Mtazamohalisi

Monday, November 22, 2010

Urusi Ya Laani Bwana Bout(Merchant Of Death) Kupelekwa Amerika


Bwana Victor Bout akiwa chini ya ulinzi nchini Thailand
                                                                                        
Baraza la mawaziri la Thailand limefikia muafaka wa kumpeleka uhamishoni  nchini Amerika ,mfanyabiashara wa silaha raia wa Urusi Bwana Victor Bout  maarufu kama Merchant of Death baada ya mvutano wa kisheria wa muda mrefu wa ama kumsimamisha kujibu mashtaka  au kumuachia huru.

Bwana Victor Bout ,43  afisa wa zamani katika jeshi la anga la urusi alikamatwa Hotelini mjini Bangkok mnamo  mwezi march 2008 kwa ushirikiano wa maafisa wa usalama wa Thailand na Mawakala wa ujasusi toka Amerika.

Anashutumiwa   kusambaza silaha zilizo chochea vita ya kiraia katika nchi za kusini mwa Amerika,Mashariki ya Kati na Afrika miongoni mwa wateja wake ni Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor,na kiongozi wa Libya Muumar Gadhafi- na pia Angola pande zote mbili(MPLA na UNITA) .

Kitendo hicho cha uhamisho wake toka Thailand kwenda Amerika kumeibua vita ya kidiplomasia baina ya Urusi na Amerika.Wakati serikali ya Amerika imefurahia kumpata Bwana Bout ambaye yupo katika orodha ya watu hatari duniani,Urusi wamelaani kitendo hicho nakusema haki haikutendeka kwani Bwana Bout ni mtu safi.


Baada ya hilo tukio hebu angalia movie hii utajua ni hatari gani ya wafanyabiashara wa silaha wasivyojali watu maskini hasa Afrika. Angalia trailer kisha click link hapo chini uangalie full movie.

                              LORD OF WAR BY NICOLAS CAGE
           
Na hii link ni vipande vya filamu nzima:   http://www.youtube.com/watch?v=1KGu0FMDJfk&feature=related                                                                                                             

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...