Mtazamohalisi
Monday, November 29, 2010
Kuuawa Mwanasayansi wa Nyuklia-Iran Yazishutumu Marekani na Israel
Mashambulio mawili ya bomu la Kuegeshwa kwenye gari nchini Iran
limeua mwanasayansi wa nyuklia na kujeruhi mwengine.
Mahmoud Ahmednajad,Rais wa Iran amezishutuma nchi za Marekani na Israel kuwa zipo nyuma ya mashambulio mwawili yaliotokea leo na kuua mwanasayansi mmoja wa myuklia na kujeruhi mwengine.
Amesema"Pasi shaka kuna mkono wa wazayuni na mataifa ya magharibi uliohusika" katika mauaji haya. Lakini amesisitiza mashambulizi ya kushtukiza hayata izuia Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia.
Mohamed Reza Rahimi,Makamu wa Rais wa Iran ameishutumu israel nakuwaita kuwa "wamebeba silaha za ugaidi".Mwaka huu Iran imeshuhudia ikiuawa wanasayansi wake wawili wa nyuklia
Wakati hayo yakijiri, leo tena imetolewa kashfa ya simu ikimuhusisha Mfalme Abdullah wa Saudi Arabi pamoja na chi za Ghuba kuishawishi Marekani kuishambulia Iran kuharibu mpango wake wa nyuklia.Kasjfa hiyo imetolewa na Jarida la WIKILEAKS.
Rais wa Iran,Mahmoud Ahmednajad amesema" hawatilii nyaraka hizo maanani, kwa kuwa hazina uzito wa kisheria .Iran na majirani zake ni marafiki.Kitendo hicho kiovu hakina athari za mahusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi". Aliendelea kusema"hizi nyaraka zimeandaliwa na kutolewa na serikali ya marekani kwa ajili ya mpango maalumu ili kutekeleza azima yake.Ni sehemu ya vita vya ujasusi na hiyo haina athari ya kisiasa kama wanavyotaka".
Chanzo: http://english.aljazeera.net/news/middleeast/2010/11/20101129131235776706.html
Labels:
Kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment