Mtazamohalisi

Sunday, November 21, 2010

50 Cent anakuja na kali"Things Fall Apart"

Sanaa ni kazi hasa pale unapotakiwa kuivaa tabia halisi ya kile unachoigiza, na kazi kubwa ni kuwa tayari kwa gharama yoyote hata iwe kujibadilisha muonekano na hadhi yako.
                              
Mathalani tumeshuhudia mara nyingi kwa kuona waigizaji kama Will Smith alivyofanikiwa kuigiza kama Mohamed Ali na Beyonce kupunguza uzito kwa pauni 20 kwa siku 10.
Lakini wote hao tisa, kumi ni curtis"50 cent" Jackson mwenye uzito wa pauni 214 alipojipunguza kwa pauni 54 ili kufikia lengo la pauni 160 kwa ajili ya filamu yake mpya "Things Fall Apart". Kwa muda wa wiki 9 amekuwa katika mlo maalumu ili kuuvaa uhalisi wa mchezaji wa American Football ambaye aliugua ugonjwa wa kansa.

Hebu angalia picha alizotoa wakati akiitangaza filamu hiyo mpya, kisha ujiulize kama itawezekana kwa msanii wa bongo kuweza kuigiza mathalani hata sehemu ya harakati za Mwalimu Nyerere.
                                                                                 
                                                                                            50_cent_things_fall_apart_skinny_02

50_cent_things_fall_apart_skinny_01


  50_cent_buff                      

Katika picha ya kwanza na ya pili ndivyo atakavyoonekana katika filamu hiyo.
Na picha ya tatu jinsi 50 cent akiwa katika muonekano halisi.
Kazi kwenu wasanii, ujumbe umefika  .                    
                                                  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...