Hayo ni kwa mujibu wa kitabu kipya kilichozinduliwa hii leo na professa wa chuo kikuu cha Havard Calestous Juma.
Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais Mwai Kibaki wa Kenya(shoto) na Pierre Nkurunziza wa Burundi kwenye mkutano wa usalama wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa,leo Arusha. (Picha na Freddy Maro) |
Ripoti hiyo itawasilishwa kwa viongozi wa Afrika siku ya Ijumaa nchini TanzaniaMarais wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanafanya kikao kuzungumzia usalama wa chakula pamoja na suala la mabadiliko ya hali ya anga.
Akizungumza na BBC kabla ya mkutano huo, Professa Juma alisema viongozi wa Afrika hawana budi kutambua uhusiano wa kilimo na uchumi wa Afrika.
''Ni jukumu la viongozi wa Afrika kuuboresha uchumi wao na hiyo inamaanisha kuanza kutumia teknonologia ya kisasa katika kilimo'', alisema.
Kwa mujibu wa Professa Juma, uzalishaji wa chakula duniani unaendelea kuongezeka lakini katika maeneo mengi ya Afrika hali ni tete licha ya kuwepo na ardhi ya kutosha ya kilimo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment