Mtazamohalisi

Thursday, December 23, 2010

Benitez apigwa chini Inter

Inter Milan ya Italia imethibitisha kuwa imemfukuza kazi meneja Rafael Benitez, miezi sita tu baada ya kuteuliwa kuiongoza klabu hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Benitez kutaka kuungwa mkono ndani ya bodi ya wakurugenzi kununua wachezaji, kufuatia klabu hiyo kushinda kombe la dunia la vilabu, kwa kuifunga TP Mazembe siku ya Jumamosi.

Badala yake, Inter, ambayo inasuasua katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ya Serie A, imeamua kumfukuza kazi Benitez.
Benitez
'Jino la pembe' Moratti na Benitez
Benitez alichukua kazi hiyo San Siro kutoka kwa Jose Mourinho.

Mourinho, ambaye aliondoka Inter na kwenda Real Madrid ya Uhispania, aliiongoza timu hiyo kuchukua ubingwa wa ligi ya Italia na klabu bingwa Ulaya msimu uliopita na kumuachia Benitez kazi ngumu ya kufuata nyayo zake.

Benitez, alichukua majukumu ya San Siro wiki moja baada ya kuondoka Liverpool ya England Juni 3. Ingawa amekuwa na majeruhi kadhaa, lakini imeonekana kuwa mbinu zake hazijaweza kumsaidia.

Ingawa Inter ina kiporo cha mechi mbili dhidi ya timu zilizo juu yake, imeshinda mechi sita tu kati ya mechi 15 za ligi.
katika kutetea ubingwa wao wa klabu bingwa, Inter imeweza kumaliza katika nafasi ya pili ya makundi, nyuma ya Tottenham ya England, na kuiacha katika wakati mgumu kwani itapambana na Bayern Munich katika raundi ya timu 16.

Ingawa Inter imeshinda Kombe la Dunia la Vilabu kwa kuichapa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, mafaniko hayo hayakumfanya Benitez kutotoa dukuduku lake baada ya mchezo huo wa fainali
Soma zaidi.....BBC


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...