Mtazamohalisi

Monday, November 29, 2010

Mheshimiwa Sitta Nakugeukia Okoa Kambi Ya Upinzani Bungeni

Mheshimiwa Samwel Sitta
Waziri Afrika Mashariki
Mdahalo wa juzi  kuhusu mustakbali wa kambi ya upinzani bungeni baina ya Mheshimiwa Freeman Mbowe  wa Chadema na Mheshimiwa Hamadi Rashid wa CUF umeniacha na jibu la matumaini.Kwa mujibu wa serikali kivuli ya upande wa upinzani kambi ya Chadema inadai ina haki ya kuwakilisha wapinzani hali pia CUF kwa upande wake inadai mamlaka hayo kwani inawakilisha sauti ya vyama vyengine vya upinzani vyenye wabunge.

Ni katika mdahalo huo tulipata sura ya kambi hizi mbili za upinzani na misimamo yao,Mheshimiwa Freeman Mbowe alisema alimtaka Mheshimiwa Hamad Rashid waunde serikali kivuli ya kambi ya upinzani na ikatokea tofauti ya kimtazamo kwani Chadema walitaka vyama vyengine visishirikishwe wakati CUF walisimama kwa kusisitiza ushirikishwaji wa vyama vyengine vyenye wabunge.

Hebu Tujikumbushe kidogo kwa maneno ya Mheshimiwa Hamad Rashid aliposema kuwa ni aliyekuwa Spika Mheshimiwa Samwel Sitta ndiyo aliyoasisi kwa kuwa kutanisha Mheshimiwa Hamad Rashid na Mheshima Wilbrod Slaa lakuwataka kuunda serikali kivuli ya kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa kambi ya upinzani haikuwa na sauti ya umoja.

Kwanini Mheshimiwa Sitta wa CCM tena Spika wa Bunge alichukua uamuzi huo nakuwataka wapinzani wa CCM kujiunga pamoja kuelekeza mashambulizi bungeni,hali mashambulizi yenyewe yata hatarisha uhai wa chama chake. Hayo yote aliyafanya kwa makusudi kwa sababu ya mapenzi ya nchi yake kwani kutokana na sauti ya upinzani japokuwa ni wachache wakishirikiana na vilio vya wananchi(Peoples Power) vita dhidi ya ufisadi vitafanikiwa.Ni ishara njema ya kiongozi mwenye hekima na kiukweli bunge lile la tisa lilitetemesha vigogo na kuamsha hisia za kizalendo kwa wananchi,matokeo yake si tu Chadema kuibuka na viti vingi bungeni hata CUF wamefanikiwa kupata viti viwili vya Ubunge Tanzania bara hii imevunja kawaida na kuipa homa chama tawala.

Leo narudi kwako ukiwa kama Waziri wa Afrika Mashariki nikijua fika utapokea pole toka kwa majirani zetu kwa kutofanikiwa kutetea kiti chako cha uspika. Na ndio huko pia kutakako kukumbusha kazi yako ya kuitaka Tanzania iwe nchi safi dhidi ya ufisadi na katiba mpya kuwa hujaimaliza. Kwani ni tegemeo lako kuwaambia nchi nyengine za Afrika mashariki licha ya kuanguka katika uspika nina fahari ya kuwa mafisadi wamefikishwa mahali hawana pa kujificha nakwamba nchi yangu ina katiba mpya kama wenzetu wa KENYA.Na kwamba leo hii unasimama mbele yao kifua mbele, ukiwatamkia Tanzania ina utawala wa sheria na kuwataka majirani zako ili kufikia lengo la soko la pamoja lazima muige toka Tanzania.

Hayo yote yanawezekana kwa kuwa siri ya umoja wa kambi ya upinzani uliyo uasisi imefungua macho wa Tanzania basi ndiyo wewe  unaeweza kuikoa kambi hii. Kwani bunge hili  tunategemea kutoa changamoto zitakazolifikisha Taifa katika muelekeo mzuri hasa pale kambi ya upinzani kwa idadi ya wabunge wao wa mwaka huu na wale wa CCM wanaopendelea mabadiliko watakapo ungana na kuwashinda mahafidhina.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...