Mtazamohalisi

Showing posts with label Mambo na Vijambo. Show all posts
Showing posts with label Mambo na Vijambo. Show all posts

Wednesday, January 26, 2011

Undugu Wamtoa Machozi Oprah Winfrey


Kwa muda wa miaka 25,mwanamama  Oprah Winfrey amebahatika kuwaunganisha watu mbali mbali katika kipindi chake maarufu cha Oprah show .

Lakini safari hii imekuwa kwa upande, katika hali ya kushangaza amejikuta anakutana na dada yake wa mama mmoja ambaye alichukuliwa kimalezi wakati yeye akiwa miaka 8.

Kwa kiasi fulani tukio hili litamliwaza Mama huyu kwani kwa kipindi kirefu alikuwa ana dai yakuwa ana asili ya Kizulu kutokana na vipimo vya DNA, hali wakuu wa kabila hilo lililopo nchini Afrika kusini wakikanusha kwa vizazi vyao kuchukuliwa utumwa kwenda Marekani.

Thursday, December 23, 2010

Umuhimu wa Vyeti Vya Kuzaliwa

Mara nyingi,umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa hauji mpaka kuwe na jambo la kisheria linalokukabili. Kutokana na umuhimu wake ni vyema wazazi na vijana mliofikia umri wa kujitegemea kuanza kulifikiria, kwani athari yake unaweza kupoteza haki zako za msingi kama raia na hata kutiliwa shaka uraia wako.

Naandika haya kwa ushahidi mkubwa wa mambo yalivyojitokeza nyuma hasa ukiwa unakumbuka kunyang'anywa uraia wa Jenerali Twaha Ulimwengu na Marehemu Ali Nabwa.

Kuhifadhi cheti cha kuzaliwa ni muhimu kwani ushahidi wake unatambulika kisheria,kumbuka wakati wa mchakato wa kutafuta wagombea wa ubunge wa CCM kulijitokeza mgogoro baada ya Mgombea toka Nzega kukataliwa na chama chake kwa madai ya kutokuwa raia.

 Hussein Bashe ilimlazimu si tu kumuhatarisha uanachama wake katika CCM bali kubwa kuliko yote ni haki nzima ya uraia kama Mtanzania, kwa kuwa alithibitisha uraia wake wa kuzaliwa kwa kigezo hicho Idara ya Uhamiaji ilijiridhisha kuwa ni raia halali.

Leo hii,licha ya uthibitisho wa kuzaliwa ,masomo na nyadhifa mbali mbali alizopitia Marekani, Rais Barack Obama wapo watu wanaodai kutaka uthibitisho wake wa kuzaliwa huko Honolulu,Hawaii.

Picha inayonijia ni kuwa kuhifadhi vyeti vya kuzaliwa ni muhimu kwa ajili kupata haki zako za msingi za kisheria kama raia.

Ijapokuwa Obama na familia yake wapo Hawaii ambako ina aminika ndiko alikozaliwa  katika mapumziko ya Krismasi,lakini swali la uhalali wa cheti cha kuzaliwa kwake huko Honolulu ,Hawaii bado ni tete.


Saturday, December 11, 2010

Obama Na Kisa Cha Lipstick

Atumia ushawishi wa Cliton kukubalika

Katika hali isiyo kawaida Rais wa Marekani ,Barack Obama amejikuta katika wakati mgumu mbele ya waandishi wa habari. Tukio hili limetokea leo mara baada ya kikao cha dharura na rais wa zamani wa marekani Bill Cliton.

Kama kawaida ilifika muda wa kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya mazungumzo yao.
Na ndipo likaibuka jibu la Obama kumtaka Bill Cliton kuelezea umuhimu wa kukubaliana na Rais Obama juu ya makubaliano yake na chama cha Republican kuhusu kuendelea kutumia sheria ya upunguzaji wa kodi kwa watu wakipato cha juu iliyotumika wakati wa utawala wa George Bush.

Ila jambo lilochukua picha nzima ni tukio la Rais Obama kumuwacha pekee Bill Cliton kukabiliana na maswali ya waandishi wa habari huku yeye akienda kujumuika na Mkewe. Rais Obama aliomba dharura kwa Bill Cliton kwa kumwambia aendelea kwani mkewe Michelle Obama  alikuwa akimsubiri muda mrefu na anachelea kumkwaza.


Swali ambalo wengi wanajiuliza vipi Obama amuwachie Bill Cliton kuendelea kujibu maswali ya waandishi wa habari katika hali ngumu kama hii.Wachambuzi wamekifananisha kitendo hicho na kisa cha lipstick.
Inasemekana  ilitokea mwaka 1961 wakati Muigizaji wa Filamu Eddie Fisher alipomruhusu mkewe  Elizabeth Tailor kwenda Rome akijumuika na muigizaji mwenzie Richard Burton kwenda kuigiza katika filamu gonga hapa Cleopatra  hali yeye akibaki Los Angeles.

Hatimaye mapinduzi ya mapenzi yakaibuka,kwani kitendo cha Fisher kubaki Los Angeles kilimkutanisha na muigizaji wakike wa TV ya Ernie Kovac,Sue Kennedy .Na huko Rome Elizabeth Taylor alifungua ukurasa mpya wa mahusiano wa mapenzi na Richard Burton.

Nini kiliutambulisha ulimwengu juu ya mapinduzi haya ya mapenzi ni kitendo cha Sue Kennedy kuchukua Lipstick nyumbani kwa Elizabeth Taylor na Richard Burton na kumpa rafiki yake wa karibu na hapo ndiyo kosa kwani rafiki yake aliitoa siri kwa shangazi yake ambaye ni mwandishi.

Hatimaye talaka zikatembea na uhusiano mpya wa ndoa ukachanua baina ya Elizabeth Taylor na Richard Burton nahuku Eddie Fisher akijichukulia mazima Sue Kennedy.

Chanzo: michelemalkin.com

Obama Na Odinga Mpira Kati

Odinga: Hii  Imekaaje



Obama:Dini Au Dunia

Tuesday, December 7, 2010

Fungate Afrika Kusini Lageuka Mauaji

Katika hali isiyo kawaida bwana harusi amelipia mauaji ya mke wake, hayo yamejitokeza leo katika mahakama moja mjini capetown,Afrika kusini mara baada ya mtuhumiwa  wa mauaji  kukiri kulipwa sehemu ya makubaliano ili kutekeleza zoezi hilo la mauaji.

Zola Tongo ambaye ni dereva teksi amejitetea kwa kudai kuwa Shrein Dewan raia wa Uingereza alimuhadaa  ili amuue mke wake mpya Ani Dewan raia wa sweden siku baada ya kuwasili Afrika kusini.Mwili wa Ani Dewan ulipatikana siku ya pili katika kitongoji cha Gugulethu ambacho ni maarufu kwa uhalifu katika jiji la Capetown,Afrika kusini.Marehemu alikutwa ameuawa kwa risasi iliyopigwa toka nyuma ya shingo.

Tongo alidai kuwa Shrein Dewan alimtaka amtafutie mtu ambaye ataweza ufanikisha mauaji ya mke wake na kwamba atawalipa kila mmoja randi 50000(US$ 7000) lakini wamejikuta wakiambulia randi 1000(US$ 145).

Akiongea katika mahojiano na jarida moja nchini Uingereza ambalo kwa muda wa majuma kadhaa lilikuwa likimshutumu Shrein Dewan kwa mauaji hayo,msemaji wake alikana shutuma hizo.Na kwamba Shutuma zilizotolewa na dereva teksi kuwa Shrein alihusika katika mauaji ya mkewe  si kweli, kwani vithibitisho vya mwili wa marehemu vilivyotolewa  na polisi havikumuhusisha Shrein na mauaji hayo.Na kwamba mamlaka husika haikuwahi kuwasiliana na Shrein ambaye alirudi Uingereza mara baada ya mwili wa mkewe kupatikana.

Mthunzi Muhanga ,msemaji wa ofisi ya mshtaki mkuu wa Afrika kusini  amesema kutokana na ushahidi uliyojitokeza siku  ya jumanne suala la ombi  la kupelekwa Afrika kusini bwana Shrein linawezekana" jambo ambalo tunalifikiri kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea.

Mtuhumiwa wa mauaji Zola Tongo amehukumiwa miaka 18,na anatarajiwa kutoa uthibitisho wa watuhumiwa wengine wawili ambao waliwekwa kizuizini mara baada ya mauaji ya Ani Dewan.

Akitoka nje ya mahakama huku akibubujikwa na machozi Mzazi wa Marehemu Ani Dewan,Bwana Vinod Hindocha ambaye alikuwepo wakati wa hukumu hiyo aliishukuru mamlaka ya Afria kusini iliyofanya uchunguzi wa kesi hii ,wananchi wa Afrika kusini na watu wote duniani walioiunga mkono familia yake.

Friday, November 12, 2010

Malikia Elizabeth ajiunga na facebook, na kukutana na kashfa

Malikia Elizabeth wa Uingereza
Hivi karibuni, Queens Elizabeth II alijiunga na facebook na siku moja baada ya kujiunga katika tovuti hii ya jamii ukurasa wake ulijaa maoni machafu kutoka kwa watu . Walengwa wakuu walikuwa Carmilla na Charles na picha zao zilishambuliwa kwa maoni ya matusi.
Ukurasa  huu wa Familia ya Kifalme ya Uingereza, ulizinduliwa Novemba 8 pamoja na akaunti ya Twitter na Flickr. Wakati watu zaidi ya 220,000 "waliipenda", picha 28 katika albamu zilishambuliwa kwa maoni ya aibu na matusi.Familia ya kifalme ina wafuasi zaidi ya 75,500 kwenye Twitter na huweka picha mpya katika akaunti yake  ya Flickr kila siku. Pia ina channel kwenye Youtube
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...