Ratiba za mechi mbalimbali nchini Scotland zinakabiliwa na hatari ya kuvurugika wiki ijayo baada ya waamuzi wa daraja la kwanza kupiga kura kuidhinisha mgomo wao.
Waamuzi hao wa Scotland wamekatishwa tamaa na jinsi wanavyoandamwa msimu huu na hata kutishiwa maisha.
BBC nchini Scotland imegundua kuwa waamuzi wana wasiwasi na pia kushushwa heshima yao na baadhi ya vilabu na hata watu binafsi.
Kumekuwa na ongezeko la vitisho kwa usalama wao kutokana na kuchukiwa na jamii.
Uamuzi wa kugoma ulifikiwa na katika mkutano wa chama cha waamuzi uliofanyika siku ya Jumapili mchana, wengi wakiunga mkono.
Kuna mechi sita za Ligi Kuu ya Scotland zilizopangwa kuchezwa mwishoni mwa wiki ijayo.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment