Kutokana na utoaji wa leseni za biashara kwa bei ya mwaka 2001
Uamuzi wowote wa mahakama utakaomtia hatiani huenda ukahatarisha nafasi yake
Waziri Mkuu wa India Dk.Manmohan Singh |
Duru za siasa nchini India zimeingia katika sura mpya, baada ya Jumanne hii kwa Waziri Mkuu wake Bwana Manmohan Singh kutakiwa na mahakama kuu kujibu maswali ya kwanini imemchukua miezi 16 bila kumfungulia mashtaka Waziri wa mawasiliano aliyejiuzulu hivi karibuni kwa kile kinachoitwa kashfa ya uuzaji wa leseni kwa makampuni ya mawasiliano kwa bei ya mwaka 2001.Ombi la kumtaka waziri mkuu kumchukulia hatua za kisheria waziri wa mawasiliano lilitolewa na Mbunge wa upinzani.Uamuzi wowote wa mahakama utakaomtia hatiani Bwana Singh huenda ukamuia vigumu kubaki katika nafasi yake.
Kati ya mwaka 2007 na 2008, waziri wa mawasiliano Bw.Raja alitoa leseni kwa makampuni 85 kati ya 122 yaliyo omba kwa bei ya chini iliyopelekea hazina kupata hasara ya dola bilioni 39,kwa mujibu wa maafisa waliochunguza. Hata hivyo Bwana Raja alijiuzulu kwa shinikizo lakini amekana kuwa na makosa.
Kwa mujibu wa mkaguzi mkuu wa mahesabu anasema makampuni mengi ya mawasiliano yalificha habari,kughushi nyaraka na pia kutumia njia za ulaghai kupata leseni.
Bunge la India limesimama kwa kile upande wa upinzani unachodai tume ya uchunguzi wa kashfa ya utoaji wa leseni ya mawasiliano.Shughuli za serikali haziathiriki kutokana na kusimama kwa bunge.
India ndio inayoongoza duniani katika sekta ya mawasiliano ambayo inakuwa kwa kasi kwa takribani ya watumiaji milioni 700
Chanzo : http://english.aljazeera.net/news/asia/2010/11/20101123751335817.html
No comments:
Post a Comment