Ikiwa ni muendelezo wa mikutano mingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kama wa Kyoto,Copehagen na kwa mara nyengine mkutano wa Cancun, Mexico umeendeleza kile kinachoonekana kufeli kwa makubaliano baina ya nchi tajiri na maskini kuhusu upunguzaji wa uzalishaji wa kaboni kwa digrii 4 kabla 2060.
Inasemekana 20% ya uzalishaji wa kaboni dunia inatoka Nchi zinazoendelea kutokana na uchomaji misitu hali nchi zilizoendelea zikiwa vinara wa uzalishaji wa kaboni kutokana na matumizi ya viwanda.
Benki ya dunia kama mdhamini wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani imekutwa na kashfa ya kutokuwa makini katika mambo yake hasa linapokuja suala la uchumi na nchi matajiri.Ni taasisi inayoendeshwa na mataifa tajiri na kuzinyima sauti nchi maskini kwenye maamuzi makubwa ya uchumi wa dunia.
WIKILEAKS ilipiga msumari wa dau pale ilipotoa kashfa kuhusu nchi matajiri kutumia pesa za kuchangia kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa kwa nchi maskini kama rushwa ili kudhoofisha lengo la nchi tajiri kupunguza uzalishaji wa kaboni. Pesa hizi zinatolewa na nchi tajiri na kusimamiwa na Benki ya dunia,taasisi ambayo nchi maskini hazina imani nayo kutokana na uendeshwaji wake kutokuwa wa kidemokrasia.
Kabla ya mkutano wa Cancun nchi kama Marekani ilitishia kujitoa mkutanoni kama matakwa yake hayata timizwa,Japan nayo ikisisitiza utekelezwaji wa makubaliano ya Kyoto hali Urusi ikishinikiza kuwa kama Japan haita ahidi zaidi ya makubaliano ya Kyoto basi na wao hawako tayari.
Ingawa kulikuwa na shinikizo kubwa toka Marekani,nchi zinazoendelea na Ngo's ilikufikia mkataba mwengine unaolingana na ule wa Kyoto.Lakini juhudi hizo hazikuleta mabadiliko yoyote na kubaki kukubalina kutokubaliana.
Ikiwa maafikiano hayatafikiwa ili kutekeleza lengo la upunguzaji wa uzalishaji wa kaboni duniani kwa digrii 4 kabla ya mwaka 2060,watu na viumbe wengi duniani wataendelea kuathirika na mabadiliko ya hali ya hali ya hewa ambayo hawakuya sababisha kutokana na usaliti wa viongozi wao.
Mkataba wa Kyoto ndiyo mkataba rasmi unaotambulikana na umoja wa mataifa. na kutofikiwa makubaliano baina ya nchi tajiri na maskini ,mkataba wa Kyoto unaelekea kufa taratibu.
Chanzo: Conspiracy
Athari ya mabadiliko ya hali hewa(The day after tomorrow)
No comments:
Post a Comment