Mtazamohalisi

Saturday, October 16, 2010

Mtazamo halisi(Hekima,Maarifa na Busara)

Wengiwetu tumelala Wengiwetu tumeamka,basi zinduka kwa "Mtazamohalisi" .
Mtazamohalisi ni blog yenye lengo la kuelimisha jamii,kwakufungua Maarifa mapya
yenye kujenga.
Kwa kuwa mtandao wa habari ni mpana, ushirikiano ni muhim ili kufikia lengo
lakufikisha ujumbe kwa jamii.
Kuna ambayo tunajua basi pokea,na kwako kuna ambayo unajua tutapokea.
" Jamii moja ,hujengwa kwa umoja".

Kwajina lake manani,muumba yetu dunia
hakika yake nishani,viumbe kujivunia
akili zakila fani,hakika kajaalia
twakuomba rahmani,ukweli kusimamia.
"Ni mtazamo halisi,wastara haumbuki".

Ni mtazamo halisi,wastara haumbuki
tumia yako nafasi,fursa hii shiriki
kutoa hakufilisi,hasa kutoa kwahaki
hidaya ya almasi,pokea kwa halaiki.
"Ni mtazamo halisi,wastara haumbuki".

Hekima kubwa thamani,maarifa na busara
mazuri yalo maoni,hujenga ikawa dira
yawe yatokea pwani,yawe yatokea bara
kwa kuwa jambo yakini,hakuna zuri hasara
"Ni mtazamo halisi,wastara haumbuki".

Karibu hii baraza,tujue yanayojiri
elimu yako mwangaza,si vema ikawa siri
shauri kutengeneza,tupate kujiajiri
wema wako kuwekeza,haitokuwa sifuri.
"Ni mtazamo halisi,wastara haumbuki".

Kaditama ndiyo mwisho,mtazamo kufikisha
ijenge leo kwa kesho,makosa kusahihisha
mbaya roho ya korosho,mazuri kuyafifisha
mtazamo suluhisho,sasa taa tumewasha.
"Ni mtazamo halisi,wastara haumbuki".

1 comment:

  1. huu ni mtazamo wa kila mwanajamii, hakika mtazamo huu haubagui wala hauchagui. kikubwa i kuandika chochote kilicho kichwani mwako, bora tu usikengeuke maadili ya mtanzania.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...