Mtazamohalisi

Monday, December 13, 2010

Ahmadinejad amfuta kazi Mottaki

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amemuachisha kazi Waziri wa Mambo ya Nje Manouchehr Mottaki Jumatatu, wakati waziri huyo akiwa kwenye ziara huko Senegal.

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amemuachisha kazi Waziri wa Mambo ya Nje Manouchehr Mottaki Jumatatu, wakati waziri huyo akiwa kwenye ziara huko Senegal.

Bwana Ahmadinejad alimuachisha kazi Mottaki Jumatatu na kumteuwa mkuu wa nyuklia nchini Iran, Ali Akbar Salehi kama waziri mpya wa mambo ya nje kwa sasa. Shirika rasmi la habari la Iran Mehr linaripoti kwamba Bwana Ahmadinejad alituma barua kwa Mottaki akimshukuru kwa kazi yake.

Salehi anajulikana kama mshirika wa karibu wa rais. Zaidi ya mwaka mmoja uliopita vyombo vya habari vya Iran viliripoti mifarakano kati ya Mottaki na wabunge wa Iran. Ripoti hizo zilisema wabunge wa Iran walisema kwamba Mottaki hakuwa mahiri au mwakilishi shupavu kwa Iran kwenye jukwaa la kimataifa.

Walimshinikiza Mottaki kujiuzulu kama vikwazo zaidi vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa vingewekwa katika kujibu program ya nyuklia ya nchini humo, na mzunguko wa nne wa vikwazo hivyo viliwekwa mwezi Juni. Duru za kimataifa zinaonesha vikwazo hivyo vinaharibu mno uchumi wa Iran.

Chanzo: Voa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...