Mtazamohalisi

Tuesday, December 7, 2010

Fungate Afrika Kusini Lageuka Mauaji

Katika hali isiyo kawaida bwana harusi amelipia mauaji ya mke wake, hayo yamejitokeza leo katika mahakama moja mjini capetown,Afrika kusini mara baada ya mtuhumiwa  wa mauaji  kukiri kulipwa sehemu ya makubaliano ili kutekeleza zoezi hilo la mauaji.

Zola Tongo ambaye ni dereva teksi amejitetea kwa kudai kuwa Shrein Dewan raia wa Uingereza alimuhadaa  ili amuue mke wake mpya Ani Dewan raia wa sweden siku baada ya kuwasili Afrika kusini.Mwili wa Ani Dewan ulipatikana siku ya pili katika kitongoji cha Gugulethu ambacho ni maarufu kwa uhalifu katika jiji la Capetown,Afrika kusini.Marehemu alikutwa ameuawa kwa risasi iliyopigwa toka nyuma ya shingo.

Tongo alidai kuwa Shrein Dewan alimtaka amtafutie mtu ambaye ataweza ufanikisha mauaji ya mke wake na kwamba atawalipa kila mmoja randi 50000(US$ 7000) lakini wamejikuta wakiambulia randi 1000(US$ 145).

Akiongea katika mahojiano na jarida moja nchini Uingereza ambalo kwa muda wa majuma kadhaa lilikuwa likimshutumu Shrein Dewan kwa mauaji hayo,msemaji wake alikana shutuma hizo.Na kwamba Shutuma zilizotolewa na dereva teksi kuwa Shrein alihusika katika mauaji ya mkewe  si kweli, kwani vithibitisho vya mwili wa marehemu vilivyotolewa  na polisi havikumuhusisha Shrein na mauaji hayo.Na kwamba mamlaka husika haikuwahi kuwasiliana na Shrein ambaye alirudi Uingereza mara baada ya mwili wa mkewe kupatikana.

Mthunzi Muhanga ,msemaji wa ofisi ya mshtaki mkuu wa Afrika kusini  amesema kutokana na ushahidi uliyojitokeza siku  ya jumanne suala la ombi  la kupelekwa Afrika kusini bwana Shrein linawezekana" jambo ambalo tunalifikiri kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea.

Mtuhumiwa wa mauaji Zola Tongo amehukumiwa miaka 18,na anatarajiwa kutoa uthibitisho wa watuhumiwa wengine wawili ambao waliwekwa kizuizini mara baada ya mauaji ya Ani Dewan.

Akitoka nje ya mahakama huku akibubujikwa na machozi Mzazi wa Marehemu Ani Dewan,Bwana Vinod Hindocha ambaye alikuwepo wakati wa hukumu hiyo aliishukuru mamlaka ya Afria kusini iliyofanya uchunguzi wa kesi hii ,wananchi wa Afrika kusini na watu wote duniani walioiunga mkono familia yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...