Mtazamohalisi

Saturday, December 25, 2010

Zitto Kabwe:Aeleza Kulikoni Yake


Mbunge wa Kigoma kaskazini,
Mheshimiwa Zitto Kabwe

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe amesema kuwa hajapewa sumu kama ilivyokuwa imedaiwa huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu anayeweza kufanya hivyo.Pia mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, amesema hana nia wala mpango wa kukihama chama hicho.

Bw. Kabwe aliyasema hayo juzi wakati akiwahutubia mamia ya wananchi Mkoa wa Kigoma katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kawawa ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji.

Alisema kuwa migogoro inayoendelea ndani ya chama chake isiwafanye wananchi wa Kigoma kuwa na hofu yeyote na hata yale yanayoandikwa na vyombo vya habari pia yasiwanyime rah,a waendelee kukisimamia chama chao.

"Wananchi wenzangu msiwe na wasiwasi, mimi ni mzima kabisa, yameandikwa mengi katika vyombo vya habari, mara nimepewa sumu, nataka niwahakikishie hizo habari si za kweli, mimi sijapewa sumu na hakuna binadamu anayeweza kunipa sumu, tuendelee kufanya kazi na kukijenga cha chetu," alisema Kabwe.

Siku za karubuni kumekuwapo na mgogoro ndani ya CHADEMA kutokana na mbunge huyo kutofautiana na wabunge wenzake kuhusu msimamowa kususia hotuba ya Rais jakaya Kikwete bungeni, hali iliyosababisha chama hicho kuundama kamati ya kuzungumza naye kumpa ushauri.hatua hiyo ilichukuliwa siku chache baada ya wabunge wenzake kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, kama Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Wakati wabunge hao wanachukua uamuzi huo, Bw. Kabwe aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan akisumbuliwa na tumbo, na baadhi ya vyombo vya habari vililiripoti kuwa amelishwa sumu, ingawa madaktari walisema ni tumbo lake lilikuwa tu limechafuka.

Katika hatua nyingine Zitto aliitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI) kuitisha uchaguzi wa meya wa Kigoma/Ujiji haraka ndani ya wiki mmoja uliokuwa umesimamishwa wiki iliyopita kutokana na mgogoro wa mgawanyo wa madiwani wa viti maalumu.

"Halmashauri zingine tayari zimeshafanya uchaguzi na wamepata meya, na kazi za kuleta maendeleo wameshaanza, sasa wao wanapozidi kutucheleshea sisi kufanya uchaguzi, wajue na kazi ya kuleta maendeleo katika manispaa yetu inazidi kuchelewa," alisema Bw. Kabwe.

Mbunge huyo amewataka viongozi wa vyama mbalimbali nchini kutumia fursa walizozipata katika kuleta maendeleo ya jamii na sio kuendekeza uadui na serikali kuu.
Chanzo: Majira

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...