Mauaji ya kujitolea Muhanga
Zaidi Ya watu 35 wauawa
Zaidi ya watu 35 wameuawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua wakati waumini wa kishia walipokuwa kwenye shughuli zao kwenye mji wa Chabahar kusini mashariki mwa Iran.
Afisa wa Shirika la Hilali nyekundu Mahamoud Mozafar amesema mshambuliaji huyo alijiripua katika eneo la kati ambapo waumini hao walikuwa wakifanya ibada ya kuadhimisha siku ya mwisho ya Ashura.
Kundi la Jundallah limedai kuhusika na shambulio hilo.Kundi hilo katika kipindi cha muongo mmoja uliyopita limekuwa likihusika na mashambulio kadhaa dhidi ya vikosi vya usalama nchini Iran.
Mkuu wa kamati ya mambo ya Nje ya Bunge la Iran Alaeddin Borujerdi amezishutumu idara za kijasusi za Uingereza na Marekani kuhusika na shambulio hilo.
Mjini London Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Alistair Burt amesema ameshtushwa na shambulio hilo na kwamba inalaani vikali.
Chanzo: Dw
No comments:
Post a Comment