Mtazamohalisi

Saturday, November 27, 2010

Rais Obama Apigwa Kiwiko Akicheza Mpira Wa Kikapu

Ashonwa kwa nyuzi 12
Aliyemuumiza anaitwa Rey Decerega


Kutoka vyanzo mbali mbali vya habari leo asubuhi Rais wa Marekani Barack Obama amepatwa na jeraha la mdomoni kufuatia kupigwa kiwiko na mchezaji wa upande mwengine katika mazoezi ya Mpira wa Kikapu ambayo yalijumuisha ndugu na marafiki zake.

Rais Obama ilibdi ashonwe kwa nyuzi 12 baada ya kujeruhiwa na Rey Decerega.Taarifa toka Ikulu ya Marekani imemnukuu Bwana Decerega akisema"leo amefahamu kama rais ni mahiri na ni mwanamichezo mzuri.Nimefurahi kucheza nae Mpira wa kikapu asubuhi hii.Natumaini atarudi tena kiwanjani hivi karibuni".Bwana Rey Decerega ni mfanyakazi wa taasisi ya kihispania katika Congress.

Ikulu ya Marekani imetoa majina ya ndugu wa rais waliocheza nae Mpira wa Kikapu na miongoni mwao ni mpwa wake Avery Robinson,Waziri wa elimu Arne Duncan na Reggie Love  msaidizi binafsi wa Obama ,ambaye anacheza katika chuo kikuu cha Duke,lakini haikuetoa majina ya wachezaji wengine.

Habari nyengine inatupasha kuwa askari mstaafu  amewekwa kizuizini kwa kutishia kumuua rais Obama.
Akutwa na silaha 16 nyumbani kwake ,ni mstaafu mwenye miaka 78

Image: Michael Stephen Bowden
Aliyetishia kumuua Rais Obama,Askari Mstaafu
Bwana Michael Stephen Bowden,78
Taarifa hiyo ya kiapo cha kuua imetolewa na idara ya ujasusi imesema Bwana Michael Bowden aliwekwa kizuizini  mwanzoni mwa mwezi huu.Wakati Bowden alipomuambia muuguzi mmoja katika zahanati maalumu ya wastaafu iliyopo South Carolina kwamba"nafikiri kwenda Washington,kumuua rais kwa kuwa hajafanya jitihada za kuwasaidia wamarekani weusi". Alitamka hayo wakati muuguzi alipomuuliza ya kuwa kama alishawahi kujitoa muhanga,baadaye iligundulikana Bwana Bowden hana hatia ya kujitoa muhanga.
Chanzo: http://www.msnbc.msn.com/id/40379129/ns/us_news-crime_and_courts/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...