Mtazamohalisi

Monday, November 22, 2010

Kesi Ya Uhalifu Wa Vita Dhidi ya Bemba ni Jumatatu Hii

Kiongozi wa chama cha upinzani MLC, Jean-Pierre Bemba akipiga kura Kinshasa, DRC 2006.
 Kiongozi wa chama cha upinzani MLC, Jean-Pierre Bemba akipiga kura Kinshasa, DRC 2006.
 
"Jean-Pierre Bemba atafikishwa mahakamani Jumatatu, Novemba 22, kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulotendwa CAR kati ya 2002 na 2003." amesema bi Daphne Anayiotos
Kesi ya uhalifu wa vita dhidi ya makamu rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean Pierre Bemba, inanaza The Hague, Uholanzi Jumatatu kufuatana na Mahkama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC.
Msemaji wa ICC Daphne Anayiotos, ameiambia Sauti Ya Amerika kwamba Bermba anashtakiwa kwa tuhuma za uhalifu ulotendwa na wapiganaji wake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Bi Anayiotos amesema, "Jean-Pierre Bemba atafikishwa mahakamani Jumatatu, Novemba 22, kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulotendwa CAR kati ya 2002 na 2003."
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, iliwasilisha mashtaka hayo mbele ya ICC 2004. Wakosowaji wanashuku na mashtaka hayo wakidai kwamba Rais Ange-Felix Patasse ndiye aliyemualika Bembe kumsaidia kuzima uwasi nchini mwake.

 Chanzo:Voa  swahili

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...