Mtazamohalisi

Wednesday, November 24, 2010

Nigeria Yakamata Shehena Ya Madawa Ya Kulevya



Maofisa wa kupambana na madawa ya kulevya wanigeria wamekamata shehena ya madawa ya kulevya ambayo yalikuwa yamefichwa ndani ya spea za magari kwenye gari iliyosajiliwa iran,maafisa hao walipata msaada wa kijasusi wa shehena hiyo toka Marekani.Inakisiwa thamani ya madawa hayo ni dola milioni 9.9 ambao ulikuwa unasafirishwa kuelekea Ulaya.

Mwezi uliopita serikali ya Nigeria ilikamata shehena 13 za silaha haramu zikiwemo roketi,mizinga na bunduki zinazosemekana toka Iran. Baada ya kukamata shehena hizo Serikali ya Nigeria iliwasilisha malalamiko dhidi ya Iran katika Umoja wa Mataifa.
Umoja wa mataifa umeiwekea Iran vikwazo vya kusafirisha silaha nje ya nchi.

Nigeria imekuwa ndiyo njia kuu ya kusafirisha madawa kwa nchi za Amerika, Ulaya na Afrika .

Wakati huo huo, Serikali ya Gambia mekatisha uhusiano wake na serikali ya Iran nakuwataka maafisa wa ubalozi wa Iran kuondoka ncho hiyo katika muda wa masaa 48.Haijaelezwa sababu ya hatua hiyo nini lakini duru za habari zinahusisha na tukio la mwezi uliopita la serikali ya Nigeria kukamata shehena 13 za silaha zilizosafirishwa kiharamu , ambazo zinadaiwa zikipelekwa Gambia.
Hata hivyo Afisa wa ngazi ya juu wa Iran Alaeddin Borujerdi amesema hatua hiyo ya Gambia imechukuliwa kutokana na shinikizo kutoka Marekani.

 Chanzo:CNN, BBC-Swahili

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...