kupata haki zako za msingi za kisheria kama raia.

Ijapokuwa Obama na familia yake wapo Hawaii ambako ina aminika ndiko alikozaliwa  katika mapumziko ya Krismasi,lakini swali la uhalali wa cheti cha kuzaliwa kwake huko Honolulu ,Hawaii bado ni tete.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...